Saturday, April 26, 2014

BLEEDING HEART SEHEMU YA 22







   “Samhani Joe kwa kuwa mbinafsi na kusahau kuhusu ugonjwa wa mama yako.Hii imetokana na kulewa na penzi lako kiasi kwamba siwezi kukaa mbali nawe kwa hofu ya kuibiwa na wanawake wengine.Kama ulivyosema kwamba maamuzi yamekwisha fanywa na hatuwezi kuyapangua.Japokuwa roho inaniuma sana lakini sina namna ya kuweza kukuzuia usiondoke na kurudi nyumbani kwenda kumuuguza mama yako.Kama ingekuwa ni kwa uwezo wangu nisingekubali kamwe uondoke na kuniacha hapa peke yangu.Sina mtu mwingine wa karibu hapa Swaziland na katika dunai nzima ambaye anaweza akanipa furaha kama ninayokuwa nayo nikiwa nawe.Wewe ni malaika wangu na siku zote utaendelea kuwa wangu.Sintakuacha kamwe na sintakubali hata siku moja mwanamke mwingine akuchukue toka mikononi mwangu.Joe penzi lako limenifanya nisione mwanaume mwingine zaidi yako na kwa maana hiyo niko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa dhumuni moja tu la kuwa nawe.Nitafanya kila niawezalo kwa ajili ya kuwa nawe tena.Nitakuja Tanzania muda si mrefu kwa dhumuni moja tu la kuwa nawe karibu.Nitakutafuta usiku na mchana mpaka nikupate.Ila naomba nikukumbushe kwamba wewe ni wangu peke yangu na sintakubali hata siku moja kukuona ukiwa na mwanamke mwingine ambaye si mimi.Sikutishi ila nitaumia mno na kutokana na maumivu hayo nitakayoyapata ninaweza kufanya jambo lolote.Naomba ujichunge sana Joe na usijaribu kuwa na mwanamke mwingine.Niko tayari kuja kukuona kila mwisho wa wiki kwa sababu uwezo huo ninao .Sitaki kuwe na umbali kati yangu nawe.Nakupenda sana Joe zaidi ya unavyoweza kufikiri” Swazi akasema kwa hisia kali na kukilaza kichwa chake kifuani kwa Joe ambaye alimshukuru Mungu kwa Swazi kukubali japo kwa shingo upande yeye kurudi nyumbani.Wakiwa katika hali ya simanzi kubwa mara kunasikika muungurumo wa gari nje ya nyumba yao.Joe akainuka na kwenda kuchungulia dirishani.Nguvu zikamuisha baada ya kuwaona polisi watatu wakishuka ndani ya gari wakiwa wameongozana na mtu mmoja mnene aliyekuwa amevaa mavaziya kiutamaduni ya watu wa Swaziland.Joe akatetemeka na kijasho chembamba kumtoka.Haraka haraka akamuita Swazi.


0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi