Tuesday, April 8, 2014

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 7






RIWAYA : TEN CHAPTERS
SEHEMU YA 7
 


Wazee wale walionekana kuvutiwa sana na Genes na hawakutaka yeye na Naomi wandoke pale.Naomi hakukaukiwa na tabasamu.Alifurahi kupita kiasi.Kila mtu aliyemfahamu alikuwa akimtambulisha kwa Genes.Kila mtu alimsifu Naomi kwa kuwa na kijana mzuri kama Genes.Hakuna aliyefahamu kama Genes na Naomi ni marafiki wa kawaida tu na hawakuwa wapenzi lakini kwa muonekano wao usiku huu walionekana ni kama wapenzi walioendana sana.












  " Genes wewe ni rafiki yangu na sitaki kukuficha kitu.Ninaweza kusema kwamba nilikutana na yule kijana nikiwa bado mbumbumbu wa mapenzi.Awali kijana yule alikuwa akifanya kazi katika kampuni yetu.Alikuwa mwongozaji  watalii.Siku moja nilikwenda kikazi katika moja ya hoteli zetu iliyoko nje ya Arusha.Jioni nikiwa nimepumzika alikuja yule kijana na kuanza kuongea na mimi.Alikuwa akiiga gita huku akiimba nikafurahi sana.Nilifurahi kupata mtu wa kuongea naye kwa sababu nilikuwa nahisi upweke sana.Toka hapo ndipo urafiki kati yangu naye ulipoanza.Tulitokea kuwa marafiki wakubwa sana.Kwa bahati mbaya kijana yule alifukuzwa kazi katika kampuni yetu na hakuwa na mahala pengine pa kwenda na kama rafiki yake nikamuonea huruma na kumpa hifadhi nyumbani kwangu.Nilimpa chumba kimoja cha kulala kwa kuwa wakati huo nilikuwa nimepanga katika nyumba ya vyumba vitatu.Nilimpa hifadhi ya wiki moja tu ili aweze kutafuta sehemu nyingine ya kuishi lakini siku zilidi kwenda nikajikuta nikishindwa kumuondoa pale kwangu Tayari nilikwisha mzoea sana na sijui kitu gani kilinipelekea mimi kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na kijana yule.Nilijikuta nikimpenda na tukawa katika mapenzi moto moto.Kwa kweli ninajuta sana kila nikikumbuka muda nilioupoteza na yule kijana.Nilikuja kugundua kwamba alikuwa ni kijana mlevi,mvuta bangi na mwingi wa wanawake.Kwa kuwa alifahamu kwamba mimi sina kauli kwake alinipeleka alivyotaka.Kila nilipopata mshahara aliuchukua na kuupeleka katika starehe. Sikuwa na kitu cha kufanya zaidi ya kulia.Nitaendelea kukushukuru sana kwa kunisaidia kumuondoa yule muhuni nyumbani kwangu." akasema naomi kwa sauti yenye majuto ndani yake.Genes akamuangalia kisha akauliza






















































KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI

0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi