MASIMULIZI
Monday, April 7, 2014
TEN CHAPTERS SEHEMU YA 6
RIWAYA : TEN CHAPT
ERS
SEHEMU YA 6
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Maongezi yaliyojaa vicheko na utani wa hapa na pale yakaendelea.Naomi alifurahi kupita kiasi.Hakuwahi kuipata furaha ya namna hii hapo kabla.Alitamani kila siku iwe ni kama usiku huu yaani awe karibu na Genes.Saa tatu za usiku wakarejea nyumbani na kuagana
kila mmoja akaelekea chumbani kwake.
Mpaka saa sita za usiku bado Genes hakuwa ameupata usingizi.Alikuwa akikumbuka usiku huu wa kihistoria kwake.Ni usiku huu ambao aliweza kumsoma vizuri Naomi a kugundua kwamba pamoja na uzuri alionao lakini pia ni mwanamke mwenye akili nyingi na uelewa mpana wa mambo.Alizidi kumpenda Naomi zaidi baada usiku ule.Picha ya Naomi akitabasamu ikamjia mara kwa mara nakumfanya atabasamu .Wakati bado akimuwaza Naomi mara ujumbe wa mfupi wa maandishi ukaingia katika simu yake.Ulitoka kwa Naomi
" Genes ninashindwa kupata usingizi kutokana na furaha niliyo nayo leo .Genes naomba nikushukuru tena kwa usiku wa leo..You real made my night.Thank you and good night" Genes akatabasamu na kurudia kuusoma ujumbe ule tena na tena kisha akarejesha majibu
" Hata mimi nashukuru sana Naomi kwani nimefurahi mno na kilichonifurahisha zaidi ni kukuona ukiwa na furaha na amani ya moyo.Nafurahi kukuona ukitabasamu na kucheka tena.Naomi I'll always be here anytime you need a friend...Sleep tight. Akaubusu ujumbe ule kisha akautuma.
ENDELEA..........................................................................................
Ni Jumatatu wiki mpya ikaanza.Ni wiki ambayo wote Genes na Naomi walikuwa na furaha kubwa mioyoni mwao.Kwa Naomi tukio la kupata chakula cha usiku na Genes bado liliendelea kukaa kichwani na kumfanya atabasamu kila akkumbuka.Kwa upande wa Genes alikuwa na furaha kubwa kwa sababu alianza vizuri harakati za kumpata Naomi msichana mwenye uzuri wa kipekee mno.Katika wiki hii Genes na Naomi walionana mara moja tu siku moja asubuhi .Naomi alikuwa ametingwa na shughuli nyingi wiki hii na alionekana mra chache sana nyumbani .Walikuwa wakiwasiliana kwa simu.Siku zilikwenda kwa kasi na hatimaye ikawadia siku ya ijumaa.Siku hii ni siku ambayo Genes alikuwa na furaha kuzidi siku zote.Ni siku ambayo angemsindikikiza Naomi katika sherehe ya kumuaga bosi wake wa zamani na kumkaribisha mpya.Kwa Genes kuambatana na Naomi katika sherehe kama hii kilikuwa ni kitu kikubwa sana na alikuwa akilala akiiota siku hii muhimu.
" Leo ndiyo siku yenyewe,ile siku niliyokuwa naisubiri kwa hamu kubwa.Naomi kuomba nimsindikize katika sherehe hiyo amenipa heshima kubwa sana.Hakuna shaka ameona ninastahili kuongozana naye.Kwa mujibu wa maelezo yake alisema kwamba hajawahi kuhudhuria katika sherehe yoyote na yule kijana muhuni kwa sababu hakuwa akistahili kwenda naye katika sehemu za heshima kama hizo.Nimepata nafasi ya dhahabu lazima niitumie ipasavyo.Nafasi kama hizi huwa ni chache sana kutokea." akawaza Genes huku akiifunga vizuri tai tayari kuwahi kazini asubuhi.
" Safari yangu ya kumpata Naomi mwanamke
ambaye moyo wangu unaamini kwamba hakuna mwingine zaidi yake imeanza
vizuri.Urafiki mkubwa unaanza kujengeka kati yetu na nina imani siku moja urafiki huu utageuka na kuwa uchumba.Wataalamu wa masuala ya mahusiano wanasema kwamba ili kupata ndoa iliyo njema na yenye furaha inapendeza kama wapenzi wakianza na urafiki halafu urafiki wao ukabadilika na kuwa uchumba na hatimaye ndoa.Nina imani siku moja Naomi atakuwa mchumba wangu na tutafunga ndoa.Hicho ndicho kitu pekee ambacho ninakiota kwa sasa.Kuwa na Naomi.Ameiteka akili yangu huyu msichana .Sijawahi kuumiza kichwa changu kwa kumuwaza msichana kama ninavyomuwaza Naomi.Natamani niwe namuona kila siku kabla ya kwenda kazini .Kila niionapo sura yake nasikia faraja na furaha moyoni mwangu." akaendelea kuwaza Genes huku akipakia nyaraka zake muhimu tayari kwa kuelekea kazini.
" Naomi ..Naomi ...Naomi..Leo ni siku ya
nne sijamtia machoni.Laiti angejua kama nisipomuona sipati usingizi angejitahidi nimuone kila siku asubuhi....Ouh Genes hatimaye umenasa katika penzi la Naomi na huna ujanja wa kujinasua tena." akasema kwa sauti ndogo genes, akasimama akafikiri jambo kwa dakika moja .
" Ngoja niwahi kazini..." akasema Genes , akazima vifaa vyake vinavyotumia umeme akafunga mlango
na kuondoka kuwahi kazini.
Japo uso wake ulijawa na tabasamu kubwa lakini moyoni alikuwa na mawazo mengi kwa kutomuona Naomi kwa siku nne.
" Naomi sijaonana naye kwa siku nne na hajanipa taarifa yuko wapi..Najua siwezi kumuuliza yuko wapi kwa sababu bado si mpenzi wangu lakini moyoni mwangu ninaungua kwa wivu.Ni vipi ikiwa huko aliko yuko na mwanaume mwingine? Ninaumia moyo kila nikiwaza jambo hilo lakini sina namna ya kufanya.Itanibidi niwe mvumilivu sana kwa Naomi.Lakini sidhani kama anaweza akafanya kama ninavyofikiri Naomi ni msichana anayejiheshimu sana..Lazima atakuwa ametingwa na kazi nyingi na ndiyo sababu tumeshindwa kuonana.." akawaza Genes huku akijipa moyo halafu akaendelea na kazi.
Saa tano za asubuhi wakati akiendelea na kazi simu yake ikaita.Akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Naomi.Haraka haraka akaipokea.
" Hallo Naomi"
" Hallo Genes..Habari yako?
" Habari yangu nzuri sijui wewe"
" Mimi mzima kabisa Genes ..vipi maendeleo yako."
" Ninaendelea vizuri Naomi..habari za siku mbili tatu"
" Habari nzuri.hatujaonana kwa siku kadhaa nimekuwa na kazi nyingi sana kiasi kwamba inanilazimu kulala huko huko hotelini.Nimekuwa nikimsaidia bosi wangu anayehama, kukabidhi ofisi kwa uongozi mpya ."
" Pole sana Naomi.Nilishangaa kwa kutokuona kwa siku kadhaa nikaogopa labda pengine kuna mtu amekwisha kuweka ndani" akasema Genes katika hali ya utani na kumfanya Naomi acheke
" Hapana Genes si hivyo ulivyofikiri..sihitaji kuwekwa ndani kwa sasa.Kumbuka ni wewe mwenyewe umekuwa ukinishauri hivyo kwamba nichukue muda kujipanga na kutafuta mtu ambaye atanifaa katika maisha yangu." akasema Naomi
" Ndiyo nakumbuka Naomi.Usijali nilikuwa nakutania"
" Hata mimi nilijua ni utani..Sasa Genes nimekupigia simu kukumbushia kuhusu ile sherehe niliyokuomba tuongozane wote."
" Ndiyo nakumbuka Naomi" akasema Genes kwa wasi wasi akitaka kusikia kama imeahirishwa ama la.
" Sherehe yenyewe ni leo jioni." akasema Naomi
" Bado nakumbuka Naomi.."
" Nashukuru kama bado unakumbuka.Nilifikiri umesahau ili nikukumbushe." akasema Naomi
"Hapana siwezi kusahau Naomi.Ninaikumbuka sana siku ya leo.."
" Ok vizuri ..Sasa ni hivi mimi nitakupitia hapo nyumbani mida ya saa moja na nusu za jioni.Si utakuwa umekwisha jiandaa? akauliza Naomi.
" Ndiyo Naomi .Muda huo tayari nitakuwa nimejiandaa..Ninatoka kazini mapema siku ya leo" akasema genes
" Ok.Nashukuru sana Genes kwa kukubali kunisindikiza katika sherehe hiyo." akasema Naomi
" Usijali Naomi nilikuahidi kitu chochote ambacho utakihitaji toka kwangu nitakupatia.Kwako wewe hakuna kitu nitakwambia hapana" akasema Genes huku akitabasamu.
" Nashukuru sana Genes.Tutaonana hiyo jioni" akasema Naomi na kukata simu.
Taratibu Genes akaiweka simu yake mezani kisha akaegemeza kichwa chake katika kiti.Akavuta pumzi ndefu
" Ouh Naomi..Naomi ..Naomi....! !! Unaifanya kaili yangu ishindwe kutulia kila mara nikiisikia sauti yako.Laiti ungejua ni jinsi gani moyo wangu unahitaji kuwa nawe ungeniruhusu haraka sana niingie moyoni mwako.Nakupenda sana Naomi..Nakupenda sana" akawaza Genes...
"Naomi amesema kwamba ni sherehe yake ya kwanza kwenda na mwanaume.Ameniona ninafaa kwenda naye sehemu za heshima kama hizi .Sintamuangusha hata kidogo.Nitamuonyeha kwamba hakukosea kuniomba tuongozane katika sherehe hiyo.Nitahakikisha Naomi anajiona ni mwanamke mwenye bahati kuogozana na mimi.Nitamfanyia vitu ambavyo hajawahi kufanyiwa.This is my day..Ni siku yangu ya kupiga hatua kubwa katika safari yangu ya kumpata Naomi msichana ambaye hana wa kufananishwa naye" akawaza Genes.
*******************************************
Saa ya ukutani ilionyesha ni saa moja kamili za jioni.Genes bado alikuwa mbele ya kioo chake kikubwa akiendelea kujitengeza kwa usiku huo muhimu kwake.Usiku huu alikuwa amevaa suti mpya nyeusi ilimyomkaa vyema na kumfanya aonekane ni kama mwanamfalme.Alijitazama mara mbili mbili katika kioo akatabasamu mwenyewe kwa namna alivyokuwa amependeza.
" Du ! sipendi kujisifu mwenyewe lakini kusema ukweli nimependeza sana siku ya leo." akasema kwa sauti ndogo akitabasamu. Alijipulizia kwa mara nyingine tena uturi wa gharama kubwa ambao huutumia aendapo katika sherehe kama hizi.Kwa yeyote ambaye hamfahamu Genes na angemuona kwa mara ya kwanza katika usiku huu angeamini kwamba ni mmoja wa wafanya biashara wenye mafanikio makubwa au ni kijana mwenye wadhifa mkubwa serikalini au ni kijana toka familia yenye uwezo mkubwa kifedha.Alipendeza isivyo kawaida kuanzia juu hado chini.
"Ni saa moja na dakika ishirini sasa.Nafikiri Naomi atakuwa njiani kwa muda huu.Ana kawaida ya kuheshimu sana muda na miadi." akawaza Genes halafu akarudi tena katika kioo akajitazama tena akatabasamu.
Saa moja na dakika thethini na tano mlango wake ukagongwa.
" Lazima atakuwa ni mwenyewe.Nilisema msichana huyu anajua sana kuheshimu miadi na muda." akasema Genes akielekea mlangoni.Akaufungua mlango na kukutana na sura yenye tabasamu la mshangao la Naomi.
Kwa sekunde kadhaa wote wakabaki wakishangaana.Genes alimshanga Naomi na Naomi alimshangaa Genes kwa namna alivyokuwa amependeza.
" Wow ! Naomi you look like an angel tonight" akasema Genes kwa mshangao huku akitabasamu
" Genes you are amazing..." akasema Naomi huku sauti yake ikiwa na kitetemeshi ndani yake.
" Karibu ndani Naomi." akasema Genes
" Ahsante genes.Nadhani ndiyo muda wenyewe huu.Tunaweza kuondoka kama uko tayari? akauliza Naomi.
" Mimi niko tayari Naomi" akasema Genes halafu akazima vifaa vyake vya umeme akaufunga mlango akatoka nje.
Gari jipya la kifahari lenye rangi nyeusi lilikuwa limeegeshwa nje ya nyumba ile.Genes akahisi lile ndio gari watakalolitumia kuendea katika sherehe.Toka ndani ya lile gari akashuka Naomi akamfungulia mlango Genes ambaye alibaki akishangaa.Kwanza alikuwa akiushangaa uzuri wa Naomi usiku huu halafu akashangaa kumuona Naomi na gari lile la kifahari.Naomi akaingia garini akaligeuza gari wakaondoka.Kila mmoja alikuwa akimtazama mwenzake kwa kuibia.Ni Genes ndiye aliyeanzisha maongezi.
"Naomi sikujua kama wewe ni dereva mzuri namna hii." akasema Genes huku akitabasamu.Naomi akatabasamu na kusema
" Ninafahamu kuendesha gari lakini mara nyingi huwa sipendi kuendesha .Ndiyo maana hata hili gari huwa ninalihifadhi kwa kaka."akasema Naomi na kumfanya genes azidi kushangaa.
"Hili gari ni lako? akauliza Genes.
" Ndiyo Genes.Hili ni gari langu mwenyewe.Kaka yangu anafanya biashara ya kuagiza na kuuza magari toka nje ya nchi nilimuagiza anitafutie gari zuri akaniletea hili"
" Hongera sana.Ni gari zuri" akasema Genes.
" Genes wewe unafahamu kuendesha gari?
" Ninafahamu..Nilijifunza nyumbani..Baba yangu ana gari ..lakini bado sina leseni"
" Vizuri..siku ukihitaji kupata leseni niambie ili nikusaidie kuipata.Ninafahamiana na watu ambao wanaweza wakakusaidia kuipata leseni hiyo ndani ya muda mfupi" akasema Naomi
"Nitashukuru sana naomi kama utanisaidia kuipata leseni"
" Usijali Genes.." akajibu Naomi huku akiwa makini zaidi katika usukani.
Safari ikaendelea kimya kimya .Ni sauti ya muziki iliyokuwa ikisikika pekee.Genes hakutaka kumsemesha Naomi ambaye alikuwa makini sana katika usukani.
" Sifahamu ni kwa nini Naomi aliamua kupoteza wakati na yule muhuni.Naomi ni msichana mrembo mno.Uzuri wake usiku huu umetia fora.Ni kama ninamuona kwa mara ya kwanza vile.Ninajihisi nina bahati iliyoje kuchaguliwa kuongozana naye katika sherehe kubwa kama hii.Wapo wanaume wengi ambao wangependa kuipata nafasi hii lakini amewaacha hao wote na kunichagua mimi.Lazima kuna kitu maalum ambacho amevutiwa nacho toka kwangu na ndiyo maana akaniomba niongozane naye kwa usiku huu.Nitahakikisha simuangushi katika usiku huu.Nitajitahidi kumfanya ajione ni kweli amekuja na mwanaume katika sherehe " akawaza Genes.Safari ikaendelea kimya kimya.Magari yalikuwa mengi sana barabarani usiku huu hivyo ikamlazimu Nami kuwa makini katika uendeshaji.
Saa mbili na dakika kumi wakawasili katika ukumbi inamofanyika sherehe.Nje ya ukumbi magari mengi yalikuwa yameegeshwa na watu kadhaa walikuwa wamesimama nje ya ukumbi ule wakibadilishana mawili matatu..Naomi akasimamisha gari katika maegesho.Haraka haraka Genes akashuka na kumfungulia mlango Naomi akashuka huku akitabasamu.Genes akamshika mkono Naomi wakaanza kuongozana kueleka ukumbini.watu waliokuwa wamesimama pale nje ya ukumbi wote wakapigwa na mshangao.Walikuwa ni wafanyakazi wenzake na Naomi.
" Wow ! Naomi..mbona unapita kimya kimya bila kututambulisha? akasema kijana mmoja aliyekuwa amesimama na wanawake wawili wakiongea na wote walionekana kupatwa na mshangao.Kwa mwendo wa madaha wakiwa wameshikana mikono kama wafanyavyo wapenzi wanaopendana sana Naomi akamuongoza Genes kuelekea ndani.
"Genes usiwajali hao wanafiki..siku zote wamekuwa wakinicheka leo nimewakata kauli.wote wamekaa kimya.Walitegemea labda ningekuja peke yangu kama ilivyozoeleka." akasema Naomi na kumfanya Genes atabasamu na kusema
" Usijali Naomi..I'm your man tonight...." Naomi akatabasamu baada ya kuisikia kauli ile ya Genes
" thank you" akajibu Naomi.
Baada tu kuingia ukumbini Naomi akakutana na watu wanne waliokuwa wamesimama karibu na mlango wa kuingilia na mikononi mwao walikuwa na glasi za vinywaji.Wote walipomuona Naomi akiwa ameongozana na Genes wakasitisha maongezi yao wakabaki wakimtazama kwa mshangao
"
Wow ! Naomi..you are amazing tonight ! " akasema mzee mmoja mnene aliyevaa suti ya kijivu.
Naomi akawasogelea akawasalimu wote kwa adabu,Genes naye alifanya kama alivyofanya Naomi.
" Naomi who is this handsome man you've broght here tonight? akauliza yule mzee mnene ambaye alikuwa mchangamfu sana.
Naomi akatabasamu na kisha akasema.
" gentlemen ! this is Genes..he's my friend.."
" Wow ! ..Naomi hujafanya vizuri hata kidogo.Siku zote hizi kwa nini hujatutambulisha kwa rafiki yako?
Akasema yule mzee Mnene . " hallow Genes...I'm Michael sipanya.Its nice to meet you...Naomi tunafanya naye kazi hapa tunamlea kama binti yetu..Ni binti mtulivu na mwenye heshima kubwa.Kila mtu anampenda sana.You are so lucky to have her...." akasema mzee Michael akiwa bado amemshika mkono Genes.
" Please take a good care of my daughter..if you'll make her cry you'll answer to me." akasema mzee Michael huku akitabasamu
" nashukuru kukufahamu mzee" akajibu Genes Naomi akiwa amesimama pembeni akitabasamu.
Naomi akamsogela Genes akaupitisha mkono wake kiunoni kwa Genes kisha akasema
"Genes huyu ndiye Mzee Michael..bosi wangu ambaye leo hii tunamuaga.Kwangu mimi yeye ni kama baba yangu.Usimuone anacheka namna hii lakini akiwa kazini ni mkali sana na huwa hataki mchezo " akasema Naomi kisha akendelea kuwatambulisha na wengine waliobakia.Wahudumu waliokuwa wakizunguka na masinia ya vinywaji walifika pale walipokuwa wamesimama.Genes akachukua glasi mbili za mvinyo mwepesi akampatia moja Naomi.Maongezi yakaendelea.Wazee wale walionekana kuvutiwa sana na Genes na hawakutaka yeye na Naomi wandoke pale.Naomi hakukaukiwa na tabasamu.Alifurahi kupita kiasi.Kila mtu aliyemfahamu alikuwa akimtambulisha kwa Genes.Kila mtu alimsifu Naomi kwa kuwa na kijana mzuri kama Genes.Hakuna aliyefahamu kama Genes na Naomi ni marafiki wa kawaida tu na hawakuwa wapenzi lakini kwa muonekano wao usiku huu walionekana ni kama wapenzi walioendana sana.
Ilipofika saa tatu za usiku sherehe ikaanza rasmi.Wageni wote waliokuwa wamesimama wakaomba waketi vitini na wale waliokuwa nje wakaombwa waingie ndani.Naomi na Genes wakachagua meza ya peke yao iliyokuwa pembeni sehemu lliyokuwa na mwanga hafifu wakakaa.Wakaangaliana kwa sekunde kadhaa usoni wote wakatabasamu.Naomi akatazama chini halafu akainua kichwa akataka kusema neo lakini muda huo huo muhudumu akafika wakachukua tena glasi mbili za mvinyo mwepesi.
SHEREHE IMEANZA..NINI KITATOKEA KATIKA SHEREHE HIYO.? MPENZI MSOMAJI TUKUTANE TENA KATIKA SEHEMU IJAYO YA SIMULIZI HII
KWA SIMULIZI ZAIDITEMBELEA HAPA MASIMULIZIA
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment