Friday, April 18, 2014

SERENA SEHEMU YA 16













            “Wakati taratibu zikiendelea za kumfanyia upasuaji ,jana jioni likatokea tukio la kustusha sana .Mtu mmoja aliingia katika chumba cha mgonjwa na kuchoma sindano ya sumu katika chupa ya maji aliyokuwa ametundikiwa mzee Albano.Bahati nzuri daktari aliyekuwa zamu aliwahi kugundua hilo na kunipigia simu nikamuelekeza nini cha kufanya na kwa juhudi zangu na madakatari wenzangu tukafanikiwa kuokoa maisha ya mgonjwa huyu.Kilichonistua zaidi ni taarifa za kipolisi zilizomuhusisha daktari kutoka hapo hapo hospitalini kuhusika na kitendo hicho.Daktari huyo alikutwa amekufa katika ajali ya gari muda mfupi baada ya kudhaniwa kuwa alitenda kosa hilo.Kwa kweli taarifa hizo zilinipa woga mkubwa na kunifanya kutomwamini mtu yeyote wa pale hospitalini kwetu kwa sababu daktari huyu anayeshukiwa kuhusika na kitendo kile alikuwa ni mmoja kati ya madaktari wa kutumainiwa sana .Mpaka sasa hivi uchunguzi unaendelea kubaini ni nani wanahusika na tukio lile na nini kusudio la kufanya vile.Ndugu zanguni sipendi kuwaficha kuwa mzee huyu ni mtu muhimu mno kwangu na siwezi kukubali mzee huyu auawe.Mzee huyu ugonjwa wake unatibika na nimekwishaiahidi familia yake kuwa nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa baba yao anapona.Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nimewaita ninyi wenzangu ninaowaamini mno ili muweze kushirikiana nami katika operesheni hii.Nina imani kuwa pamoja na uchache wetu huu tunaweza kabisa kuifanya operesheni hii na tukafanikiwa .Baada ya kufanya operesheni hii, mgonjwa nitakuhamishia hapa na nitamuhudumia hadi atakapopona.Nyumba hii hakuna anayeifahamu kama ni yangu na kwa taarifa yenu ni kwamba nyumba tayari nimekwisha ifanyia maandalizi ya kutosha ya kuifanya hospitali ya magonjwa ya fahamu na nimewahi kufanya operesheni kama mbili hivi kwa siri na zote zimefanikiwa.Kwa taarifa tu ni kwamba operesheni hii itafanyika kesho.Usiku wa leo mtapumzika hapa na kesho tutaingia kazini.”



0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi