Ndugu zanguni sipendi kuwaficha
kuwa mzee huyu ni mtu muhimu mno kwangu na siwezi kukubali mzee huyu auawe.Mzee
huyu ugonjwa wake unatibika na nimekwishaiahidi familia yake kuwa nitafanya
kila niwezalo kuhakikisha kuwa baba yao anapona.Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana
nimewaita ninyi wenzangu ninaowaamini mno ili muweze kushirikiana nami katika
operesheni hii.
Nina imani kuwa pamoja na uchache wetu huu tunaweza kabisa kuifanya operesheni hii na tukafanikiwa .Baada ya kufanya operesheni hii, mgonjwa nitakuhamishia hapa na nitamuhudumia hadi atakapopona.Nyumba hii hakuna anayeifahamu kama ni yangu na kwa taarifa yenu ni kwamba nyumba tayari nimekwisha ifanyia maandalizi ya kutosha ya kuifanya hospitali ya magonjwa ya fahamu na nimewahi kufanya operesheni kama mbili hivi kwa siri na zote zimefanikiwa.Kwa taarifa tu ni kwamba operesheni hii itafanyika kesho.Usiku wa leo mtapumzika hapa na kesho tutaingia kazini.”

0 comments:
Post a Comment