“Jambo
la tatu ambalo nataka kukufahamisha ni kwamba kabla hatujakwenda Arusha kwa
dhumuni la kuwaeleza wazazi kuhusu uhusiano wetu,nilikupa ahadi kwamba chochote
kitakachokwenda kutokea huko mimi sintakuacha kamwe.Pamoja na mambo yote
yaliyotokea na kusababisha tukatengana ,bado napenda kukuhakikishia kwamba
ahadi niliyoiweka bado nitaitimiza.
Joe ulikuwa ni mwanaume wa kwanza kukupenda na siku zote niliamini wewe ndiye malaika wangu.Hata baada ya kuachana nawe bado umeendelea kuwa mtu muhimu sana katika maisha yangu ambaye sina wa kumlinganisha naye sasa na maisha yote.Ninapenda kukufahamisha kwamba kwa kuwa wewe ndiye uliyekuwa mwanaume wa pekee kabisa maishani mwangu na kwa sasa hauko nami tena sina sababu yoyote ya kutafuta mwanaume mwingine kwa sababu sintaweza kumpata mwingine kama wewe.Kwa maana hiyo nimeamua kwa hiari yangu kujiunga na shirika la masista wa Mtakatifu Anna.Nimeamua kuwa mtawa na kuyatoa maisha yangu kwa bwana.Nitamtumikia yeye peke yake.Wiki ijayo nitaingia katika konventi ya shirika na kuanza mafunzo na baada ya miaka miwili nitafunga nadhiri yangu ya kwanza.” Paula akasema huku akitabasamu.

0 comments:
Post a Comment