MASIMULIZI
Tuesday, April 8, 2014
" BEFORE I DIE " SEHEMU YA 7
RIWAYA: BEFORE I DIE
SEHEMU YA 7
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kabla hajaendelea Marina akaanza kucheka.
“hahahahahaaaaa !! leo umenifurahisa sana Innocent.Yaani mimi Marina nikasome?
“Ndiyo Marina hilo linawezekana kabisa.Marina unahitaji kukubali mabadiliko.bado u msichana mdogo na ambaye hustahili kuishi maisha haya unayoyaishi.”
“Innocent kama unataka kunisaidia ,labda unipe fedha za kutosha”
“Fedha si tatizo Marina.Ninaweza kukupa mamilioni ya fedha lakini hayatakusaidia kitu chochote.Ninachokitaka ni mabadiliko ya kifikra,kimaisha na kiroho pia.Unatakiwa uishi maisha yenye kumpendeza Mungu siku zote na ni yeye ndiye atakayekunyooshea mkono wake na kukumiminia baraka zake nyingi na utakuwa na maisha ya amani na furaha tele daima.”
“hahahaaaa ! Leo nimekutana na mchungaji..Hahahaa” marina akacheka kwa nguvu.
“Kumbe hata ninyi wachungaji huwa mnafuata makahaba..hahahaaa”
Innocent hakujibu kitu akaendelea kumtazama Marina aliyekuwa akicheka kicheko kikubwa.
ENDELEA………………………………
“nadhani hatutaweza kuelewana.Tayari amekwisha
lewa huyu.Ngoja nimsubiri mpaka asubuhi ulevi utakapokuwa umemtoka kichwani.Amenigusa sana mtoto huyu ,kamwe siwezi kuacha kumsaidia.Atake asitake ni lazima abadilike.Nitafanya kosa kubwa sana iwapo nitamuacha mtoto mzuri kama huyu aendelee kupotea.Mungu aliyenipa mimi uwezo ndiye aliyemnyima huyu binti hivyo ninapaswa kumsaidia kwa kila namna ninavyoweza.” Akawaza Innocent huku akimtazama Marina ambaye alikuwa ameanza kusinzia.Inno akamlaza vizuri pale sofani halafu akachukua shuka akamfunika vizuri yeye akapanda kitandani akajilaza.Ni usiku ambao Innocent alikuwa
na mawazo mengi sana kuhusiana na jinsi atakavyomsaidia Marina.
Saa kumi na mbili za asubuhi Innocent akaamka.Kitu cha kwanza ilikuwa ni kumtazama Marina kama yupo kwa sababu alikwisha sikia sifa za makahaba kwamba huvizia usiku ambapo mteja wake amelala fofofo kisha hubeba kila kitu na kutokomea zake .Marina bado alikuwa amelala pale sofani.
Inno akainuka pale kitandani akanawa uso halafu akamwamsha Marina.
“Ouh kumbe kumekucha? Marina akasema kwa uchovu huku akiinuka na kujinyoosha.
“Amka nikupeleke nyumbani kwako” Innocent akasema
Marina akakaa pale sofani huku ameinama chini.baada ya dakika kama mbili hivi akainua kichwa na kuiona chupa ile ya mvinyo akaitikisa na kukuta bado mvinyo ulikuwepo akajimiminia katika glasi na kuunywa wote.
“Du ! Afadhali nimezimua manake nilikuwa nahisi kufa kufa.” Marina akasema huku Innocent akimtazama kwa mshangao.
“twende ukaniache mitaa ya kati” Akasema Marina
“nataka nifahamu mahala unapoishi” Innocent akasema
“Mimi naishi gheto na washkaji zangu.Mtu kama wewe hapakufai”
“Usijali Marina.Hata kama ungekuwa unaishi jalalani ningekufuata tu kujua mahala unapoishi” Innocent akasisitiza.
Wakatoka mle hotelini na kuingia garini na safari ikaanza ya kuelekea mahala anakoishi Marina.
“Simamisha gari hapa kwa sababu huko tunakoenda gari yako haiwezi kupita.” marina akamwambia Innocent ambaye alisimamisha gari wakashuka.Marina akamuita kijana mmoja aliyekuwa amesimama katika kibaraza kimoja.
“Juma hebu ilinde hii gari ya mshkaji naingia naye hapo maskani.Usijali jamaa atakutoa na kitu kidogo” Marina akasema huku akiwasha sigara.Innocent akatoa noti mbili za elfu kumi kumi na kumpatia yule jamaa aliyezipokea huku akishukuru.
Toka walipoacha gari walitembea kama mita mia mbili ,wakafika katika nyumba moja iliyochakaa,wakazunguka uani na kuingia katika chumba kimoja kilichokuwa na giza.
“Karibu Innocent.hapa ndio maskani kwetu” marina akasema huku
akilifungua dirisha kwa ajili ya kupata mwanga na hewa. Innocent akapigwa na butwaa kwa mambo aliyoyaona mle ndani.Chumba kilinuka harufu mbaya ya uvundo iliyochanganyika na harufu ya moshi wa sigara,na bangi.Kondom zilizokuwa zimetumika zilitapakaa hovyo mle ndani.Juu ya mfuko wa nailoni kulionekana mabomba matatu ya sindano ambazo huwa wanazitumia katika kujidunga madawa ya kulevya.Mle ndani kulikuwa na kitanda kimoja ambacho juu yake walilala wasichana watano wengine wakiwa uchi.Innocent akahisi kama anataka kutapika.Akatoka nje
akapiga chafya mfululizo ..
“Du ! siamini kama ndani ya chumba kile wanakaa binadamu. Chumba kidogo namna ile wanalala watu zaidi ya saba !!….” Wakati akiendelea na kuwaza alichokiona mle ndani akatoka mwanadada mmoja aliyevaa kaptura fupi na fulana ndogo .Mikononi alikuwa amejichora michoro
na maandishi mengi.Macho yake yalikuwa mekundu na kwa jinsi alivyoonekana hakuwa mtu wa masihara.Moja kwa moja akamuelekea Innocent pale alipokuwa amesimama.
“kaka habari” Akasema dada yule mwenye sauti nzito kama ya mwanaume.
“Nzuri habari yako” Innocent akajibu
“Wewe ndiye umekuja na Marina? Akauliza kwa sauti ya ukali
“Yes ndiye mimi” Innocent akajibu.
“Mbona sasa uko nje? Si tabia nzuri hebu karibu ndani ukae.Au umeona hapalingani na hadhi yako?.Karibu ndani nina maongezi kidogo na wewe.Mimi ndiye mkubwa wa ghetto hili.” Akasema dada yule huku akigeuka na kurudi chumbani.Kwa kuwa alikuwa na lengo la dhati la kumsaidia Marina Innocent akakubali kurudi tena mle chumbani.Akafunua pazia na kuingia ndani.Kitu cha kwanza alichokutana nacho ni moshi wa bangi.Yule dada aliyesema kwamba yeye ndiye mkuu wa chumba kile alikuwa amegeukia ukutani akivuta bangi.Marina alikuwa amekaa chini pembeni ya kitanda akiwa anachambua bangi Innocent akapewa ndoo ya maji akalie kwa kuwa ndani mle hakukuwa na kiti wala kitu chochote cha kukalia.Kwa dakika zile chache alizokuwa amekaa mle ndani Innocent akahisi kama kizungu zungu kutokana na moshi wa bangi uliokuwa umejaa mle ndani na kusababisha kukosekana kwa hewa ya kutosha.
Akiwa bado anashangaa shangaa akastukia akishikwa mabega na yule dada mkubwa wa kile chumba.Kabla hajajua nini kinaendelea akajikuta akifunguliwa vifungo vya shati.Akasimama.
“Nini kinaendelea hapa? Innocent akauliza kwa mshangao
“Ina maana hujui kinachoendelea? Mwanaume yoyote akiingia humu ndani kitu cha kwanza ni lazima alale na mimi kwanza.Nashukuru Mungu Marina amekuleta kwa sababu usiku kucha wa jana sijapata mwanaume hata wa kulala naye bure.Leo utakata kiu yangu” Akasema dada yule mwenye sauti nzito na ambaye alionyesha kutokuwa na masihara.Macho yake yalikuwa mekundu na yaliashiria hakuwa akitania kwa kitendo kile.Kwa kasi na nguvu Innocent akamsukuma dada yule akaangukia ukutani na hivyo kumpa nafasi ya kuweza kuponyoka.Kabla hajatoka mlangoni akakutana na dada mwingine ambaye naye alikuwa akirudi kutoka katika mihangaiko yake.
“Ziada hebu mzuie huyo” Akasema yule dada aliyesukumwa na Innocent akimwambia yule mwenzake aliyesimama mlangoni amzuie Innocent.Ziada aliyekuwa amesimama mlangoni akamsukumia Innocent ndani na kujikuta akidakwa shati na dada yule aliyemuangusha chini.Ikaanza purukusahani kubwa kati ya wale akina dada na Innocent.Purukushani zile zikawavuta majirani ambao walimuokoa Innocent ambaye kwa wakati huo hakuwa na shati.Suruali yake ilikuwa imechanwa chanwa.Simu yake ilikuwa imechukuliwa halikadhalika pochi yake iliyokuwa na fedha.
“Nini kimetokea hapa? Mjumbe wa eneo lile ambaye alifika mara moja baada ya kuarifiwa kuhusu vurugu ile aliuliza.
“Mjumbe, huyu kaka amelala na mdogo wangu Marina na asubuhi hii amekataa kumlipa fedha na kutaka kukimbia,ndio maana tumeamua kumfundisha adabu ili asirudie tena kitendo kama hiki.” Akajibu mwanadada yule mkubwa wa ghetto.
“Eti Marina ni kweli hayo anayoyasema Mwanaidi? Mjumbe akauliza
Marina akakaa kimya huku akitazama chini.
“Marina hebu sema ukweli haraka “ Akaamrisha Mwanaidi ambaye alionekaa kuwa na amri kwa wasichana wote waliokuwa wakiishi katika chumba kile.
“Ni kweli mjumbe” Marina akasema huku akitazama chini.Innocent hakuyaamini masikio yake.Akabaki akiuma meno kwa hasira.Alikosa la kuongea.Hakutegemea kama Marina angeweza kumgeuka kiasi kile.
Mjumbe akamshika mkono Innocent na kuanza kuondoka naye eneo lile ambalo tayari lilianza kujaa watu.Innocent alihisi aibu ya aina yake.Katika maisha yake hakuwahi kuaibika kiasi kile.Alikuwa kifua wazi hakuwa na shati wala viatu.Suruali yake ailikuwa imechanwa chanwa.Kila mtu aliyekuwa akimuona alikuwa akimcheka.
“Huyooooo…kaumbuka leo”
“Sharobaro kaumbuliwa na changu doa !!!!…” Hizi zilikuwa ni kauli za kubeza zilizotolewa na watu walioshuhudia kitendo kile.Zilimuumiza mno Innocent .
“Kijana ninavyokuona wewe hufanani kabisa na mazingira haya.Kwa nini lakini umeamua kujidhalilisha namna hii kijana wangu?”
Mjumbe akasema huku akimuongoza Innocent nyumbani kwake kwa madhumuni ya kumpatia shati la kuvaa na viatu.
“Mjumbe sijui hata nikueleze nini.Hapa nilipo siwezi hata kuongea.Katika maisha yangu sijawahi kukutwa na tukio kama hili la leo.Tukio hili limenifunza mambo mengi sana.Nashukuru mjumbe kwa kuniokoa kwa sababu mabaradhuli wale walikuwa wanifanyie kitu kibaya sana.” Innocent akasema
“Unatakiwa uwe makini sana unapojihusisha na akinadada kama wale.Si watu wazuri hata kidogo.Hata sisi hapa mtaani tuna mpango wa kuwaondoa kwa sababu imekuwa kero kubwa kwa watoto na wake zetu.Mipira ya kiume iliyotumika inaonekana imezagaa hovyo maeneo wanayoishi na watoto wetu wadogo wanaiokota na kuichezea kitu ambacho ni hatari kubwa.Sisi kama serikali ya mtaa tumefikia uamuzi wa kuwaondoa kabisa maeneo haya.Zoezi hili la kuwaondoa litaanza hivi karibuni” Akasema mjumbe.Innocent alikuwa amejiinamia chini akitafakari.
Mjumbe alimpatia shati suruali na viatu.Ingawa hazikumtosha Vyema lakini alishukuru kwa msaada ule uliomsitiri na aibu ile kubwa iliyompata.
“Mjumbe nashukuru sana mzee wangu kwa msaada wako huu mkubwa.Sijui ningepita mtaa upi leo.Hili ni fundisho kwangu.Sina cha kukupa mjumbe lakini naomba siku ya jumatatu ufike katika kampuni ya Benard & Sons company useme unahitaji kuonana na ndugu Innocent basi utaletwa moja kwa moja kwangu.Nahitaji kukupa ahsante kwa msaada wako mkubwa ulionisaidia..Tafadhali usikose mzee” Innocent akasema
“Nitafika bila kukosa .Siwezi kukosa kijana wangu..Halafu kabla hujaondoka mimi naitwa Bw.Mustapha kinyezi mwenzangu unaitwa nani?
“Mimi naitwa Innocent “ Innocent akasema huku akiinuka na kuanza kuondoka huku akisindikizwa na mjumbe hadi mahala alipokuwa ameegesha gari lake.
“Mjumbe nashukuru tena kwa kila kitu.Nadhani tutaonana hiyo jumatatu” Innocent akasema huku akiufungua mlango wa gari.Katika mapambano yale na wale makahaba kitu kikubwa alichokuwa akikichunga ni funguo za gari .Bahati nzuri hazikuweza kupotea.
“Hili ni gari lako” akauliza mjumbe kwa mshangao
“ndiyo Mjumbe hili ni gari langu” Innocent akajibu na kuagana na mjumbe ,akaliondoa gari kwa kasi maeneo yale .
*
*
*
*
Hakuna mtu aliyegundua kwamba Innocent alikuwa akiendesha gari huku machozi yakimtoka.Aliumia mno kwa kitendo alichofanyiwa.
“Siamini kama wema wangu leo umetaka kunitokea puani.Makahaba wale wameniabisha mno .Aibu niliyoipata ni kubwa mno.Nimetaka kubakwa hivi hivi.”
Akawaza Innocent.
Saa nne za asubuhi akawasili nyumbani kwao.Alikuwa amesawajika sana .Hakutaka kuongea na mtu yeyote moja kwa moja akaelekea katika chumba chake kujipumzisha.
“Bado siamini kama mtu ninayeheshimika kama mimi nimedhalilishwa na machangudoa.Wamenichukulia kila kitu nilichokuwa nacho.Kama si kwa jitihada za mjumbe wangefanikiwa kunibaka wale wanaharamu.I hate them so much.Halafu Marina naye alikuwa yuko radhi kuona nikiaibishwa .Hakuwa akijali chochote.Na hata alipoulizwa kama ni kweli nililala naye na kumdhulumu fedha zake alikubali kuwa ni kweli …Masikini pamoja na wema wangu wote na kuonyesha kila dalili za kutaka kumsaidia lakini bado hakuonyesha jitihada zozote za kuukubali msaada wangu.Aliipata bahati ambayo wenzake wanaitafuta usiku na mchana lakini yeye ameichezea na kuitupa mbali….Masikini mtoto mdogo kama yule anaangamia hivi hivi.Mtoto mzuri mwenye umbo safi na zuri anapotea hivi hivi jamii ikimuona…..Anyway sina namna nyingine ya kuweza kumsaidia.Kwa vile yeye mwenyewe ameonyesha hataki mabadiliko katika maisha yake na mimi sina budi kuachana naye.” Innocent akawaza akiwa kitandani kwake usingizi ukamchukua akalala.
TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO………
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment