MASIMULIZI
Saturday, April 5, 2014
SERENA SEHEMU YA 5
RIWAYA : SERENA
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Ulitakiwa kusimama Imara Serena.Hukutakiwa kuonyesha udhaifu.This is your own life my sister,no one should……….”
“save your breath Isabella.Wewe ndio chanzo cha haya yote.Lakini anyway imesaidia kujua nini kilichokuwa nyuma ya pazia.Nilikubali kiurahisi kwa sababu sikutaka Jason apate shida yoyote.Iwapo ningekataa ombi la baba basi Jason angekuwa katika matatizo makubwa .
I know our father very well.Kwa hatua aliyofikia ilikuwa ngumu kukataa.Nina imani dunia nzima itanishangaa kwa uamuzi wangu lakini I have to protect Jason even if it costs my life.” Akatulia na kufuta machozi kisha akainua kichwa na kusema
“ I’ll do what he wants but Jason will be the one I love and someday he’ll be mine.I wont stop loving Jason not for one second.For now let me do what he wants but.I hate him so much”
“ Sister kwa nini usimwambie tu kuwa umebadili uamuzi ?” Isabela akasema
“No Isabella siwezi kwa sasa.Nimekwambia I don’t want Jason to get hurt.Nikikataa matakwa yake ni lazima Jason apate matatizo.Jason hana kosa and above all he doesn’t know that I love him sasa kwa nini apate matatizo?Let this be…He exchanged me for money…just money.!!!!.Serena akasema kwa hasira huku akilia.
ENDELEA…………………………………………
Ni asubuhi ya kuamkia siku ya mahafali ya kidato cha sita siku iliyokuwa na kila aina ya pilika pilika na heka heka.Maeneo yote ya shule yalipambwa yakapendeza mno.Kila mwanafunzi alikuwa na uso uliojaa tabasamu .Kwa ujumla ilikuwa ni siku ya furaha kwa kila mmoja.
Toka Jason afanikiwe kuonana na Serena kwa mara ya kwanza ulikwisha pita mwaka mmoja na nusu sasa.Toka walipoonana kwa mara ya kwanza usiku ule hawakuwahi kuoanana
tena kwai Serena alipotea ghafla.Alipata taarifa
toka kwa Ray kwamba Serena alihamishiwa nchini marekani kwa masomo.Kwa Jason hii ilikuwa ni habari mbaya kwa sababu tangu alipomuona Serena kwa mara ya kwanza kuna kitu alihisi kinaisumbua nafsi yake.Tayari alikwisha zama penzini kwa binti huyu mwenye uzuri usioelezeka .Hii ilikuwa ni siri yake ya moyoni ambayo hakuweza kumweleza mtu yeyote yule.
“Hey ! Jason naona uko mbali sana kimawazo leo ,unawaza nini?.This is our day brother just be happy and smile.”Ray akamstua Jason toka katika lindi la mawazo.Jason hakujibu kitu akatabasamu kisha akaendelea kujiandaa .Baada ya kujiandaa wakatoka na kuelekea mahala ambako wahitimu wote walikutana kabla ya kuelekea katika sehemu yatakapofanyikia mahafali.
Wakati wahitimu
wakijiandaa kwa sherehe gari aina ya Range rover evogue yenye rangi nyeusi
likiongozana na gari nyingine kama saba hivi ziliwasili katika eneo la shule na moja kwa moja kuelekea katika ofisi ya mkuu wa shule.Mlango wa Range rover ile
ukafunguliwa na binti mmoja mrembo mwenye umbo dogo,akashuka taratibu huku akitabasamu.Huyu ni mgeni rasmi wa shughuli za leo ambaye ni mbunge mwenye umri mdogo kabisa kuwahi kutokea katika historia ya bunge na yuko bungeni kwa uwakilishi wa Vijana.Huyu ndiye mheshimiwa Stella Kamutere ambaye pamoja na udogo wake wa umri lakini ameweza kuonekana kuwa ni mmoja kati ya wabunge machachari sana.Toka ameingia bungeni amekuwa ni msemaji mkubwa wa vijana na amekuwa akiwasemea kwa nguvu zote bila kuogopa
. Mkuu wa shule alimpokea mgeni rasmi pamoja na ujumbe wake na kuwaongoza katika ofisi yake ambako walipewa maelekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na kusaini katika kitabu cha wageni muhimu.Tayari wanafunzi walikwisha chukua sehemu zao na aliyekuwa akisubiriwa ni mgeni rasmi ili sherehe zianze.
Hatimaye muda ukafika,mgeni rasmi akafika na sherehe kuanza .Ni sherehe zilizofana mno.Kulikuwa na kila aina ya burudani.Nyimbo ziliimbwa,risala zikasomwa,maonyesho mbali mbali yakafanyika ili mradi ikawa ni burudani bila kukoma.Hatimaye ukafika wakati wa kupokea zawadi.Ni Jason ndiye aliyewaongoza wanafunzi wengine kwa kupata zawadi tatu.Zawadi ya taaluma,nidhamu na usafi zote alichukua yeye.Ray alipata zawadi ya mchezaji bora.
Saa tisa alasiri shughuli zilimalizika na kilichofuata ikawa ni chakula.Wanafunzi wote wakaelekea katika bwalo la chakula ili kupata chakula cha mchana pamoja na wageni waalikwa.Wakati wakielekea katika ukumbi wa chakula mgeni rasmi Mheshimiwa Stella Kamutere akamwita mkuu wa shule pembeni na kuongea naye jambo.
“Mkuu, sherehe zimefana sana,hongera kwa maandalizi mazuri”
“ahsante sana mheshimiwa,tunashukuru kusikia hivyo toka kwako” akajibu mkuu wa shule
Mheshimiwa Stella akatabasamu kisha akaendelea
“Mkuu kuna yule kijana ambaye amechukua zawadi tatu peke yake anaonekana ni kijana mwenye akili sana”
“ndiyo mheshimwa.Kijana yule
anaitwa Jason.Ni kijana safi na mfano wa kuigwa hapa shuleni.Ni kijana mwenye akili sana.Nina imani atafika mbali
katika masomo yake”
Stella akatabasamu na kusema.
“Mimi nina taasisi yangu ya kuwasaidia na kuwaendeleza vijana kama huyu ili waweze kufikia malengo yao.Nafikiri litakuwa jambo la maana sana kama nitamuunganisha katika taasisi yangu ili ndoto zake zisiweze kupotea.Vijana kama hawa ni wachache kutokea na taasisi yangu inawasaidia kwa kuwapatia ajira za muda
katika kampuni wakati wakisubiri matokeo yao na vile vile kuwatafutia vyuo na kuwalipia gharama za masomo ya juu .Nitafurahi iwapo utanisaidia kumpata kijana yule ili niweze kuona ninamsaidiaje”akasema mheshimiwa Stella
“Mheshimiwa nimefurahi sana kusikia hivyo.Nafikiri hata yeye mwenyewe atafurahi akizipata taarifa hizi.Nitajitahidi kabla hujaondoka ili uweze kuonana naye na kuongea naye mawili matatu”
“Nitashukuru sana mkuu” Akasema mheshimiwa Stella halafu akaungana na waalikwa wengine kuelekea meza kuu.
Jason akiwa ananawa mikono kujiandaa kwa ajili ya kupata chakula mara akatokea mwalimu wa taaluma na kumwita pembeni.
“Jason ukishamaliza kupata chakula mheshimiwa mbunge anahitaji kukuona.Nasikia kuna habari njema sana.Nadhani kuna zawadi anataka kukupa”
Jason akatoa tabasamu pana linaoambatana
na uoga kwa mbali.Yeye kuombwa kuonana na mheshimiwa mbunge lilikuwa ni jambo la kumstusha mno.
“Ok mwalimu nitajitahidi nimuone.”
Saa nzima ilitumika kwa ajili ya chakula na baada ya hapo ndipo mkuu wa shule akaenda mbele ya ukumbi na kuwaeleza wanafunzi kuwa mgeni rasmi alikuwa akitaka kuwaaga na kuondoka kwani alitakiwa katika majukumu mengine ya kiserikali.
Mheshimiwa mbunge Stella Kamutere akasimama na kuongea machache ikiwa ni kuwashukuru wanafunzi na uongozi wa shule kwa kumualika na kuahidi kuwa yale yote yaliyoombwa katika risala zilizosomwa yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.Alipomaliza akawatakia wanafunzi sherehe njema halafu mkuu wa shule akawaongoza yeye na ujumbe wake kutoka nje ya ukumbi.
Jason alikuwa nje ya ukumbi kijasho kikimtoka asijue atamuona vipi mheshimiwa mbunge.Alikata tamaa baada ya kuona wageni walioambatana na mgeni rasmi wakiingia katika magari yao tayari kwa kuondoka.
“Mkuu vipi yule kijana ulifanikiwa kuonana naye? Akakumbusha Mheshimiwa Stella akiwa tayari amekwisha funguliwa mlango wa gari na mlinzi wake
“Ndiyo mheshimiwa nilimtuma mwalimu wa taaluma amtafute.Hebu ngoja nimuangalie haraka”
Stella akatabasamu wakati mkuu wa shule akikimbia kuelekea ukumbini kumtafuta Jason.
Dakika kama tatu hivi akarejea akiwa na Jason ambaye kijasho kilikuwa kikimtoka.
“You are Jason,right? Akasema Stella huku akitabasamu ili kumuondolea Jason woga ambao ulionekana dhahiri machoni pake.
“Ndiyo mheshimiwa naitwa Jason” akajibu Jason kwa uoga
Stella huku akitabasamu akamwambia
“Come follow me” Akamvuta pembeni kidogo ya watu na bila kupoteza muda akasema
“Jason
nimefurahishwa sana na uwezo na juhudi zako katika masomo.Mimi nina taasisi yangu ya kuwasaidia vijana kama nyie ambao ndio kwanza mnahitimu kidato cha sita
ili kutimiza ndoto zenu.Sasa kwa kuwa muda wa kuongea hautoshi basi nitakupigia simu kesho kupitia kwa mkuu wa shule ili tuongee
zaidi.Lengo kuu ni kukusaidia ili uweze kutimiza malengo na matarajio yako kimaisha.Kwa leo nina kizawadi kidogo hapa kitakusaidia…..” Stella akafungua pochi yake na kutoa kitita cha noti mpya halafu akahesabu shilingi laki moja na nusu na kumkabidhi Jason.
“Hizi zitakusaidia katika matumizi madogo madogo kwa muda uliobaki hapa shuleni” akasema Stella halafu akampa Jason mkono kisha akaelekea katika gari lake akaingia na gari likaondoka .Jason alibaki amesimama pale akiliangalia gari likiondoka asiamini kilichotokea hadi mkuu wa shule alipomstua.
"Jason hongera sana,mheshimiwa mbunge ameguswa
na uwezo na uhodari wako na hivyo ameahidi kukusaidia”
Maongezi kati ya Jason na mkuu wa shule yalichukua zaidi ya saa moja.Jason alikuwa amefurahi kupita kiasi.Akatoa shilingi elfu hamsini na kumpatia mkuu wa shule ambaye alifurahi mno.
*
*
*
*
Saa nne asubuhi siku iliyofuata Jason akaitwa ofisini kwa mkuu wa shule.Kulikuwa na simu yake kutoka kwa mheshimiwa Stella .Alipoingia ofisini alikutana na sura yenye tabasamu kubwa ya mkuu wa shule ambaye alimkaribisha katika kiti aketi kisha akapiga namba kadhaa katika simu ya mezani kwake.
“Haloo mheshimiwa Jason tayari niko naye hapa” akasema mkuu wa shule halafu akaurudisha mkono wa simu mahala pake na kumtazama Jason.
“Mheshimiwa amesema atapiga baada ya dakika tano.Mimi natoka kidogo akipiga ongea naye . Jason tafadhali kijana wangu nafasi hii usije ukaiachia.ni moja kati ya nafasi adimu mno kutokea.”
“Usijali mwalimu hata mimi nafahamu nini ninachokitafuta katika maisha yangu.” Akajibu Jason huku akitabasamu.
Mkuu wa shule akatoka na kumwacha Jason peke yake mle ofisini.Baada ya kama dakika sita hivi simu ikaita.Akainua mkono wa simu na kuiweka sikioni.
“Hallow” Akaita
“hallow naongea na nani? Sauti ya upande wa pili ikauliza.Ilikuwa ni sauti nzuri na nyororo ambayo moja kwa Moja Jason akaitambua ni ya Mheshimiwa mbunge Stella kwa sababu alikwisha isikia jana yake
“Unaongea na Jason hapa”
“Ouh Jason habari ya toka jana”
“:nzuri tu Mheshimiwa”
“ Umejuaje kama ni mimi ndiye ninaongea? Akauliza Stella huku akicheka
“ Ninaikumbuka sauti yako toka jana na kamwe haiwezi kunipotea tena” akajibu Jason
“Nafurahi kusikia hivyo Jason .Jana hatukupata muda mzuri wa kuongea.Ni kwamba mimi nina taasisi yangu ambayo inawachukua vijana kumi kila mwaka wenye kuonyesha juhudi na uwezo mkubwa darasani na kuwaendeleza katika kutimiza ndoto zao.Huwa tunachukua vijana wa kidato cha sita ambao ndio kwanza wamemaliza shule na kuwapa ajira za muda katika kampuni zetu kwa kipindi wanachosubiri matokeo yao na baada ya hapo tunawatafutia nafasi za masomo katika vyuo vikuu vya nje ya nchi.Jana niliguswa sana na sifa ulizopewa juu ya uwezo na juhudi zako Darasani . Jason ninafurahi
kusema kuwa nimekuchagua uwe ni mmoja kati ya wanafunzi kumi ambao wataingia katika program yetu kwa mwaka huu.Kwa kuwa Jumatatu mnaanza mitihani nisingependa kukuchanganya sana ila ningeomba tu kama utakuwa tayari basi tuwasiliane baada ya kumaliza mitihani ili nikupe malekezo nini cha kufanya.Mkuu wa shule atakupa namba zangu za simu utanipigia mara utakapomaliza mitihani yako ya mwisho.Hivyo fikiria kwa kina ili utakapomaliza mitihani yako uwe na jibu lenye uhakika.Sawa Jason……..”
“Sawa nimekuelewa mheshimiwa.Nashukuru sana kwa kuniona na kuamua kunisaidia ili niweze kutimiza malengo yangu maishani.Mimi kwa upande wangu sina kipingamizi chochote kwani suala hili linahusu mustakabali mzima wa maisha yangu ya baadae…Nashukuru sana.Mungu akubariki mheshimiwa mbunge….” Akasema Jason akiwa na furaha isiyoelezeka
“Nafurahi kusikia hivyo Jason…Nakutakia kila la kheri katika mitihani yako,Mungu akutangulie ufanye vizuri na ufaulu.Usisahau kunipigia mtakapokuwa mmemaliza.”.
“Sintasahau mheshimiwa.”
“Ok Jason kwa heri”
“Ahsante mheshimiwa .Kwa heri”
Simu ikakatwa lakini bado Jason aliendelea kuushikila mkono wa simu.Ni mwalimu wa fizikia ndiye aliyemstua Jason baada ya kumkuta katika ofisi ile ya mkuu wa shule akiwa ameushikilia mkono wa simu huku akitabasamu.
*
*
*
*
Wiki mbili ngumu zilipita kama mvua.Ni wiki ngumu kwa vijana wa kidato cha sita waliokuwa wakifanya mitihani yao ya mwisho.Hakuna aliyeweza kuelezea furaha aliyokuwa nayo Jason baada ya kumaliza mitihani yake.Furaha yake ilijumuisha mambo mengi.Kwanza mtihani ulikuwa mzuri na alikuwa na uhakika wa kufanya vizuri sana,vile vile alifurahi zaidi kwa kuwa na uhakika wa kupata kazi ya kufanya wakati anasubiri matokeo yake na zaidi
kuunganishwa katika taasisi ya mbunge Stella Kamutere ilimpa furaha sana ya yeye kutimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuwa daktari..
Baada tu ya kumaliza mitihani Jason hakuwa na muda wa kupoteza akanyoosha moja kwa moja hadi katika ofisi ya mkuu wa shule.Moja kwa moja akaeleza kilichompeleka.Mkuu wa shule alitabasamu akainua simu na kubofya namba kadhaa.
”Haloo” Alisema mkuu wa shule akaoongea kidogo kisha akampa Jason mkono wa simu
“Ongea na mheshimiwa mbunge”
“Hallow mheshimiwa mbunge” Jason akasema
“Haloo Jason.Pole sana na mitihani” Akasema Stella
“Ahsante mheshimiwa nimekwisha poa.”
“Vipi mitihani ilikuwaje? Akauliza Stella
Huku akitabasamu Jason akasema
“Mitihani ilikuwa safi, nina imani Mungu atajaalia nitafanya vizuri”
“Nafurahi kusikia hivyo Jason hata mimi nakuombea iwe hivyo.Jason kwa ufupi ni
kwamba
niko katika mipango ya safari.Nina safari ya kuelekea Malasia usiku wa leo.Sintakuwepo kwa muda wa kama mwezi mmoja hivi.Unachotakiwa kufanya ni kwenda Dar es salaam.Tarehe 22 saa mbili asubuhi unatakiwa ufike katika ofisi za Kamutere group of companies zilizopo pale Waridi plaza Masaki.Ukifika pale muulize dada moja anaitwa Digna Constantine Ubwaya.Tayari ana maelezo yako na maelekezo yote nimemwachia yeye.Mimi tutaonana nitakaporudi.Usihofu
muone tu huyo dada na kila kitu kitakuwa safi.”
“Ok Mheshimiwa nashukuru sana.Nitafanya kama ulivyonielekeza.Nakutakia safari njema.” Akajibu Jason na kukata simu
*
*
*
*
Ni Jumatatu asubuhi ya tarehe 22 Jason tayari alikwisha fika katika jengo hili kubwa la Waridi Plaza.Moja ya majengo mapya ,makubwa na mazuri yanayolipendezesha jiji hili la Dar es salaam.Akiwa kwa nje alionekana kutabasamu kwa jinsi jengo lilivyokuwa kubwa na zuri.Nakshi na maua ya kupendeza vyote vilipafanya mahala hapa pavutie mno.Pamoja na kwamba ni asubuhi lakini watu walikuwa katika pilika pilika nyingi za kuwahi katika ofisi zao.
“Am I going to work in this building? Its like a dream ..” Akawaza Jason huku akitabasamu.Kwake ilikuwa kama ndoto kufanya kazi katika jengo kubwa na zuri namna ile.Akionekana kama ni mmoja wa wafanyakazi katika jengo hilo akaingia moja kwa moja zilipo ofisi za Kamutere group of companies mpaka mapokezi palipokuwa na wadada watatu warembo .
“Karibu kaka” Akakaribishwa na dada mmoja aliyekuwapo pale mapokezi.
“Habari za asubuhi” Jason akawasabahi.wote wakaitika kisha Jason akauliza
“Samahani namuulizia dada mmoja anaitwa Digna Constantine Ubwaya”
“Unaitwa nani?
“Jason.,…JasonPatrick Charles”
Yule dada akafungua kompyuta yake akaangalia kisha akasema.
“Mbona jina lako haliko katika orodha
ya wageni wanaotakiwa kumuona Digna leo?
“Yawezekana nikawa sipo katika orodha lakini ana taarifa ya ujio wangu.Naomba umpigie simu mwambie nimekwishafika”Akasema Jason kwa kujiamini
Yule dada akainua simu akaongea kidogo kisha akapiga simu tena na mara akatokea kijana mmoja aliyevaa sare za ulinzi.
“Mnene mpeleke huyu kaka ofisini kwa dada Digna”
Yule mlinzi akamchukua Jason na kumuongoza kuelekea ofisini kwa Digna
Ndani ya ofisi kubwa iliyopendeza mwanamke mmoja mweupe,mwenye sura ya kutabasamu muda wote alikuwa mbele ya kompyuta yake.Huyu ndiye Digna Constantine.
“Karibu sana Jason”
“Ahsante sana” akajibu Jason na maongezi yalichukua kama nusu saa hivi kisha Digna akasema
“Jason maagizo niliyopewa na mheshimiwa mbunge ni kwamba nikupeleke katika kitengo cha promosheni na matukio kwenye kampuni yetu ya simu za mikononi ya Masai com.Wewe
utakuwa msaidizi wa meneja wa promosheni na matukio.Jason mengi yatasemwa hasa wewe kupewa nafasi hii ambayo ilikuwa inawaniwa na watu wengi.Unachotakiwa kufanya ni kukaa kimya na kuvumilia yote huku ukijifunza kazi kwa bidii.Kikubwa zaidi wewe fanya kazi kwa ushirikiano na watu wote.Natumai u kijana mchapakazi kutokana na sifa zako tulizozisikia”
“Nashukuru sana dada Digna.Changamoto huwa hazikosekani katika kila sehemu.Majungu chuki ni vitu vya kawaida sehemu za kazi.Nimekwisha jiandaa kukabiliana na hayo yote hivyo ninachoweza kukuahidi ni kwamba nitafanya kazi hii kwa moyo wangu wote na hatimaye kuiletea mafanikio kampuni.Nahitaji ushirikiano wenu.”
" Usijali Jason..tuko pamoja na muda wowote ukiwa na tatizo lolote usisite kunitafuta nitakusaidia.Kwa kukukumbusha tu Jason ni kwamba una bahati kubwa sana kuipata nafasi hii.Watu wengi walikuwa wakiililia nafasi hii lakini imekuangukia wewe.Usikubali kuipoteza bahati hii,fanya kazi kwa bidii.Dhirisha kwamba ulistahili kuwepo mahala hapo.." akasema Digna kisha
akainua simu akaongea na mtu Fulani na muda huo huo akaingia dada mmoja aliyevaa suti iliyomkaa vyema.
“Ney
huyu ni mfanyakazi mwenzetu anaitwa Jason.Ndiye msaidizi wa Kulangi.Naomba umkabidhi kwake tafadhali”
Jason akainuka akaagana na Digna kisha akaongozana na yule dada mwingine
“Dada sikusikia jina lako vizuri unaitwa nani vile? Jason akauliza wakati wakielekea katika ofisi za promosheni.
“Naitwa Neema”
“Ouh Neema.Jina zuri.nafurahi kukufahamu Neema.Natumai tutakuwa tukionana mara kwa mara”
“Usijali Jason tutakuwa pamoja”Akajibu yule dada huku akitoa tabasamu pana na kuuonyesha mwanya wake mzuri kati kati ya meno ya juu.
Jason akakabidhiwa kwa Mr Kulangi ambaye ndiye meneja wa promosheni na matukio ,akatambulishwa kwa watu wote wa kitengo hicho na mara moja akanza kujifunza kazi.
Akiwa ofisini kwake mara simu ya mezani ikaita akaipokea
“Jason hapa”
“Jason ni mimi Stella .Nimetaarifiwa mambo yamekwenda vizuri na tayari umeshapewa ofisi.”
“Ndiyo mheshimiwa nashukuru sana.Kila kitu kimekwenda vizuri”
“Vipi unaonaje kazi?
“Kazi siwezi kusema rahisi kwa sababu ndio kwanza najifunza ili nipate uzoefu lakini nina imani nitafanya vizuri zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele”
“ good.Nafurahi kusikia hivyo Jason.Jitahidi uelewe kila kitu.Mr Kulangi yupo atakusaidia kuelewa kila kitu .Mimi bado niko safari.Kabla sijasahu kuna gari nimeamuru upewe na dereva wa kukuendesha hadi hapo utakapoweza kuendesha mwenyewe.Nimewaambia kesho wakakuandikishe katika chuo cha udereva ili uwe ukijifunza muda wa jioni.Nataka uwe na muonekano wa kimeneja Jason”akasema Stella
“ mheshimiwa nashukuru sana.Sina kuongea kinachoweza kupita neno ahsante sana kwa yote uliyonitendea”
“Usijali Jason.Kazi njema.Kama una tatizo lolote muone Digna”
Jason akashindwa kujibu ,kwa furaha aliyokuwa nayo.Hakuamini kama angeweza kufikia hatua kama hii mapema namna hii.
“ Life is full of miracles..jana nilikuwa kapuku lakini leo hii ni meneja..Huu ni muujiza kwangu “ akawaza Jason kisha akaendelea na kazi
TUKUTANE SEHEMU IJAYO
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment