MASIMULIZI
Saturday, April 5, 2014
TEN CHAPTERS SEHEMU YA 5
RIWAYA : TEN CHAPTERS
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Naomi naomba usiendelee kuwa na mawazo ya aina yoyote ile kuhusiana na kilichotokea kati yako na Sheddy.Ni jambo la kawaida kwa wapenzi kuachana na hutakiwi kuwa na mawazo hata kidogo.Yaliyopita yamekwisha kwenda..Jipange na maisha ya mbele "Genes akasema
" Najitahidi sana kutokuwa na mawazo Genes lakini nashindwa"
" Bado unamuwaza Sheddy" akauliza Genes
" Hapana si hivyo Genes.Siwezi kupoteza hata sekunde moja kumuwaza muhuni yule.Ninamshukuru Mungu kwamba Sheddy ametoweka machoni na maishani mwangu."
"
Kama Tayari Genes amekwisha toweka maishani mwako mawazo ya nini Naomi?
" Ninawaza mambo mengi sana Genes.Ninawaza ni jinsi gani nitakavyoweza kuyatengeneza tena maisha yangu yaliyoharibiwa na yule muhuni.Ninawaza ni kwa namna gani nitaweza kuifuta aibu yote aliyonitia yule kijana.Sikufichi nimepata aibu kubwa sana
kwa kuishi na kijana yule.Sikuwa nikifahamu hata kidogo kwamba heshima yangu ilikuwa imeshuka na kupotea kwa kuishi na kijana yule.Najutia sana kupoteza muda mwingi na Sheddy.Najuta sana" akasema Naomi
" Naomi ,maisha ni kama darasa ambalo sisi sote tuko ndani yake na tunaendelea kujifunza kila uchao.Kila siku tunajifunza kutokana na makosa tunayoyafanya.Binadamu kukosea ni jambo la kawaida na sote tunakosea lakini kurudia kosa mara ya pili ndilo tatizo kubwa.Tunapogundua kwamba tumefanya kosa tunajitahidi kujirekebisha ili tusije rejea tena makosa.Usiumize sana kichwa kwa sababu tayari umekwisha ligundua kosa ulilolifanya ,kitu cha msingi ni kujitahidi kuyapanga tena maisha yako .Bado unayo nafasi kubwa ya kuweza kuyapanga tena maisha yako.Bado umri unaruhusu na zaidi ya yote bado ni msichana mrembo mno
na kwa usiku huu ouh my Gosh ! You are amazing..You are the queen of the night" akasema Genes huku akiusogeza mkono wake na kuuweka juu ya mkono wa Naomi uliokuwa juu meza.Naomi akastuka kama vile amemwagiwa maji ya baridi.Genes mwili ukamsisimka alipoyakutanisha macho yake na macho ya Naomi.
ENDELEA................................................
Macho ya Genes na Naomi yakakutana na kila mmoja akajikuta akisisimka.Hakuna aliyekuwa ametegema hali ile kutokea.Waliangaliana kwa sekunde kadhaa Genes akafungua mdomo wake na kutaka kusema neno lakini kabla hajasema neno lolote lile akatokea muhudumu akiwa na sinia lililokuwa limejaa matunda.
" Samahani jamani tulisahau kuweka matunda.." akaomba radhi mhudumu yule kisha
akaweka sahani ya matunda katika meza na kuondoka.Hakuna aliyetaka kukiongelea tena kitendo kile kilichokuwa kimetokea muda mfupi uliopita ambacho kilinekananwazi kwamba kilikuwa na hisia kubwa ndani yake.Wakaendelea na kupata chakula kimya kimya.
" Sielewi ni kwa nini hali ile ilinitokea..Hapana !
natakiwa niende taratibu vinginevyo ninaweza nikaharibu kila kitu.Naomi ni msichana mjanja sana na mwenye akili nyingi.Ili kumpata sitakiwi kwenda haraka.Ameumwa na nyoka muda mfupi uliopita na hivyo yuko makini sana na hataki tena kufanya kosa lingine ...." akawaza Genes huku akimtazama Naomi kwa kuibia.
" Kuna hali ambayo ilimtokea Naomi wakati nimemshika mkono.Alistuka sana na akashindwa aseme nini.Kwa jinsi alivyoniangalia machoni nina hakika hakuwa amechukizwa na kitendo kile.Sielewi ni kwa nini nilisisimka sana mara baada ya kuushika mkono wa Naomi.Kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kumjua Naomi na kumpenda zaidi.Ni msichana ambaye anavutia na mwenye kila sifa ya mwanamke mzuri.Laiti angefahamu jinsi ninavyosikia furaha moyoni kwa kuwa naye usiku huu...." akawaza Genes akachukua glasi yake ya maji akanywa na kuendelea kula kimya kimya.
Naomi alikuwa akila taratibu huku akimtazama Genes kwa kuibia ibia.Alitaka kumfahamu vizuri kijana huyu ambaye moyo wake ulimwambia kwamba ndiye anayemfaa katika maisha yake.
" Nilisisimka sana Genes aliponishika mkono.Nilihisi kama vile nimemwagiwa maji ya baridi.Nilitamani aendelee kunishika mkono wangu kwani nilijisikia raha ya ajabu sana.Sidhani kama moyo wangu
unanidanganya kwamba Genes ndiye mtu sahihi kwangu.Nimetokea kumpenda sana na ninaamini kwamba ndiye kijana mwenye sifa za mwanaume ninayemuhitaji katika maisha yangu."Akawaza Naomi akiendelea kula huku akiendelea kumchunguza Genes kiujanja bila ya Genes kugunda kwamba anachunguzwa.
" Nakumbuka yule mwanamuziki anayeitwa mwanafalsafa aliimba mistari fulani katika wimbo wake
wa Yalaiti akisema
akili haiuwezi moyo nao una ubongo pia, hauwezi ukafata kila itakachouambia
." Kwa mimi akili yangu na moyo wangu vyote kwa pamoja
vinaniambia kwamba Genes ndiye mwanaume wa maisha yangu.Kwa Genes moyo wangu umekubali kuongozwa na akili yangu na kukubali kwamba Genes ananifaa.Pamoja na moyo kumkubali kwa asilimia mia moja lakini bado ninahitaji kumfahamu zaidi tabia zake za ndani na nje." akawaza Naomi na kujikuta akiacha kula na kumtazama Genes kwa makini.Genes akainua uso wake na kukutana na sura ya Naomi akimuangalia.
" naomi unawaza nini? akauliza Genes
" Siwazi kitu Genes.Nimekifurahia chakula.You've made my night kwa kunileta mahala hapa" akasema Naomi na kumfanya Genes atabasamu.
" Naomi furaha yako ni furaha yangu .Kama umeridhika na kupafurahia mahala hapa hata mimi nimefurahi pia." akasema Genes
" Genes nimepafurahia sana mahala hapa.Kila kitu kilich.............."
mara simu yake ikaita.
" Excuse me Genes ...akasema Naomi kisha akaitoa simu yake na kuizima.
" Samahani nilisahau kuizima simu" akasema Naomi
" Usijali Naomi..hakuna kilichoharibika" akajibu Genes
" Hakuna kilichoharibika lakini si jambo zuri kutoizima simu hasa kwa muda kama huu ambao umetoka na rafiki yako kwa matembezi au chakula cha usiku.Unajua ghasia za simu.Unaweza ukapokea simu ukaambiwa jambo ambalo likaifanya furaha yako yote kutoweka" Naomi akasema na wote wakacheka.
Walipomaliza kula wahudumu wakafika na kutoa vyombo .Genes na Naomi wakaendelea kupata vinywaji.
" Genes nashukuru sana kwa chakula hiki kitamu.Nashukuru nimekaa na wewe hapa na kujikuta nikiyasahu matatizo yangu yote.Kama nisingekuwa hapa na wewe mida hii ningekuwa nimejifungia mwenyewe chumbani kwangu nikiwa na mawazo mengi sana lakini kwa kunileta hapa umenisaida kuniondolea mawazo mengi yanayokisumbua kichwa changu." akasema Naomi
"Usjali Naomi,nafahahamu hali uliyonayo kwa sasa .Kuhama kutoka katika mfumo mmoja wa maisha kwenda mwingine si jambo rahisi na huwaumiza watu wengi.kama rafiki yako ninafahamu ni hali gani uliyonayo kwa sasa kwa hiyo ni wajibu wangu kuhakikisha kwamba ninakusaidia kwa kila niwezavyo..niasimama pamoja nawe hadi pale utakapokuwa na furaha kamili ."akasema genes
" Genes unafanya kazi gani? Naomi akauliza
" Mimi ni mtaalamu wa Kompyuta..nimeajiriwa katika kampuni moja inayouza vifaa vya elektroniki."
" Usinielewe vibaya Genes lakini unajua ni
kwa nini nimekuuliza hivyo? akasema Naomi huku akitabasamu
" Kwa nini umeuliza hivyo Naomi?
" Genes nafikiri ungebadilisha kazi"
" Nibadilishe kazi? akauliza Genes huku akicheka kidogo
" Ndiyo ninakushauri ubadilishe kazi" akasema Naomi
" Unanishauri nifanye kazi gani Naomi? Pengine unaweza ukanishawshi nikajikuta kweli ninafanya maamuzi hapa hapa na kubadili kazi"
" Genes ninakushauri ukafanye kazi ya unasihi.."
" hahahaa Unasihi? akasema
Genes akishangaa kidogo
" Ndiyo genes.Kazi ile ingekufaa sana kwa sababu una uwezo wa kumshauri mtu akakusikia na kukuelewa.Una uwezo wa kumfanya mtu aliye kata tamaa ya maisha akapata tumaini tena na kurejea katika maisha yake ya kawaida" akasema Naomi huku sura yake ikionyesha kwamba hakuwa akitania.
" Naomi sina hakika kama kazi hiyo inaweza ikanifaa.Sijawahi hata mara moja kufikiria au hata kuota kwamba ninaweza kuwa mnasihi.Ninaipenda kazi ya kompyuta its an interesting job and I love it..Kila nikilala ninawaza kompyuta ,nikiamka ninawaza kompyuta.maisha yangu yote yametawaliwa na kompyuta." akasema Genes
" Genes nina uhakika mkubwa kwamba unaweza kabisa ukaifanya kazi hiyo ninayokushauri uifanye.Naomba nikwambie kitu ambacho imekuwa ni siri yangu ili uamini kwamba ninayosema ni mambo ya kweli.Baada ya kuachana na yule jamaa yangu nilikuwa katika wakati mgumu sana.Nilikuwa nikijiuliza nitaanzaje maisha yangu mapya.Nilikuwa na mawazo mengi sana na kutokana na mambo aliyonifanyia yule jamaa niliwaogopa mno wanaume .Nilihisi heshima yangu mepormoka kwa kiasi kikubwa sana na sikujua nitairejesha vipi.Nilitamani hata kuhama na kwenda kuishi mbali ambako hakuna mtu yeyote anayenifahamu.Kuna wakati nilijichukia hata mimi mwenyewe na kujiona ni mtu mjinga sana kwa kuamua kumpa mwili wangu kijana muhuni kama yule .Nilikuwa nikitembea lakini hakuna mtu yeyote aliyekuwa akielewa nini ninakiwaza.Ninamshukuru MUngu kwa sababu aliyaona matatizo yangu na akakutuma kwangu na ukanipa maneno machache ya busara ambayo yalinifanya nisipate usingizi usiku ule
nikitafakari.Asubuhi nilipoamka nilikuwa mtu mpya.Sikuwa tena yule Naomi ambaye alikuwa akitembea na
mzigo wa mawazo.Niliweza haya yote kwa sababu yako.Kama umeweza kunisaidia mimi na kunifanya nirejeshe tumaini katika maisha yangu
,basi unaweza ukaifanya kazi hii tena kwa ufanisi mkubwa na ukawasaidia watu wengi wenye matatizo,wenye misongo ya mawazo na waliokata tamaa." akasema Naomi na kumfanya Genes atabasamu na kusema
" Naomi nashukuru kwa ushuhuda huo..sasa ninaamini kwamba ninaweza kuifanyakazi hii ya unasihi.Sikujua kama maneno yale machacvhe niliyokuwa nikikueleza kukutia moyo yalikurejeshea tena tumaini na kukufanya uyaanze upya maisha yako." akasema Genes
" Genes unaweza ukaifanya kazi hii hata kama hujaisomea.Nakushauri ufungue ofisi na utatengeneza pesa nyingi" akasema Naomi na kwa sauti ndogo na ya taratibu Genes akasema
" Nashukuru sana kwa ushauri wako mzuri Naomi lakini kumsaidia mtu si lazima akulipe.Kama ningekuwa na muda wa kutosha ningeweza kuifanya kazi hii bila hata kuhitaji malipo ya mtu .Sioni kama ni busara kutumia matatizo ya mtu kutengeneza pesa.Nitaangalia kama nikipata muda kwa siku za usoni ninaweza kufungua ofisi na kutoa bure msaada wa ushauri"
Naomi akamuangalia Genes usoni kwa sekunde kadhaa na kusema
" Genes una
roho nzuri sana.Sura yako inaendana kabisa na moyo wako ulivyo.Una moyo wa huruma ,moyo wa kusaida ,moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine.Mwanamke atakayebahatika kuolewa na wewe atakuwa ni mwenye furaha daima" akasema Naomi na kumfanya Genes atabasamu
" Nashukuru Naomi lakini muonekano wa nje usikudanganye na kukufanya ufikiri kwamba hata ndani ya moyo mtu huyo ni safi.Wapo wanaume wengi ambao wana sura nzuri kwa nje lakini kwa ndani ni wachafu na wanatabia zinazokinaisha"
" Genes wewe hauko hivyo..nina uhakika na ninachokisema kwamba wewe ni kijana wa tofauti sana na vijana wengi..Maisha yako,tabia zako na kila kitu chako vinaonyesha ni jinsi gani ulivyo mtu mwema na mwenye roho nzuri.Halafu Genes kuna kitu ninaomba nikuulize ..samahani lakini" akasema naomi .
" Uliza Naomi usiogope "
" Genes toka nimehamia katika ile nyumba nikakufahamu hata mara moja sijawahi kumuona mwanamke yeyote yule amekuja pale kwako..Wifi yangu unamficha wapi? Au hutaki tumfahamu? akauliza Naomi uso wake ukiwa na tabasamu
Genes akacheka kicheko kikubwa kwa swali lile la Naomi.Akachukua kitambaa na kujifuta machozi yaliyomtoka kwa kucheka sana halafu akasema
" Naomi ni kweli unavyosema .Si wewe peke yako unayeniuliza swali kama hili.Nimekuwa nikiulizwa mara nyingi swali kama hili na watu wengi wakiwemo hata ndugu zangu wakitaka kufahamu kwamba ni lini nitawatangazia habari njema kwamba nina mchumba.Naomi kusema ukweli ni kwamba nimeamua tu kuishi mwenyewe na si vingnevyo"
" Kwa nini uishi mwenyewe Genes.Kijana mzuri kama wewe,una sura nzuri,roho nzuri,una kila aina ya sifa zinazomvutia kila mwanamke na kumfanya akutamani kwa nini uamue kuishi mwenyewe?
" Naomi nilifanya maamuzi haya baada ya kugundua kwamba sina bahati katika mapenzi.Nimewahi kuwa katika mahusiano zaidi ya mara nne lakini mara zote hizo hakuna raha wala furaha yoyote ile niliyoipta zaidi ya karaha na kuishia kuumiza moyo wangu.Sikutaka tena kuendelea kuumiza moyo wangu kwa hiyo nikaamua kuishi maisha ya peke yangu."
" Pole sana Genes.Mapenzi ndivyo yalivyo.Mapenzi ni kama bahati nasibu kuna kupata na kukosa"
" Kama ni bahati nasibu basi mimi nilikosa.Mara zote niliangukia katika mikono ya wasichana ambao walichokitaka toka kwangu ni fedha na si mapenzi ya kweli hivyo nikaishia kuumia moyo .Baada ya kuumia mara nne nikagundua kwamba sina bahati katika mapenzi na suluhisho hapa ni mimi kujiweka mbali kabisa na masuala hayo ya kupenda."
" Ouh Genes pole sana.
Lakini unavyofanya unaona ni sahihi? unautendea haki moyo wako? akauliza Naomi.Genes akanyamaza
akafikiri kidogo na kusema
" Sina hakika kama maamuzi haya niliyoyafanya ni sahihi lakini kitu kimoja ninachokifahamu ni kwamba ninaishi kwa furaha baada ya maamuzi hayo.Siumizwi tena nammapenzi na ndiyo maana ninaweza kumpa mtu aliyeumizwa na mapezni ushauri wenye kufaa kwa sababu ninayafahamu na nimeyapitia mateso hayo...Lakini life is full of wonders.Who knows.. may be someday I'll meet an angel who can change my mind and make me love again" akasema Genes na kumfanya Naomi atabasamu.
" Natamani malaika huyo ningekuwa mimi.Kila dakika ninayokuwa karibu na Genes najikuta nikimpenda zaidi.Hao wasichana waliomuumiza moyo wake waliipoteza bahati kubwa sana.Nitafanya kila niwezalo hadi Genes anipende.Anastahili mtu ambaye atampenda kwa dhati na mtu huyo ni mimi.Ni kweli ninampenda sana Genes " akawaza Naomi halafu akakumbuka jambo.
" Genes kuna jambo ninataka kukuomba" akasema Naomi huku akivichezea vidole vyake
" Omba chochote Naomi niko tayari kukupatia.Hata ukitaka kichwa changu niko tayari kukikata sasa hivi na kukupa" akasema Genes na wote wakaangua kicheko.
" Genes Ijumaa ijayo kuna sherehe ya kumuaga bosi wetu wa zamani na kumkaribisha mpya kwa hiyo ninakuomba kama hutajali twende wote unisindikize katika sherehe hiyo.Sherehe zote zinazofanyika pale kazini kwetu ni mimi pekee ambaye huwa nnakuwa mwenyewe.Sikuwa tayari kuongozana na yule muhuni katika sherehe zilizojaa watu wa heshima" akasema Naomi kwa sauti yenye uoga ndani yake .Genes akatabasamu na kusema
" Sintajali Naomi na nitakusindikiza katika hiyo sherehe.Si katika sherehe tu hata sehemu yoyote ile ambayo ungependa nikusindikize kwako sintakuwa na neno hapana.Siku yoyote na muda wowote niombe chochote nitakuwa tayari kukufanyia.Naomi you deserve happiness kwa hiyo chochote ambacho kinakupa furaha niko tayari kukupa kama rafiki yako" Akasema genes
" Genes nashukuru sana.Namshukuru Mungu kwa kunikutanisha na wewe kwa sababau kuwa nawe karibu kunayafanya maisha yangu yawe rahisi sana kwani nina furaha kubwa moyoni."
Maongezi yaliyojaa vicheko na utani wa hapa na pale yakaendelea.Naomi alifurahi kupita kiasi.Hakuwahi kuipata furaha ya namna hii hapo kabla.Alitamani kila siku iwe ni kama usiku huu yaani awe karibu na Genes.Saa tatu za usiku wakarejea nyumbani na kuagana
kila mmoja akaelekea chumbani kwake.
Mpaka saa sita za usiku bado Genes hakuwa ameupata usingizi.Alikuwa akikumbuka usiku huu wa kihistoria kwake.Ni usiku huu ambao aliweza kumsoma vizuri Naomi a kugundua kwamba pamoja na uzuri alionao lakini pia ni mwanamke mwenye akili nyingi na uelewa mpana wa mambo.Alizidi kumpenda Naomi zaidi baada usiku ule.Picha ya Naomi akitabasamu ikamjia mara kwa mara nakumfanya atabasamu .Wakati bado akimuwaza Naomi mara ujumbe wa mfupi wa maandishi ukaingia katika simu yake.Ulitoka kwa Naomi
" Genes ninashindwa kupata usingizi kutokana na furaha niliyo nayo leo .Genes naomba nikushukuru tena kwa usiku wa leo..You real made my night.Thank you and good night" Genes akatabasamu na kurudia kuusoma ujumbe ule tena na tena kisha akarejesha majibu
" Hata mimi nashukuru sana Naomi kwani nimefurahi mno na kilichonifurahisha zaidi ni kukuona ukiwa na furaha na amani ya moyo.Nafurahi kukuona ukitabasamu na kucheka tena.Naomi I'll always be here anytime you need a friend...Sleep tight. Akaubusu ujumbe ule kisha akautuma.
MPENZI MSOMAJI UKARIBU KATI YA GENES NA NAOMI UNAONGEZEKA NA WANAZIDI KUTAMANIANA KADIRI SIKU ZINAVYOKWENDA.NINI HATIMA YAO? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII KILA SIKU
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment