MASIMULIZI
Wednesday, April 9, 2014
SERENA SEHEMU YA 8
RIWAYA : SERENA
SEHEMU YA 8
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“I promised to hug you tightly and this is the day………..this is the day……this is the day…….uuh.” Akasema Stella huku akizidi kumkumbatia Jason kwa nguvu na kumpiga mabusu mazito mazito.Jason hakujibu kitu aliendelea na zoezi la kuuvinjari mwili wa Stella.Mkono wake wa kulia ukashuka chini ya shingo ya Stella akiwa anapapasa taratibu mara Stella akastuka na kutoa mguno mkubwa.
“ouh ! Jassssssss……!!!”
Jason hakuacha akaendelea na zoezi lile kwa umakini na ufundi mkubwa.
“ouh Gosh ! what a sexy lady” Akawaza Jason .Akauzungusha mkono wake wa kulia na kuifungua zipu ya lile gauni la Stella na taratibu akalivua na Stella akabaki na nguo ya ndani.Jason mzuka ukampanda baada ya kuushuhudia mwili ule na mzuri wa binti huyu aliyeumbwa akaumbika .
“Jasss I need you now………..” Akaguna Stella.Jason ambaye naye hali yake ilizidi kuwa mbaya akavua nguo na kumvuta Stella karibu yake na dakika tatu baadae ikaanza kusikika milio na miguno ya kimahaba.Tayari walikuwa katika sayari nyingine kabisa.
ENDELEA…………………………………….
Jason alikuwa wa kwanza kustuka toka usingizini .Kifuani pake alikuwa amelala Stella Kamutere mwanamke mwenye uzuri wa kipekee kabisa. Picha ya matukio ya usiku ikamjia na kumweka Jason katika fikara nzito.
“Gosh !.Siwezi kuusahau usiku wa jana maishani mwangu.Ulikuwa ni usikuwa kipekee kabisa.I enjoyed a lot.Stella is so wonderfull..….” Akawaza Jason huku akizichezea nywele za Stella
“Ninaanza kujikuta nikimpenda Stella.” Akawaza Jason na mara Stella akaamka
“Morning Jason” Akasema Stella kwa sauti yenye usingizi huku akimkumbatia zaidi Jason.
“Morning Stella.Unajisikiaje?
“Ouh I cant say.Please hug me tight” akasema Stella
Jason akamkumbatia Stella ambaye aliinua
kichwa na kumtazama Jason kwa makini usoni.
“Mbona unaniangalia hivyo ? Jason akauliza
“Jason kuna kitu ambacho nilikuwa nataka kukwambia lakini nilikuwa natafuta namna ya kuanza.I think now it’s the perfect time that you know.”
Stella akavuta pumzi ndefu ,huku Jason akizidi kumkodolea macho kwa shauku ya kutaka kufahamu alichotaka kuambiwa na Stella.
“Jason I love You.I love you more than you can imagine.Toka siku ile nilipokuona shuleni kwenu nilihisi kusisimka mwili na toka siku ile niliapa ni lazima uwe wangu.Jason sijui jinsi ya kujieleza vizuri kabisa lakini naomba tu ufahamu ya kuwa you are that man I’ve been dreaming for.A man of my dreams.A man whom I breath for,I’ve done everything I could just to have this moment to tell you how much I love you…and please Jason don’t say anything yet…” Stella aliongea kwa hisia kali huku machozi yakimtoka. Jason akamfuta machozi ,akamvutia kwake na kumpiga busu moja matata sana.
“Stella don’t cry .Usilie my angel.Tafadhali naomba usitoe machozi.” Akasema Jason halafu akakaa kimya kidogo akamtazama Stella usoni na kusema.
“I love you Stella.I love you very very much.”
Stella akapandwa na uchizi wa ghafla baada ya kuisikia kauli ile ya Jason,akamrukia na kumpiga mabusu mfululizo.
“Ouh Thanx God….thanx God.This is the man I love.I love this guy” Akasema Stella huku akiweweseka kwa furaha.
Penzi jipya likachipua na kumea kama kasi ya mwangaza.
PATRICK CHARLES MEMORIAL HOSPITAL
Kila mtu ndani ya chumba kile akageuka na kumwangalia Dr Jason aliyekuwa amemtumbulia macho Serena.Moyo wake ulipatwa na mstuko hakutegemea kumuona Serena sehemu kama ile baada ya miaka mingi kupita.Serena bado alikuwa na uzuri uliopindukia uzuri ambao kwa sasa uliongezeka mara dufu.Ni sura hii ambayo Jason imekuwa ikimtesa Jason kwa miaka mingi hadi alipoamua kuwa na Stella baada ya kujua kwamba hataonana tena na Serena katika maisha yake.Pamoja na kuufungua ukurasa mpya na Stella bado sura
ya Serena imekuwa ikimjia Jason kila mara na ndiyo maana alipomuona tu mle chumbani alistuka sana na
kuishiwa nguvu akidhani labda ameona mzuka.
Serena naye alistuka sana alipomuona Dr Jason.Alibaki ameduwaa akimtazama asiyaamini macho yake.Ni muda mrefu umepita toka alipomuona Jason kwa mara ya kwanza tena usiku na akatokea kumpenda lakini kwa muda huo wote hajawahi hata siku moja kumsahau kijana huyu ambaye amekuwa akiusumbua moyo wake kwa muda mrefu mno.Aliwahi kumuona mara moja tu kijana huyu na toka siku hiyo picha yake haikufutika moyoni mwake.Jason ndiye alikuwa sababu ya yeye kuhamishiwa nchini Marekani kwa kigezo cha masomo lakini nyuma ya pazia ni kumuweka karibu na kijana mtoto wa tajiri Kenneth Mclay Patel kitu ambacho baadae ilikuja kudhihirika kwamba hakiwezekani kwa sababu akili ya Serena ilikuwa kwa mtu mmoja tu Jason ambaye ndiye aliyempenda na hakujua angemuona wapi.
Kila mtu ndani ya chumba kile aliendelea kuwaangalia Jason na Serena na kuwashangaa.Hakuna aliyeelewa ni kwa nini wote wawili walipatwa na mstuko mkubwa baada ya kuonana. Wakati chumba chote kikiwa kimya kabisa na watu wakiendelea kutafakari kilichotokea Dr Henry akasimama na kusema
“ Dr Jason karibu.Kutana na familia ya Mzee Albano.Huyu ni mama yao Mrs Albano na hawa ni binti zake Serena na Isabella.” Akasema Dr Jason na kuendelea
“Mama na kina dada pale huyu ndiye daktari wetu bingwa wa mambo yote yanayohusiana na ubongo na uti wa mgongo anaitwa Dr Jason.Nafikiri mtapata nafasi ya kumfahamu zaidi kwani yeye ndiye anayehusika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa mzee Albano.”
Dr Henry akamaliza kutoa utambulisho mfupi.
Jason akatabasamu na kwenda kupeana mkono na mke wa mzee Albano akamsalimu kwa adabu,alafu akamsalimu Isabella na mwisho ni Serena.Wakatazamana kwa sekunde kadhaa kiasi kwamba kila mtu mle chumbani akahisi kuna kitu kinaendelea baina yao.Dr Jason akaenda kukaa huku akihisi kutokwa na kijasho chembamba.
“This is not coincidence.After all these years…!! Leo ninakutana tena na Serena katika mazingira kama haya…ouh gosh !.This is unbelievable.”Akawaza Jason huku akimtazama Serena ambaye naye hakuacha kumtazama Jason..
Dr Henry akasimama na kutoa utambulisho mfupi kwa wajumbe wote wa kikao kile na kuelezea sababu iliyofanya wakutane pale kisha akaliacha jukumu zima kwa Dr Jason ili aweze kutoa ufafanuzi kwa familia ya mzee Albano.
Dr Jason akasimama akaelekea mbele na kuanza kuuchambua ugonjwa wa mzee albano na kuonyesha ni kwa jinsi gani hospitali ya kule India walishindwa kuona sababu ya kufanya upasuaji katika ubongo wa mzee albano.Akaelezea pia kwa ufasaha ni kwa nini ana uhakika kuwa operesheni anayotaka kuifanya itafanikiwa na kuokoa maisha ya mzee Albano.
“Si mara yangu ya kwanza kufanya upasuaji mkubwa kama huu.Nina uhakika kuwa upasuaji huu utafanikiwa na Mzee albano atapona na kuwa mzima tena.Ninaomba familia na ndugu wa mzee albano wakubali tuifanye operesheni hii japokuwa wamekwisha hakikishiwa kuwa mzee wao hatapona tena.Nawahakikishia kwa mara nyingine
mzee Albano atapona.” Akamalizia Dr jason huku akitabasamu kama ilivyo kawaida yake.Akatoa kitambaa na kujifuta jasho licha ya ukumbi huo kuwa na kiyoyozi.
Mke wa mzee Albano akasimama na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa msaada mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa kumuuguza mume wake halafu akaweka wazi msimamo wa familia.Wao kama familia hawakuwa na kipingamizi chochote cha kuzuia operesheni ile isifanyike kwani wao walichokihitaji ni mzee Albano kuwa mzima.Kama kuna namna yoyote inayoweza kufanyika ili mzee wao aweze kupona wao hawana tatizo.Ruhusa ikatolewa kwa operesheni ile kufanywa.
Baada ya kauli ile ya mke wa mzee albano wajumbe wakainuka na kwenda kumpongeza kwa ujasiri wake na kumtakia kila la kheri.Jason akaandika kitu Fulani katika kijikaratasi kidogo akakishika mkononi.Akainuka pale alipokuwa amekaa akaelekea moja kwa moja alipokuwa amesimama mama Albano na Dr Henry wakiongea, akampa mkono mama albano..
“Mama usihofu kitu.Naomba uzidi kuwa na moyo na utuamini.Mzee atapona tu” akasema Dr Jason
“Daktari nashukuru sana kwa msaada wenu.nazidi kuwaombea Mungu awatie nguvu na mtusaidie mzee wetu aweze kupona.”
“Amina mama Mungu atatusaidia”Akasema Dr
jason
Alipogeuka macho yake yanakutana na macho ya Serena aliyekuwa akimuangalia kwa makini kana kwamba haamini alichokiona.Serena alikuwa katika mstuko mkubwa tangu kikao kilipoanza.Jason akamuendea.
“ you are Serena,right?” akasema Jason huku akimpa mkono na kumuachia kijikaratasi mkononi.
“Tafadhali endeleeni kumpa mama moyo katika kipindi hiki kigumu.Mzee atapona.Mungu atajaalia” akasema Dr Jason huku ameushika mkono wa Serena.
Serena akaushika kwa nguvu mkono wa Jason ,akamtazama machoni
Jason akagundua kitu katika mtazamo ule,taratibu akautoa mkono wake katika mkono wa Serena .
“Ok kwa sasa nina kikao na madaktari.Tutazidi kuwapa taarifa kadiri maandalizi yanavyokwenda.”Jason akasema huku akiondoka.Hakutaka kumpa Serena nafasi ya kusema lolote .
‘Dr…………”Serena alitaka kutamka kitu lakini mama yake akageuka na kumfanya anyamaze.Akiwa ameongozana na mdogo wake Isabella walitoka nje ya ukumbi ule wa mikutano halafu akaukunjua mkono wake akakitoa kile kijikaratasi alichopewa na Dr Jason.Kiliandikwa hivi
“+255764294499 call me this afternoon.”
Serena mikono ikaloa jasho.
TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment