MASIMULIZI
Thursday, April 17, 2014
BLEEDING HEART SEHEMU YA 15
RIWAYA : BLEEDING HEART
SEHEMU YA 15
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Ahsante sana Paula.You’ll always be here in my heart.” Joe akasema huku akikishika kifua chake mahala unapokaa moyo.
“Tafadhali niruhusu nikusindikize hadi nje “ Joe akasema na Paula huku akaitabasamu akasema
“hakuna shida Joe ila nimekuja na usafiri wangu.” Paula akasema na kisha wakaanza kutembea kuelekea mahala yanakoegeshwa magari.
“Joe nashukuru ,nitakupigia simu siku ya safari ikifika “ akasema Paula na kumpa mkono Joe kisha akaelekea katika gari moja jesui aina ya BMW ,mara akashuka kijana mmoja mtanashati akazunguka na kumfungulia Paula mlango ,halafu akaufunga na kurudi garini kisha wakaondoka maeneo hayo.Joe jasho lilimtiririka,damu ilikuwa ikimchemka.Alilisindikiza gari lile kwa macho hadi likapotea kabisa.
ENDELEA…………………………………….
“maamuzi ya kuachana na Paula hayakuwa maamuzi sahihi.Nilifanya kosa kubwa sana.Muda huu mchache niliokaa na Paula toka tumeachana nimekumbuka mambo mengi sana toka enzi za utoto wetu hadi tulipokuwa wapenzi.Nimekumbuka namna mapenzi yetu yalivyokuwa na nguvu na hakuna hata mmoja wetu aliyekuwa akitegemea kama ingetokea siku tungekuja kuachana .Sijui ni shetani gani aliyenipitia na kunishawishi niachane na Paula.Kwa sasa ndiyo ninagundua kosa nililolifanya.Nilifanya kosa kubwa sana.Japokuwa nimekuwa nikijaribu kukubaliana na ukweli kwamba mimi na Paula hatuwezi kamwe kuwa pamoja lakini ukweli halisi unabaki pale pale kwamba bado ninamuhitaji sana.I feel so empty without her.Mama alinisisitizia kwamba Paula ndiye pekee mwanamke anayenifaa lakini nikampuuza .Alinionya kwamba siku nitakayoligundua hilo nitakuwa nimechelewa sana.Kwa sasa nimeligundua hilo na kweli nimeshachelewa.Paula si wangu tena.Paula amekwisha fanya maamuzi na hakuna namna ya kuweza kumshawishi abadili maamuzi.I was so stupid….” Joe akawaza huku akitembea taratibu kurudi katika meza aliyokuwa amekaa na Paula
“Paula ameamua kunionyesha ni jinsi gani nilivyo mtu wa muhimu kwake.Pamoja na kutengana naye lakini bado nimeendelea kuwa mtu wake muhimu na kwa ajili ya upendo wake mkubwa kwangu ameamua kutokumpa nafasi mtu mwingine katika moyo wake.Ameamua kuitunza ahadi aliyonipa kwamba hataweza kuwa na mwanaume mwingine chini ya jua zaidi yangu.Amenionyesha ni jinsi gani nilivyo na thamani kubwa kwake.Amenionyesha kwamba hawezi kuishi bila mimi kwa hiyo ameamua maisha yake yote ayamalizie katika nyumba ya watawa.Huu ni upendo mkubwa usiopimika.Kwa nini niliamua kuachana na Paula?. Joe akaendelea kuumia kwa mawazo.
“Na yule kijana aliyekuwa naye garini ni nani? Inawezekana akawa amempata mpenzi mwingine? Sidhani kama anaweza akafanya hivyo.Kama ingekuwa hivyo asingekubali kuingia utawani.Moyo unaniuma sana.Nimepoteza kitu cha thamani kubwa maishani.Paula ni mtu wa pekee ambaye thamani yake haiwezi kulinganishwa na kitu chochote.” Joe akawaza na kwa mwendo wa taratibu akaanza kuondoka eneo lile akiwa na mawazo mengi.
*********************
Saa nne za usiku Paula alikuwa amejilaza kitandani akiwa amelishikilia albamu la picha.Nyingi ya picha zilizomo humu ni zile ambazo alipiga akiwa na Joe.Alikuwa akiitazama picha moja baada ya nyingine na kuanza kukumbuka kila tukio walilolipitia wakati wakiwa pamoja.Kila alipoufungua ukurasa mpaya alikuwa akitabasamu na wakati mwingine alikuwa akitoa machozi.Picha zile zilimkumbusha mbali sana.Alikumbuka historia yao toka wakiwa wadogo.Alikumbuka namna walivyokuwa wakiishi kama ndugu,akakumbuka siku mapenzi yao yalivyoanza na mpaka walipofika na kuamua kutengana.Paula akaitoa picha moja ambayo alipiga na Joe siku chache kabla hawajatengana .Walikuwa wakiogelea katika bwawa la kuogelea.Siku hii ni siku ambayo walipeana ahadi nyingi za kuishi pamoja hadi kifo kiwatenganishe.Picha ile ilimuonyesha Joe akiwa ndani ya maji amemkumbatia Paula huku wote wawili wakicheka kwa furaha.Paula akashindwa kujizuia kudondosha chozi.Akaitoa picha ile na kuiangalia tena kwa makini sana akaiweka kifuani kwake.
“Kitu kimoja ambacho nimekifanya na nitaendelea kukifanya hadi kufa kwangu ni kukupenda Joe.Nakupenda sana na sintaacha kukupenda.Wewe ni mtu wa pekee kabisa maishani mwangu.Ulikuwa ni mwanaume wangu wa kwanza kukupenda na baada yako sintapenda tena mwanaume mwingine.Hakuna wa kukulinganisha nawe Joe .Nakupenda kwa dhati ya moyo wangu.Moyo wangu unaumia sana kila nikuonapo Ninaumia sana kila nikumbukapo siku uliyoamua kutengana na mimi.Nimechukua uamuzi mgumu wa kwenda kujiunga na utawa kwa sababu siko tayari kumpa mwili na moyo wangu mwanaume mwingine.Niliumbwa kwa ajili yako pekee.” Paula akawaza ,macho yake yalikuwa yamejaa machozi.Akachukua kitambaa akafuta machozi na kuirudisha picha ile mahala alikoitoa.Akalifunga lile albamu na kuliweka pembeni.Akainuka pale kitandani na kuelekea katika meza ya vipodozi,akajitazama kwa sekunde kadhaa
“Mimi ni msichana mrembo.Ninajifahamu kwamba ni mrembo.Nimesoma na nina digrii yangu inayoweza kunisaidia kupata kazi na nikaishi maisha mazuri.Lakini vyote hivyo havitakuwa na thamani kama nitaishi bila ya kuwa na Joe.Hata nikitafuta mwanaume mwingine hatakuwa kama Joe.Yeye ndiye maisha yangu.Kwa sababu yake nimeamua kufanya maamuzi haya magumu ya kwenda kujiunga na utawa..Nitampenda yeye pekee hadi kufa kwangu” Paula akawaza.Hii ilikuwa ni moja kati ya siku yake ngumu sana.
********************
Mlio wa simu iliyokuwa mezani ukamstua Joe na kwa haraka akaikimbilia akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Paula.Joe akavuta pumzi ndefu akaitazama simu ile ikiita.Ni siku ya nne toka alipoonana na Paula na akamuahidi kumpigia simu ili kumfahamisha juu ya safari yake ya kuelekea katika nyumba ya watawa .Joe alimuomba Paula awe ni mmoja wa wale watakaomsindikiza kuelekea huko.Alihisi kama mikono ikimtetemeka.Simu hii alikuwa akiisubiri kwa hamu kubwa.
“Hallo Paula” akasema Joe baada ya kubonyeza kitufe cha kupokelea
“Hallo Joe habari yako?
“Habari yangu nzuri Paula sijui wewe”
“Mimi mzima.habari za siku mbili tatu?
“habari nzuri lakini siku zote nimekuwa kama mgonjwa nikisubiri simu uliyoahidi utanipigia” Joe akasema na kumfanya Paula acheke.
“Umeshaanza mambo yako Joe.Yaani uumwe kwa sababu ya kusubiri simu yangu?
“Sikutanii Paula.Simu yako nimekuwa nikiingojea kwa hamu kubwa.Huwezi kuelewa ni kwa namna gani ilivyo muhimu kwangu.” Joe akasema taratibu na kwa upande wa pili wa simu akasikia Paula akishusha pumzi halafu kikapita kimya kifupi.
“Joe vipi kuhusu maisha yako unaendeleaje? Una mipango gani na maisha yako ya mbele? Paula akauliza.
“Baada ya kuhitimu masomo na kupata shahada ,kinachofuata kwa sasa ni kutafuta kazi.Nimekwisha tuma maombi ya kazi sehemu mbalimbali na kuna shirika moja lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya miradi ya maji vijijini katika nchi za mashariki na kusini mwa afrika limeonyesha kuvutiwa na mimi na wameniambia niende jumatatu kwa ajili ya usaili.Hiyo ndiyo plani yangu kubwa ka sasa ,kupata kazi na kisha kuanza kuyajenga maisha yangu.Baadae nina mpango wa kuendelea zaidi na masomo” Joe akasema
“Nimefurahi kusikia hivyo.Ninakuombea kwa Mungu ili kila kitu ulichokipanga kifanikiwe.Pamoja na hayo Joe kuna kitu kimoja ninataka kukuomba”
“Paula kitu chochote unachokitaka kwangu nitakupatia.hata ukinituma nikamuue shetani nitakwenda” Joe akasema na kumfanya Paula acheke kicheko kikubwa na kusema
“ Joe ,nakumbuka wakati tuko wapenzi tulikuwa na ndoto nyingi za kutimiza.Ndoto yetu kubwa ilikuwa ni kufunga ndoa, na kuwa na watoto wawili msichana na mvulana na kujenga familia yenye furaha na amani.Tulikuwa na ndoto za kuwa na shamba la familia pamoja na ndoto nyingine nyingi.Kutokana na hali halisi ilivyo hatuwezi tena kuzitimiza ndoto hizo tukiwa pamoja.Ninakuomba Joe tafadhali fanya kila unavyoweza kuzitimiza ndoto zetu zote tulizokuwa tukiota kuzitimiz pamoja.Nakuomba utafute mwanamke mzuri ambaye utafunga naye ndoa na mtapata watoto kama tulivyokuwa tumepanga na kama mkibahatika kumpata mtoto wa kike basi nitakuomba umuite jina langu Paula.Can you do all that Joe? Paula akasema kwa sauti ndogo ambayo inamfanya Joe machozi yamlenge.
“Joe are you there? Paula akauliza baada ya kuona Joe amekuwa kimya
“I’m here Paula.” Joe akajibu halafu akatafakari na kusema.
“Paula ni kweli tulikuwa na ndoto nyingi za kutimiza pamoja lakini kwa sasa naona kama ndoto zile zote zimefutika.I cant do that……” Joe akasema kwa suti ya taratibu yenye kuonyesha majuto ndani yake.
“Please Joe.Do that for me.If you cant do that for youself ,do it for me” Paula akasisitiza
“Paula I cant do that….siwezi kufanya hivyo” Joe akasema
“Kwa nini Joe.Kama hutafanya hivyo nitajua kwamba siku zote ulikuwa ukinidanganya kwamba unanipenda na ahadi ulizokuwa ukinipa hazikuwa za kweli.” Paula akasema
“Paula naomba unisikilize.Kusema ukweli siwezi kufanya chochote kwa sasa kwa sababu….kwa sababu……..” Joe akashindwa kuendelea.
“Kwa sababu gani Joe? Please tell me”
“I feel so empty Paula....I feel so lost without you…” Joe akasema na kumfanya Paula ashushe pumzi .Baada ya kimya kifupi Paula akasema
“Joe you are not empty,you are not lost..I’m still here.Pamoja na ukweli kwamba hatutaweza tena kuwa pamoja lakini siku zote nitakuwa nipo kwa ajili yako.Nitakuwa rafiki yako na utaendelea kuwa mtu wa pekee maishani mwangu” Paula akasema.Joe akainua kichwa na kutazama juu kisha akasema
“Paula I’m so stupid..To let you go was the biggest mistake I’ve ever done and I’ll never forgive myself for that…” Joe akasema kwa masikitiko.
“Joe kila kitu kinachotokea kinapangwa na Mungu.Hata sisi kutengana ninaamini ni mpango wa Mungu ili niende nikamtumikie.Usijilaumu kwa hilo.Kuwa na amani siku zote Joe”
“Paula kila kitu kinapangwa na Mungu.Lakini kwa hil la kutengana kwetu hatuwezi kumlaumu Mungu.Hili limetokea kwa sababu ya ujinga wangu.Sikutakiwa kufanya vile.Sikutakiwa kutengana nawe Wewe ni mtu wa pekee sana maishani mwangu.Thamani yako kwangu hailinganishwi na kitu chochote kile.Paula ,ninafahamu nilifanya makosa na tayari nimeshachelewa kwa sababu tayari umeshafanya maamuzi ambayo hakuna mtu wa kuweza kuyabadili,lakini pamoja na hayo yote naomba ufahamu kitu kimoja kwamba kama wewe ulivyoamua kuitunza ahadi uliyonipa kwamba siku zote hutakuwa tayari kuwa na mwanume mwingine zaidi yangu,na mimi napenda kukuahidi leo hii kwamba sintakuwa na mwanamke mwingine katika maisha yangu.Wewe ndiye mwanamke wa pekee kabisa maishani mwangu.Siku zote nitakupenda na kukuenzi kama ua la pekee kabisa moyoni mwangu.Nafasi yako katika moyo wangu sintaweza kumpa mwanamke mwingine yoyote.Popote utakapokuwa ,fahamu kwamba ninakupenda na nitakupenda wewe pekee hadi mwisho wa maisha yangu hapa duniani.”
Kauli ile ya Joe ikamfanya Paula akae kimya kidogo,akavuta pumzi ndefu
TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO………………..
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment