Wednesday, April 2, 2014

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 2










  "Humu kwenye huu mfuko kuna nini? akasema taratibu Genes huku akiufungua mfuko ule na kukuta kuna nyama ya kuku ya kukaanga.
  "Wow ! ...Naomi... I love you so much.Nakupenda sana Naomi..Laiti ungejua ni namna gani moyo wangu unakuhitaji ungenionea huruma" Genes akasema taratibu akakibusu kigaja cha mkono wake na kukipuliza kuelekea chumba cha Naomi.


ENDELEA........................
            
 






            " Kuanzia kesho nitaanza kuweka ukaribu mkubwa.Nashukuru Mungu kwamba mwanzo nilioanza nao ni mzuri sana.Naomi ameingia kwangu kwa mara ya kwanza na kuniletea nyama ya kuku.Kwa vile yeye leo ameniletea kuku na mimi kesho itanibidi kutafuta zawadi ya kumpelekea wakati nikirudisha chombo chake.Nikiweza kumfurahsha mara mbili tatu basi tayari kutakuwa na mazoea na hapo ndipo nitakapoanza kumuomba kutoka naye kwenda kupata chakula cha usiku kama atakuwa na nafasi.Nataka kumfanyia mambo yale ambayo  hakuwa akiyapata kwa yule kijana.Naomi ni msichana mzuri na anahitaji kuwa na mwanaume ambaye atamtunza na kumfanya azidi kung'aa na kuwa mrembo zaidi,mwanaume ambaye atamthamini na kumjali ,mwanaume ambaye atampa raha zote za dunia hii na kumfanya ajione kama malkia wa dunia.Ninastahili kuwa na Naomi ka sababu nina uwezo wa kumpatia hayo yote.Nina uwezo wa kumtunza,kumjali na kumthamini.Nina uwezo wa kumpa kila aina ya raha za dunia kwa sababu ninampenda na niko tayari kufanya lolote kwa ajili yake.Moyo wangu haunidanganyi kwamba Naomi ndiye msichana pekee ambaye ananifaa.Msichana mrembo,na mwenye heshima na adabu tele.kama sifa zote anazo binti huyu kwa nini basi nimkose wakati siku zote nimekuwa nikimuomba Mungu anipe msichana mrembo kama Naomi? Nadhani Mungu ameamua kunijibu maombi yangu na kunipa macho ya kuona .Mungu ana njia zake za kukupa kitu na si mpaka amtume malaika kukuletea barua kwamba msichana anayekufaa ni Naomi." akawaza Genes na kujilaza tena kitandani akijaribu kufumba macho ili aone kama anaweza akapata usingizi.Picha ya umbo zuri la Naomi ikamjia tena kichwani.Akafumbua macho na kutabasamu kisha akavuta pumzi ndefu


            " Siamini kama yule kijana ameondoka nyumbani kwangu.Namshukuru sana Genes kama si yeye na balozi Msuya ,yule jamaa katu asingeondoka kwangu.Alikwisha goma kutoka humu.Kuna nyakati najiuliza ni kwa nini nilijiingiza katika mapenzi na yule kijana.Kweli penzi ni upofu na mimi nilipofuka macho kutokana na penzi la kijana yule na sikuona wala kusikia la mtu.Sijui alinipa nini kiasi cha kumkubalia kumpa mwili wangu auchezee.Sikujua kwamba huko mtaani watu walikuwa wakainicheka na kunishangaa msichana mrembo kama mimi kuishi na kijana mvuta bangi kama yule.Nahisi kuna kitu alinipa ili nisiweze kuona chochote na kumuacha aendelee kujifaidisha kwa kutumia mgongo wangu.Nilipoteza dira na mwelekeovmzima wa maisha yangu.Sikuwa na mawazo yoyote kuhusu kesho wala maisha yangu ya baadae.Kila pesa niliyokuwa nikiipata ilitoweka bila habari.Naujutia muda wangu nilioupoteza kwa kijana yule asiyekuwa na mbele wala nyuma.Kijana asiyekuwa na ndoto za maendeleo,kijana ambaye anawaza leo na hajui kama kuna kesho.I was so stupid..so stupid.Katika maisha yangu ninajuta sana kuamua kuishi na kijana kama yule muhuni ambaye hana hata chembe moja ya heshima kwa mtu yeyote yule..Pesa zangu alizitumia kunywea pombe ,kuvuta sigara na bangi na kuwahonga wanawake ..ouh kwa nini nilikuwa mjinga kiasi hiki? Nimekwisha aibika vya kutosha na sijui hata heshima yangu itarejea vipi." akawaza Naomi na kwa mbali machozi ya majuto yakamtoka.Alikijutia kitendo cha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana yule aliyeachana naye.

            " Ninachomshukuru Mungu ni kwamba nilijitahidi sana kujizuia kuzaa na kichaa yule.Pamoja na yote yaliyotokea bado sijachelewa.Bado ninayo nafasi ya kuweza kuyatengeza upya maisha yangu yaliyopoteza mwelekeo.Nitaanza kwanza kwa kujijenga kiuchumi ,kutumua pesa ninayopata vizuri na kujaribu kuanzisha hata biashara yoyote ndogo ambayo inanisaidia kuongeza kipato.Nikishafanikiwa kuanzisha biashara yangu nitaweza kuchukua hata mkopo katika taasisi za fedha na nikiikuza biashara yangu na baadae nikisha kuwa na mtaji mkubwa nitatafuta kiwanja nijenge nyumba yangu hata ndogo na kuondokana na nyumba hizi za kupanga na baada ya hapo nitaanza tena kutafuta mwanaume ambaye atanifaa maishani.Siwezi sema eti kwamba sintapenda tena kama wengi wanaotendwa na wanaume zao walivyozoea kusema.Nikisema hivyo nitakuwa sijitendei haki mimi mwenyewe wala moyo wangu.Nahitaji mwanaume wa maisha yangu ambaye nitampenda na kuishi naye kwa raha furaha na amani hadi nitakapofika uzee.Nahitaji mwanaume ambaye atanipenda atanithamini na kunijali,mwanaume ambaye nitampenda na kumuamini,mwanaume ambaye nitajenga naye familia yenye furaha na upendo mkubwa.Kumpata mwanaume wa sifa hizi sihitaji kukurupuka.Ninahitaji muda wa kutosha na zaidi sana kumshirikisha Mungu ili aweze kuniletea mwanaume ambaye atanifaa maishani mwangu.Nahitaji kumpata mwanaume aliye na tabia kama za Genes.Kaka yule ananivutia sana kwa tabia zake.Ni mpole,ana heshima,anapenda watu,na anapendwa na kila mtu.Anajipenda na ni mtu mwenye kujituma katika kujitafutia maendeleo.Nitafurahi kama ningepata kijana kama yule" akawaza naomi na mara sura ya Genes ikamjia kichwani akajikuta akitabasamu.




























0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi