MASIMULIZI
Thursday, April 17, 2014
SERENA SEHEMU YA 15
RIWAYA : SERENA
SEHEMU YA 15
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Stella akamtazama tena kwa macho ya ukali yaliyoonyesha hasira ya wazi wazi.
“Jason do you love me? Akauliza Stella.Dr Jason akamtazama kwa makini usoni.
“Kwa nini unauliza hivyo wakati ukweli unaujua kuwa wewe ndiye pekee nikupendaye?
“Answer
Yes or No Jason.Do you real love me?”
“Yes I do love you”Akajibu Dr Jason
Stella akainama katika mto aliokuwa ameuweka mapajani mwake.Dr Jason akamshika nywele .
“No don’t touch me Jason.U don’t love me at all” Akasema Stella kwa ukali
“Stella huko sasa unakoenda ni mbali mno.I love you and you know that.I’m sorry about last night I know u needed me but I’m a doctor Stella na muda mwingi ninautumia kuhudumia wagonjwa.Nisingeweza kuja kwako jana .Trust me I love you and I can do anything for you,anything…..
“Stop it Jason.Nimegundua unanidanganya.kama ungekuwa unanipenda kweli usingelala jana na Serena binti wa mzee Albano Panavoc hotel.Nimelia sana Jason.Sijalala usiku wote nilikuwa nalia.kwa nini unifanyie hivi? You don’t know how much I do love you Jason. I Love you more than my own life.Ulifikiri sintajua??…….
Dr Jason akabaki mdomo wazi.Hakujua ajibu kitu gani.Akamwangalia Stella ambaye alikuwa akimtazama kwa hasira.Alihisi miguu kuisha nguvu.
ENDELEA………………………….
Akajitahidi kukusanya nguvu na kujibu
“baby that’s not true.kama kuna mtu aliyekwambia mambo hayo amekudanganya.Please amini kile ninachokwambia mimi.” Jason akajaribu kujitetea huku moyo wake ukienda mbio na kijasho kumtiririka kwa mbali.
“Jason ,Jason usije ukajaribu kunidanganya.Mimi
nafahamu kila unalolifanya.Huwezi nidanganya kitu.Nina uhakika na ninachokisema na kama ukitaka nitakutajia hata chakula mlichokula .Si mlikula maini nyie,au mimi mwongo? Kataa na hilo.”
Dr jason akashindwa kukataa akabaki akimwangalia Stella huku akihema kwa nguvu.Hakuwa na sababu ya kubisha tena kwa sababu ilionekana tayari Stella ana taarifa kamili.Kilichomuumiza akili ni kwamba Stella amefahamu vipi kuhusu yeye kulala hoteli moja na Serena ?
“Jason Darling kwa nini lakini ukanifanyia hivyo hali unajua kuwa wewe ndiye kila kitu kwangu? Huyu binti wa mzee Albano , Serena yeye ana kitu gani cha tofauti na mimi??? Answer me jason” Stella akasema kwa uchungu
“Stella una uhakika gani kuwa nilikuwa pale Panavoc hotel na Serena? Akauliza Dr Jason
“Jason mimi nina vyanzo vingi vya taarifa kwa hiyo usije jaribu kunidanganya hata siku moja.Ninajua kila unachokifanya.Kila unakoenda.I know every step
of you” akasema Stella
“Kwa hiyo umeweka watu wa kunifuatilia siyo? You don’t trust me, right? Akauliza Jason
Stella akamuangalia usoni bila kujibu lolote
“Nakuuliza Stella umeweka watu wa kunifuatilia mimi ?
“It’s for your own safety Jason”Stella akajibu
“My own safety??? Unamaanisha nini?
“Jason I don’t want you to get hurt ndio maana nimeweka watu wa kukufuatilia na kukulinda”
Dr Jason akastuka akasimama na kuuliza.
“Kunilinda? Kwa nini uweke watu wa kunilinda?kwani kuna tatizo gani?Na kama lengo lako lilikuwa ni zuri kwa nini basi usiniambie?
“Jason sit down first.We need to talk.”
Dr Jason huku kijasho kikimtoka na moyo kumwenda mbio akakaa kitandani kama alivyoombwa na Stella.
“haya nambie unalotaka kuniambia” Akasema Dr Jason
“Jason mchana wa leo tunasafiri.Don’t ask
why and where we’re going.Kila kitu kiko tayari kwa safari.Kama kweli unanipenda kwa dhati ya moyo wako mchana wa leo tunasafiri.” Akasema Stella
Dr Jason akasimama akazunguka mle chumbani na kupumua kwa nguvu.
“Stella sijakuelewa unasema nini?
“Ninasema mchana wa leo tunasafiri.Kuna safari ya dharura sana imetokea
hivyo inatulazimu mimi na wewe tuondoke mchana huu wa leo.Tunakwenda nje ya nchi”
Dr jason akahisi joto akavua koti na kulitupa sofani.Shati lake lilikuwa limeanza kulowa jasho ambalo sasa lilikuwa limeanza kumtiririka kwa kasi.
“No Stella I cant go.”
Stella naye akainuka pale kitandani na kusimama karibu na Jason.
“Jason unasemaje?
“Nasema siwezi kwenda hiyo safari.Tangu lini kukawa na safari ya kustukiza namna hii? Halafu unaelewa kabisa kwamba niko katika kipindi kigumu sana cha kuokoa maisha ya mzee Albano.Nahitajika kumfanyia upasuaji mkubwa wa kuokoa maisha yake na mimi ndiyo tumaini pekee la maisha ya mzee yule.”
Stella akamsogelea karibu zaidi akamtazama usoni na kusema
“Jason please you don’t have to do that.Achana kabisa na mzee Albano.”
Dr Jason akarudi nyuma hatua kadhaa akamkazia macho Stella.Hakuamini alichokisikia
“ Stella unasema nini??? Akauliza
“Jason you don’t have to do that operation.We have to leave the country this afternoon”
Dr Jason akamtazama Stella kana kwamba ndiyo anamuona kwa mara ya kwanza.
“Stella siamini kama ni wewe ndiye unayeniambia maneno haya leo.Stella umekuwa mstari wa mbele kila siku kunihimiza nizidi kuokoa maisha ya watu leo umegeuka na kuniambia nisimfanye upasuaji
mzee Albano??? Unataka mzee Albano afariki? Mbona sikuelewi Stella?
“Huwezi kunielewa Jason.Lakini nakwambia kwamba from this moment achana kabisa kujishughulisha na kitu chochote kinachohusiana na mzee Albano.Jason darling nakupenda mno na sitaki uingie katika matatizo ndio maana nafanya kila ninaloweza kukulinda usije dhurika.” Akasema Stella kwa sauti ya upole huku akimkaribia zaidi Dr Jason
“Stella .Siwezi kukataa kufanya operesheni hii hata kama angeniambia nani.Hii ni taaluma yangu ambayo niliapa kufuata misingi yote ya taaluma hii.Mzee Albano atafariki nisipomfanyia upasuaji huu,kitu ambacho katu hakiwezi kutokea.Niko tayari nife mimi lakini mzee albano apone”
Stella akatulia akapumua kwa nguvu halafu akasema
“Its because of her,right? Ni kwa sababu ya Serena ndio maana uko tayari hata kuhatarisha uhai wako kwa ajili ya baba yake.Amekupa nini Serena Jason mpaka umfanyie hivi.??Why don’t you listen to me?
Dr Jason hakujibu kitu akaendelea kumwangalia Stella kwa jicho la ukali
“Tell me Jason Serena amekupa kitu gani….?!.Akauliza Stella kwa sauti ya juu ya ukali
“I promised to save her father !!” Akajibu Dr Jason naye kwa ukali.
“I gave her my word and I’ll do everything I can to keep my promise”
Dr Jason akachukua koti lake pale sofani akatoka mle chumbani kwa hasira akaubamiza mlango.
“Jason!!..come back here !!....” Akaita Stella kwa sauti kali lakini Dr Jason hakugeuka.Akaenda lilipo gari lake akaingia na kuondoka kwa kasi.
Huku machozi yakimtoka Stella akajitupa kitandani .
“Jason ,Jason why you are hurting me like this.Kitu gani nimemfanyia Jason kiasi cha kunitesa namna hii?I love Jason and I’m not going tp loose him because of this stupid girl Serena……..atanitambua mimi ni nani.Kwa sasa naingia mwenyewe vitani.Kwanza kumlinda Jason asidhuriwe na mtu yeyote yule hata awe baba yangu na pili nataka nimtafute huyo Serena nimuonyeshe kuwa mimi si mtu wa kuchezea.I swear ,Serena I’ll teach you a lesson.Get prepared.You must pay for this." akasema Stella
huku uso wake ukiwa umejikunja kwa hasira
*
*
*
*
Dr Jason akawasili hospitalini na kwa haraka bila kuongea na mtu yeyote akaelekea chumba cha mgonjwa.Dr Anna maria alikuwa amepokewa
na Dr Mwamvita.Dr Jason akapata taarifa ya mgonjwa,halafu akafanya vipimo kadhaa na kuridhika na maendeleo ya mzee Albano.Akatoka na kuelekea ofisini kwake.kabla hajaingia ofisini kwake akakutana na Dr Henry
“Morning Dr Jason”
“Morning Dr Henry.” Akajibu Dr Jason
“Vipi mgonjwa anaendelaje? Akauliza Dr Henry
“Mgonjwa anaendelea vizuri sana.Hali yake inatia matumaini”
“Sawa Dr Jason .Imekuwa bahati tumekutana kwani nilikuwa nakuja ofisini kwako.Kuna mambo ambayo nataka tuyajadili”
“mambo gani hayo Dr Henry” Akasema Dr Jason huku akiufungua mlango wa ofisi yake.Baada ya kuketi kitini Dr henry akasema.
“Nimepata simu leo asubuhi toka ofisi kuu wakihitaji kujua maendeleo ya mgonjwa na lini tunatazamia kufanya upasuaji.Wanataka taarifa ya mapema kabla ya saa tano asubuhi ya leo ili
waone utaratibu wa kuziba nafasi ya Dr Selemani.Mimi nimewaambia kuwa wasubiri niongee kwanza na wewe kwani wewe ndiye unayeweza kutoa taarifa kamili ni lini unaweza ukafanya upasuaji huo kutokana na maendeleo ya mgonjwa ulivyoyaona”
Dr Jason akatulia kidogo akajishika kichwa akasema
“Mgonjwa anaendelea vizuri Dr Henry.Kila kipimo kinaonyesha maendeleo ni mazuri na kwa maana hiyo tunaweza kuifanya operesheni hii ndani ya siku chache zijazo.Kwa kujibu wa hali ilivyo hatuna haja ya kusubiri sana nadhani tuwape muda ili siku ya kesho na kesho kutwa waweze kututafutia daktari huyo wa kuchukua nafasi ya Dr selemani .Ijumaa kuanzia saa nne usiku tuifanye operesheni hii ambayo inaweza kutuchukua mpaka saa kumi alfajiri.”Akasema Dr Jason.
“Kwa hiyo kama operesheni hiyo itakuwa ijumaa usiku basi toka sasa inabidi tuanze kufanya maandalizi kwa ajili hiyo.Kila kitu kinatakiwa kiwe tayari mpaka kesho jioni.Mimi ngoja nikawapigie wakurugenzi niwataarifu kuwa tutaifanya operesheni hiyo Ijumaa usiku.Orodhesha pia vifaa vyote ambavyo unavihitaji katika operesheni hii ili vitafutwe haraka sana kabla ya siku ya kesho .”
Akasema Dr Henry huku akiondoka ofisini kwa Dr Jason na kuelekea ofisini kwake
akiwa mwingi wa furaha.Akaingia ofisini kwake akaufunga mlango wake na kutoa simu yake ya mkononi halafu akazitafuta namba za Mr Kumzaya.
“Hallow Mr Kumzaya”
“Hello old boy,how are you ?”
“I’m fine Mr Kumzaya.Sasa ni hivi mambo yanakwena vizuri sana.Kila kitu kiko sawa sasa hebu tukutane ili tupeane mikakati nini cha kufanya ikiwa ni pamoja na makabidhiano ya kila kitu kama tulivyokuwa tumekubaliana”
“Ok Dr Henry kazi nzuri sana.Kwa sasa naelekea ofisini kwangu tukutane pale ndani ya dakika ishirini”
“Ok Kumzaya utanikuta pale ofisini kwako nakusubiri”
“ Dr Henry Good work,hahahahaaa !!” Akajibu Mr Kumzaya huku akicheka halafu akakata simu
Dr Henry akavaa koti lake la suti ,akafunga ofisi yake na kutoka kwa haraka.
“ Siamini kama nusu saa ijayo nitakuwa naitwa billionea.hahahaahaa !! bahati ilioje.” Akawaza Dr Henry huku akicheka na kuliacha geti la hospitali.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment