Friday, April 18, 2014

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 16




akawaza huku akiichukua kompyuta yake ndogo toka katika mkoba wake mdogo akaikunjua akaiwasha na kuiweka mapajani mwake na kisha akafungua sehemu ya kuandikia akaanza kuandika.
.




            " wazazi wetu walikuwa wakitupenda sana sisi watoto wao na walitupa kila tulichokihitaji.Hakuna tulichokitaka toka kwa wazazi wetu tukakikosa.Mimi nilikuwa na gari langu peke yangu la kutembelea pamoja na dereva maalum wa kunipeleka kila mahala ninakotaka kwenda.Wadogo zangu niliowapenda sana mpacha Martin na Yvone nao walikuwa na gari lao la kuwatembeza sehemu mbali mbali pindi tuwapo likizo.Kwa ujumla maisha yalikuwa mazuri sana .Tuliishi kwa furaha kubwa na hatukufahamu nini maana ya shida.Nyumba yetu ilitawaliwa na upendo mkubwa sana.Toka tukiwa wadogo wazazi wetu walitufunza kuwapenda watu na kujipenda sisi wenyewe.Pamoja na utajiri waliokuwa nao wazazi wangu bado walikuwa ni watu wa watu.Waliwapenda na kuwajali watu wote na hivyo sisi kama watoto wao tulifuata mfano wao.Mtaani tulikuwa sawa na watoto wengine wote wambao wazazi wao hawakuwa na uwezo mkubwa kiuchumi kama wa kwetu.Hatukubagua marafiki.Wazazi wetu walifanya kila waliloweza kuhakikisha kwamba tunakua tukiwa katika malezi mazuri.Tulijifunza kazi zote za nyumbani na kusaidiana na dada yetu wa kazi Pamela.Dada huyu tulimpenda sana kana kwamba ni ndugu yetu wa damu.Haikuwa rahisi kukubali kwamba Pamela alikuwa ni msichana wa kazi kutokana na jinsi tulivyomuheshimu na kumpenda.Siwezi kumsahau dada huyu kwa sababu ndiye msichana wa kazi aliyenilea mimi toka nikiwa mdogo na baadae akawalea pia wadogo zangu .Mungu alimjalia dada Pamela kupata mume na kwa sasa ana nyumba yake na watoto wawili.Pamela ni mtu ambaye yuko katika simulizi ya maisha yangu.Ni mtu ambaye nitaendelea kumuenzi milele na milele.Kwa ujumla naweza kusema kwamba tulikuwa ni familia ya kutiliwa mfano kutokana na aina ya maisha tuliyoyaishi .Familia yetu iliishi maisha ya tofauti kabisa na familia nyingi za kitajiri zinavyoishi."  Msichana yule akasimama tena kuandika akanywa funda kubwa la mvinyo na kisha akaendelea.
            "Kwa kadiri nilivyozidi kukua ndivyo uzuri wangu ulivyoongezeka.Katika umri wa miaka kumi na mitatu nilikuwa tayari na umbo la kupendeza sana na kila mtu alinisifu kwamba mimi ni mzuri.Si kwamba ninajisifu lakini ni kweli mimi ni msichana mzuri sana na kwa hilo siwezi kuficha.Ninajifahamu kuwa ni mzuri na ninamshukuru Mungu kwa zawadi hii aliyonipa ya uzuri wa sura,umbo hadi moyo.Wazazi walipoona dalili za kuanza kupevuka wakaekelekeza macho yao yote kwangu kwani waliamini uzuri niliokuwa nao ni sawa na ua lenye asali tamu ambalo huwavuta nyuki wengi kuliendea.Uzuri wangu wa sura na umbo viliwafanya wazazi wangu wawe na wasi wasi mkubwa kwamba ungeniletea matatizo toka kwa wanaume wakware wenye kupenda mabinti wadogo.Sifa za uzuri wangu zikaanza kuvuma mtaani  na kuwafanya wazazi wangu wazidi kuogopa pengine ningeweza kuharibikiwa kwani nilikuwa na marafiki wengi sana ninaowajua na nisiowajua.Kwa kuogopa nisiweze kuingia katika makundi mabaya wakaamua kunihamisha shule na kunipeleka katika shule moja ya kimataifa inayomilikiwa na masista wa kanisa katoliki nje kidogo ya jiji la Nairobi Kenya.Niliwapenda sana wadogo zangu na hivyo ikanilazimu kuhama pamoja nao.Hapo ndipo nikaufungua ukurasa mpya wa maisha yangu.Nilikutana na wasichana ambao walikuwa wapya kabisa katika maisha yangu wenye makuzi na tabia tofauti lakini niliweza kuwazoea kwa muda mfupi kutokana na jinsi nilivyokuwa nimefunzwa namna ya kuishi na aina zote za watu.Miezi miwili ya mwanzo nilikuwa tayari nimekwisha fahamika shule nzima kutokana na uchangamfu wangu .Hakuna mtu ambaye hakuwa akinifahamu pale shuleni.Darasani nilikuwa ni msichana mwenye akili nyingi pia.Pamoja na kubadili mazingira na kubadili mtaala wa masomo lakini nilijitahidi sana kwa kuwa katika namba tano za juu kwa kila mtihani na majaribio tuliyoyafanya.Hii ilinizidishia marafiki wengi nikafahamika na kupendwa zaidi.Kati ya marafiki zangu wote rafiki yangu mkubwa alikuwa ni msichana mmoja toka Rwanda aliyeitwa Christine kumuhoza.Msichana huyu alikuwa ni mzuri na kwa hilo siwezi kuacha kumsifia.Wanafuzi wenzetu walikuwa wakijaribu kutulinganisha mimi na yeye lakini siku zote mimi niliibuka mshindi kwa sababu pamoja na uzuri wake lakini bado hakuweza kunifikia mimi.Sijisifu ninapoweza kusema kwamba mimi ndiye niliyekuwa msichana niliyeongoza kwa uzuri shuleni kwetu.Nilikuwa ni msichana mzuri wa sura,umbo na tabia pia.Christine yeye alikuwa ni msichana mrefu mwembamba na mwenye sura ya kung'aa.Kila vazi lilikuwa likimkaa vyema.Alikuwa na sauti nzuri sana na mara zote akicheka au akitabasamu hutatamani kuacha kumuangalia au kumsikiliza.Pamoja na uzuri wake huo lakini Christine alikuwa na tabia moja ya kujiona na kujivuna sana kutokana na utajiri wa familia yake.Baba yake alikuwa ni mmoja kati ya wafanya bashara wakubwa sana nchini Rwanda.Christine hakuwa na marafiki wengi zaidi ya wale wachache anaotoka nao nchini Rwanda.Baada ya mimi kuhamia katika shule ile nikawa ndiye rafiki yake mkubwa na taratibu nikaanza kumbadilisha na kumfunza namna bora ya kuishi na watu.Nashukuru Mungu alikubaliana nami na kuanza kubadilika na katika muda mfupi akawa na marafiki wengi pia.Hili likamfanya awe karibu sana na mimi.Nilikuwa rafiki yake mkubwa mno."
            " Sogea nikwambie rafiki yangu.Wewe ni msichana mkubwa sasa na unatakiwa kuwa na boyfriend.Mimi huyu boyfriend wangu ananipa raha sana.Ananipenda na mimi pia ninampenda mno.Nikirudi Kigali kwa likizo amekuwa akinipa kampani kubwa.Huwa tunatoka na kwenda kupata chakula na kutembelea sehemu mbali mbali..Sikufichi Lina huwa ninafurahi sana na siku zote ninaomba shule ifungwe haraka ili niweze kuwa naye karibu.Hata mimi wazazi wangu hawataki kusikia nina boyfriend lakini mimi huwa ninafanya mambo yangu kwa siri kubwa.Halafu kitu kingine ninachotaka kukufundisha ni kwamba ukiwa na boyfriend si lazima mfanye mapenzi.Kuwa wapenzi si lazima mfanye mapenzi.Mimi na huyo boyfriend wangu tangu tumefahamiana tumefanya mapenzi si zaidi ya mara tano lakini bado tunapendana sana na kuheshimiana.Ananiheshimu mimi kama mwanafunzi bado na hataki kitu chochote kibaya kinitokee.Hata tukifanya mapenzi huwa anatumia kinga ili kunilinda na mimba na magonjwa ya kuambukiza .Ni yeye ndiye aliyenitoa usichana wangu na kunifanya niipate raha ile waipatayo wanawake wote duniani.Joseph ndiye aliyenifundisha mapenzi na ndiye mtu pekee ambaye ninamuwaza kila dakika.Nakushauri Lina tafuta boyfriend ili uone raha yake.Lakini utafurahi sana kama ukimpata mwanaume ambaye atakupenda.Wanaume wengi siku hizi wanapenda sana wanafuzi kwa ajili ya kuwachezea basi na si kwa mapenzi ya kweli.Ukimpata mtu ambaye ana lengo la kukuchezea na kukuacha hapo ndipo mambo kama ya mimba hutokea lakini kama ukimpata mwenye mapenzi ya kweli kama huyu wangu basi utaifurahia hii dunia.Mapenzi ni matamu sana Lina.Ouh Gosh ! when we make love he drives me crazy...huwa najihisi siko kabisa katika ulimwengu huu .Huwa ninasikia raha ya ajabu mno.Ninapotaka kufika kileleni siwezi kuelezea raha ninayoisikia...Ouh Lina I find myself screaming and screaming..and screaming.!!!.Nakushauri rafiki yangu tafuta boyfriend na utajifunza haya yote ninayokwambia" akasema Christine na kunifanya nimuangalie kwa muda .


0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi