Saturday, April 26, 2014

BEFORE I DIE SEHEMU YA 22

BLEEDING HEART SEHEMU YA 22

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 22

SERENA SEHEMU YA 22

Saturday, April 19, 2014

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 17






            " jana nilianza kuelezea maisha yangu katika shule ile ya kimataifa ya wasichana iliyoko nje kidogo ya jiji la Nairobi nilikohamishiwa baada ya wazazi wangu kuhofia pengine ningeweza kujiingiza katika vishawishi kutokana na uzuri wangu kwani tayari nilikuwa nimeanza kupevuka na kuwa gumzo mtaani.Nilielezea namna Christine Kumuhoza ambaye alikuwa ni rafiki yangu mkubwa pale shuleni alivyonipa ushawishi wa kutafuta rafiki wa kiume.Alinielezea raha anazopata toka kwa rafiki yake wa kiume.Mimi sikuwa nikihitaji kuwa na rafiki wa kiume kwa wakati huo kwa sababu hilo ni moja ya jambo ambalo lilichangia mimi kuhamishiwa nchini kenya katika shule ya wasichana ili kunilinda na wanaume wakware.Siku zote niliwaheshimu na kuwasikiliza sana wazazi wangu.Sikutaka kufanya yale mambo ambayo hawakutaka niyafanye.Na moja ya mambo ambayo hawakutaka niyafanye nikiwa shuleni ni kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.Niliachana na Christine nikapanda kitandani kulala.Siku hiyo sikuweza kupata usingizi nikifikiria maneno ambayo aliniambia Christine kuhusu kuwa na rafiki wa kiume.Taratibu nilijikuta nikianza kushawishika kuwa na rafiki wa kiume .Nilitaka nizipate hizo raha ambazo Christine alisema kwamba huwa anazipata toka kwa huyo rafiki yake .Sikuwahi kufanya mapenzi na sikufahamu yakoje ila kupitia filamu ambazo nilikuwa nikitazama na kupitia vitabu vya hadithi ambavyo nilikuwa nikisoma nilijua kwamba mapenzi ni matamu .Nilianza kutamani kujaribu siku moja kufanya mapenzi hayo kama wenzangu.Kila siku mawazo hayo ya kuwa na rafiki wa kime yakawa yananijia kichwani lakini nikajitahidi kuyapuuza na kuongeza juhudi katika masomo.Hatimaye tukafunga shule na kurejea nyumbani kwa mapumziko.Kila tulipofunga shule baba alikuwa na kawaida ya kututumia tiketi za ndege na ndivyo alivyofanya safari hii.Likizo ilikuwa nzuri kwani furaha ilirejea tena nyumbani kwetu baada ya watoto wote kurejea nyumbani.Wazazi waliongeza ulinzi mkubwa kwangu na sikutakiwa kutoka na kwenda kuzurura hovyo wakihofia pengine ningeweza kuingia katika vishawishi kutokana na uzuri wangu uliozidi kuongezeka kila siku.Muda mwingi niliutumia kwa kujisomea mwenyewe nyumbani.Wakati mwingine Savanna rafiki yangu ambaye naye anasoma nchini Kenya lakini shule tofauti na mimi alikuwa akija nyumbani tukasoma pamoja.


SERENA SEHEMU YA 17

Friday, April 18, 2014

BEFORE I DIE SEHEMU YA 16

BLEEDING HEART SEHEMU YA 16

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 16

SERENA SEHEMU YA 16

Thursday, April 17, 2014

BEFORE I DIE SEHEMU YA 15

BLEEDING HEART SEHEMU YA 15

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 15

SERENA SEHEMU YA 15

Wednesday, April 16, 2014

BEFORE I DIE SEHEMU YA 14

BLEEDING HEART SEHEMU YA 14

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 14

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi