Wednesday, April 9, 2014

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 8






RIWAYA : TEN CHAPTERS
SEHEMU YA 8
 





  " She's so sexy.Ana mvuto wa kipekee kabisa na wa aina yake.Anavyotembea ni kama hataki kukanyaga ardhi.Naomi amebarikiwa uzuri wa asili .Najisikia fahari kubwa kuwa karibu naye kwa usiku wa leo na kupata heshima kubwa.Hii ilikuwa ni ndoto yangu ya siku nyingi ya kutaka kuwa karibu na msichana huyu anayeufanya moyo wangu ukose utulivu kila nimuonapo.Sielewi ni kwa nini aliamua kupoteza muda wake mwingi kwa kuwa katika mahusiano na  yule kijana muhuni ambaye hakuwa saizi yake.Naomi anahitaji mwanaume ambaye atamtunza atamjali,atamthamini na kumpa furaha maishani.Mwanaume ambaye atahakikisha kwamba lile tabasamu la kimalaika alilonalo Naomi haliondoki usoni pake hadi siku anaingia kaburini.That man is me.Ninajiamini ninaweza kuyafanya hayo yote kwa sababu ninampenda sana Naomi.Nimempenda toka siku ya kwanza jicho langu lilipomuona na toka siku ile nimeendelea kumpenda Naomi kila siku.Nimekuwa nikiomba usiku na mchana niweze kuipata walau nafasi ya kuweza kuwa karibu na mrembo huyu na leo Mungu amesikia maombi yangu na tazama leo hii nina kwenda kulala hoteli moja na mtu ambaye nimekuwa nikimuotya usiku na mchana .Naona ni kama muujiza fulani hivi.Dunia hii imejaa maajabu mengi sana.Pamoja na hayo ninajipongeza hata mimi mwenyewe kwani hatua hii niliyofikia si ndogo.Ninaamini tayari nimeanza kuingia taratibu katika maisha ya Naomi na usiku wa leo nimejizolea alama za kutosha.Harakati zangu zinaendelea vizuri .Nitafanya kila niwezalo ili niweze kumpata Naomi .Siwezi kumuacha akaondoka mikononi mwangu na kutua katika mikono ya mwanaume mwingine.Mimi ndiye mwanaume wa maisha yake." Genes akakatishwa mawazo yake na sauti ya Naomi akisalimiana na wahudumu wa mapokezi.Ilionekana ni kama vile walikuwa wakifahamiana kwa sababau baada ya salamu walitaniana kidogo ikiwa ni pamoja na kumsifia Naomi namna alivyopendeza  usiku huu..Baada ya maongezi ya dakika kama mbili hivi Naomi akamtambulisha Genes kwa wahudumu wale.


0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi