MASIMULIZI
Friday, April 18, 2014
BEFORE I DIE SEHEMU YA 16
RIWAYA : BEFORE I DIE
SEHEMU YA 16
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ahsante sana dada latoya .Utakuwa umemsaidia sana Innocent” Sabrina na Grace wakasema kwa pamoja.
“Je kuna haja ya kuwataarifu wazazi wake kuhusiana na hili? Latoya akauliza
“dadaLatoya sidhani kama litakuwa ni jambo la busara kuwashirikisha wazazi wake kwa sababu toka mwanzo hawakuwa wamemkubali Marina kwa hiyo naamni hata Innocent asingependa kuwashirikisha katika suala la msiba.” Grace akasema
Bila kupoteza muda Latoya akachukua simu yake na kuanza kuwapigia simu watu mbali mbali akiwafahamisha kuhusiana na msiba ule.Akatoa malekezo kadhaa juu ya maandalizi ya msiba ule ambao alitaka ufanyike nyumbani kwake.
ENDELEA…………………………..
Masaa manne yamepita toka Innocent alipozinduka.Baada tu ya kupata fahamu alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa na madaktari wakawasihi ndugu zake kuwa na utulivu kwa sababu hiyo ni hali ya kawaida.Innocent akaachwa apumzike ili akili yake itulie na baada ya saa nne akafumbua macho.Chumba kilikuwa na harufu kali ya dawa.Akapepesa macho na kugundua pale palikuwa ni hospitali.Akaanza kuvuta kumbu kumbu na kujiuliza alifikaje fikaje pale hospitali.Mara akakumbuka kwamba ilikuwa afanyiwe upasuaji wa kundoa figo ili awekewe Marina.Tayari kumbu kumbu zote zikarudi.Kitu kilicho mstaajabisha hakuwa akisikia maumivu yoyote ya sehemu iliyopasuliwa .Akanyoosha mkono wake na kugusa sehemu za tumbo lakini hakukuwa na dalili zozote za kupasuliwa.Akastuka akainuka na kukaa kitandani,akajifunua shuka akatazama mwili mzima hakukuwa na sehemu yoyote ile iliyokuwa imepasuliwa.Akainama na kukishika kichwa chake kwa mikono yake .
“Hivi ni kweli au nilikuwa ndotoni? Ninachokumbuka mara ya mwisho nilikuwa katika chumba cha upasuaji nikisubuiri kufanyiwa operesheni.Nini kimetokea? Am I crazy? …No ! No ! I’m not crazy.Akili yangu inafanya kazi vizuri.Nilitakiwa kufanyiwa operesheni kwa ajili ya kumuwekea figo Marina.Yes Marina.! Where is she? “Innocent akawaza huku jasho likimtiririka na mara akaingia muuguzi.
“Marina yuko wapi? Mbona sijafanyiwa upasuaji?” Inno akauliza maswali haraka haraka
“Innocent tafadhali endelea kupumzika.mwili wako bado hauna nguvu za kuitosha.tafadhali endelea kupumzika”
“Nesi akili yangu inafanya kazi vizuri na ninakumbuka mara ya mwisho nilikuwa katika chumba cha upasuaji nimelala nikisubiri kupasuliwa.Niambie nini kilitokea? Ni kwa nini sikufanyiwa upasuaji? Innocent akauliza kwa sauti kubwa ambayo ikawafanya ndugu zake waliokuwa wamekaa nje wakisubiri arejewe na fahamu waiingie mle chumbani.Innocent akastuka baada ya kuwaona wazazi wake wakiwa wameambatana na akina Grace na Sabrina.Mtu wa mwisho kuingia mle chumbani alikuwa ni Latoya.Innocent hakusita kuachia tabasamu baada ya kugonganisha macho na Latoya.
“Latoya umekuja? Akasema Inno
“Niko hapa Innocent na akina Grace ,Sabrina na wazazi wako.” Latoya akasema
“Ninashukuru sana.” Akasema huku akiwaangalia akina Grace na Sabrina waliokuwa wamekaa pembeni ya kitanda chake.
“Unajisikiaje sasa hivi? Mama yake akauliza
“najisikia vizuri kwa sasa.lakini ninachoshangaa ni kwa nini sijafanyiwa upasuaji wakati tayari nilikuwa katika katika chumba cha upasuaji nikisubiri kupasuliwa? Inno akauliza
“Innocent kuna mambo yalitokea ndiyo yaliyopelekea hadi kushindwa kufanyika operesheni .” baba yake Innocent akasema
“baba nini kimetokea? ….where is…..yuko wapi Marina? Inno akauliza kwa wasi wasi
“Inno tafadhali jitahidi uwe na moyo mgumu lakini huna budi kufahamu kwamba Marina amefariki dunia muda mfupi kabla ya kufanyika operesheni” baba yake Innocent akasema.Innocent akacheka kidogo na kusema
“No! That’s not true….Siyo kweli.Eti Grace ni kweli Marina amefariki dunia?
Grace akashindwa asema nini machozi yakamtoka. Inno akamgeukia Latoya.
“latoya niambie ni kweli Marina amefariki dunia?
Latoya akasita aseme nini akajikaza na kutikisa kichwa.
“Ni kweli Innocent.Maria amefariki dunia.”
Inno akayafunika macho yake kwa viganja vya mikono yake na kuinama.
“Ouh Marina ! “ akasema kwa uchungu.
Chumba chote kikawa kimya kabisa.Hali ikawa ni ya simanzi kubwa.mara daktari akaingia akiwa ameongozana na muuguzi.
“Dokta tafadhali naomba nipeleke nikamuone Marina.” Inno akasema kwa haraka huku macho yake yamejaa machozi
“Innocent tafadhali endelea kupumzika hadi hapo mwili wako utakapopata nguvu za kutosha.” Daktari akasema.
“Daktari naomba tafadhali nipeleke nikamuone marina.” Inno akasisitiza
Daktari akawaomba wale wote waliokuwamo mle chumbani watoke na wamuache yeye na Innocent.
“Inno nasikitika sana kwamba pamoja na jitihada zote zilizofanyika lakini hatukuweza kuyaokoa maisha ya Marina.Alifariki muda mfupi kabla ya kuanza kufanyika kwa operesheni.” Dokta akasema
“Ouh Marina
I’m so sorry.Pamoja na jitihada zote lakini bado umepoteza maisha.” Inno akasema kwa uchungu.
“Innocent,kila lililohitajika kufanyika ,lilifanyika kwa hiyo naomba usijilaumu sana.Mungu alipenda iwe hivyo” daktari akasema
“Dokta naomba unipeleke nikamuone Marina” Inno akasisitiza.Daktari akamtuliza na kumweleza kwamba muda ule haukuwa muafaka kwa yeye kwenda kuiona maiti ya Marina hadi hapo baadae.Daktari akaondoka na kumuacha Inno pale kitandani
“Its because of them.Its because of you mom and daddy .Ninyi ndio mliosababisha kifo cha Marina...” Inno akasema kwa hasira baada ya kufungua mlango wa kile chumba na kuwakuta wazazi wake wamekaa katika viti pale nje
“Ninyi ni wazazi wangu nawapenda na kuwaheshimu sana lakini katika suala hili nawaomba mniache peke yangu.Niacheni mimi nikamzike Marina mwenyewe kwa sababu kama hamkutaka kumuona akiwa hai iweje muonyeshe huzuni wakati amefariki ? Naomba niwaambie wazazi wangu kwamba nimeumia sana.Kitendo cha kumkataa,kumdharau,na kumnyanyapaa Marina kimenisababishia jeraha kubwa moyoni
mwangu.”Inno akasema kwa sauti ya juu na kumlazimu Latoya ainuke na kumfuata akamsihi aingie ndani na kutulia.
*
*
*
*
Saa moja za jioni hali ya Innocent ilikuwa ya kuridhisha na madaktari walimruhusu arejee nyumbani.Alikuwa mkimya sana tofauti na alivyozoeleka.Kifo kile cha Marina kilimletea jeraha kubwa moyoni mwake.Mara tu Innocent alipopimwa na madaktari na wakathibitisha kwamba kwa sasa hali yake ni nzuri na anaweza kurudi nyumbani Latoya akaingia mle chumbani na kuketi karibu naye
“Inno pole sana.Naomba utambue kwamba tuko pamoja katika msiba huu.Huu ni msiba wetu sote na wote tumeguswa.Jipe moyo Innocent “ Latoya akasema huku amemshika mkono
“latoya nashukuru sana kwa ushirikiano wenu.Kifo cha Marina kimeniuma sana.Nilipambana kuyaokoa maisha yake lakini Mungu alimpenda zaidi” Inno akasema na kisha akatazama chini akakaa kimya
“Innocent kuna jambo nataka kukufahamisha.” Latoya akasema na kumfanya Innocent ainue kichwa chake kumsikiliza
“Nimeshauriana na Sabrina na Grace na kwa pamoja tumekubaliana kwamba kwa kuwa Marina hakuwa na ndugu yeyote hapa mjini basi shughuli zote za msiba zitafanyikia nyumbani kwangu na gharama zote zitakuwa ni juu yangu.Nilielezwa kuhusu matatizo yaliyotokea kule nyumbani kwenu hivyo tukaona halitakuwa jambo zuri kama msiba huu wa Marina utapelekwa pale kwenu.Tayari maandalizi ya msiba yameanza .Kuna kampuni ambayo nimeikodisha isimamie shughuli nzima ya msiba huu .Nimeona nikufahamishe mapema ili ufahamu nini kinachoendelea kwa sasa. “
Inno akamtazama Latoya ,halafu akasema.
“Latoya sijui hata niseme nini kwa jambo kubwa ulilolifanya.Napenda tu ufahamu kwamba toka ndani kabisa mwa moyo wangu ninasema ahsante sana kwa msaada huu mkubwa.Marina hakuwa na ndugu yeyote hapa mjini kwa hiyo hakuna mahala kokote ambako tungeweza kuupeleka msiba huu.Nashukuru kwa kujitolea shughuli za msiba huu zifanyike nyumbani kwako kwani nilikuwa naumiza kichwa mno kuhusu wapi ningeupeleka msiba huu.Nyumbani kwetu ni kama hivyo ulivyosikia,niliondoka baada ya kutopendezwa na mambo aliyofanyiwa Marina.Pamoja na hayo naomba niseme samahani sana Latoya kwa usumbufu huu mkubwa ulioupata.” Innocent akasema .Latoya akamwangalia kwa makini halafu akasema
”Innocent naomba uondoe hofu moyoni mwako.Hakuna usumbufu wowote utakaotokea.Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu kuupeleka msiba huu nyumbani kwangu kwa sababu si msiba wako peke yako bali ni wetu sote.Sote tumeguswa sana na msiba huu .Marina alikuwa ni rafiki yako na kwa maana hiyo ni rafiki yetu vile vile.Nakuomba uwe na amani ya moyo Innocent na wala usitie shaka.Jiandae ili tuweze kuondoka hapa hospitali na kuelekea nyumbani kwangu ambako shughuli za msiba zinaendelea hivi sasa.”Latoya akasema
“Sijui nikushukuruje Latoya.Naomba ufahamu kwamba nina deni kubwa kwako la kurudisha fadhila hii kubwa .” Inno akasema
“Innocent tafadhali usiwaze kuhusu hilo.Sisi kama marafiki tuna jukumu la kusaidiana katika kila hali.tafadhali jiandae ili tuondoke hapa ukapumzike wakati taratibu nyingine zikiendelea” Akasema latoya kisha akatoka nje ya kile chumba na kumuacha Innocent akijiiandaa.Wazazi wa Innocent bado walikuwa pale nje na walipomuona Latoya ametoka mle ndani ya chumba wakamuita .
“Mwanangu sisi ni wazazi wake Innocent,hebu tuambie mwenzio anaendeleaje?’ mama Inno akauliza
“Anaendelea vizuri mama .Kwa sasa anajiandaa ili tuondoke hapa na kwenda kuendelea na shughuli za msiba.”
“Amesema shughuli za msiba zitafanyikia wapi? Huyu binti Marina alikuwa na ndugu zake hapa mjini? Baba yake Inno akauliza
“Marina hakuwa na ndugu hapa mjini kwa maana hiyo tumeafikiana kwamba msiba utakuwa nyumbani kwangu.” Latoya akasema na mara akatokea Sarah dada yake Innocent akakuta Latoya akiongea na wazazi wake.Akastuka sana na kusimama ghafla akaufumba mdomo wake kwa mkono wake wa kulia.Alikumbwa na mstuko wa ghafla.Latoya akageuka na kwa hatua za taratibu akaondoka zake na kuwaacha wazazi wa Innocent wakiwa kimya.
“Mama sikuweza kupata nafasi ya kufika hapa mapema.Uliponipigia simu na kunitaarifu kuhusu suala hili la Innocent nilikuwa Morogoro .Nimerudi sasa hivi nikaona ni bora nije moja kwa moja hapa hospitali.Innocent anaendeleaje? Akauliza Sarah kwa wasi wasi
“Mdogo wako anaendelea vizuri kwa sasa na tayari amepewa ruhusa ya kuondoka baada ya madaktari kuhakikisha kwamba hali yake ni nzuri.Kwa bahati mbaya yule binti aliyekuwa akimtolea figo alifariki kabla ya upasuaji kufanyika kwa hiyo Inno hakufanyiwa upasuaji wowote.” Mama yake akasema
“ Ouh ahsante Mungu
! “
Sarah akasema lakini bado sura yake ilionyesha mstuko
“Mbona umestuka?” Baba yake akauliza
“Nimestuka kusikia kwamba yule msichana amefariki dunia.Baba hivi hamuoni ni matatizo kiasi gani yanakwenda kutokea baada ya huyo binti kufariki ? Moyoni mwake tayari Innocent amejenga picha mbaya sana kwa ninyi kukataa yule msichana akae pale nyumbani.Atawalaumu sana na kusema
kuwa mmechangia kifo chake .Ninamfahamu Inno vizuri,kifo hiki kitakuwa kimemuumiza mno.Lakini nashukuru kwa operesheni hii kutofanyika kwa sababu hata mimi sikuona sababu ya yeye kuamua kutoa figo yake kwa ajili ya msichana asiyemfahamu na tena kahaba.Angeidhalilisa sana familia yetu..” Sarah akasema
“Tayari amekwisha sema hilo na amesema kwamba sisi ndio tuliosababisha kifo cha binti yule.” Mama yake Inno akasema na kumtazama binti yake.
“Mama yule msichana mliyekuwa mkiongea naye hapa mnamfahamu? Sarah akawauliza wazazi wake.
“hapana hatumfahamu lakini kwa mujibu wa Grace ni kwamba yule ni rafiki wa Innocent na ndiye aliyempatia kazi Sabrina katika taasisi yake.Kwani vipi mbona unaonyesha wasi wasi na kustuka mara ulipomuona ? Mama Innocent akauliza
TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO…….
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment