Wednesday, April 2, 2014

" BEFORE I DIE" SEHEMU YA 2






.Mabibi na mabwana sina cha kuongezea zaidi ya kuwashukuru sana kwa kuja kwenu .Naomba tuendelee na sherehe hizi kwa amani na utulivu.Ahsanteni sana”
            Makofi na vigele gele vikasikika katika kila kona ya ukumbi.Watu waimshangilia Innocent kwa maneno machache aliyoyatoa.Sherehe zikaendelea hadi usiku mwingi halafu watu wakatawanyika na kurudi majumbani kwao.

ENDELEA..............................................................................................



            Siku moja alikuja mama mmoja ambaye alikuwa akitafuta mtumishi wa ndani.Mama akaniuza kwa shilingi laki tano.Japokuwa nilitoa machozi kwa kufanywa kama bidhaa lakini kwa upande mwingine nilishukuru Mungu kwani niliamini ule ungekuwa ni mwanzo wangu wa kuondokana na dhiki ile kubwa ya nyumbani kwetu.Nililetwa Dar es salaam na kuanza kufanya kazi za ndani kwa mama yule aliyenitoa Iringa.Baada ya wiki mbili mama yule akaniuza tena kwa mama mmoja wa kihindi.Nikawa nafanya kazi pale.Nilipata manyayaso makubwa sana katika familia ile.Baba mwenye ile nyumba alikuwa akija na kunilazimisha kufanya naye mapenzi kila siku kwa kigezo kwamba nikikataa atanifukuza kazi.Sikuwa na mwenyeji wala ndugu yeyote hapa dar hivyo ikanilazimu kukubali kufanya naye uchafu ule.Nilipoona sintaweza kuvumilia tena nikatoroka na kuingia mtaani.Sikuwa na mahala pa kula wala kulala.Nikiwa njiani usiku wa saa tatu nikakoswa kugongwa na gari.Mzee yule aliyetaka kunigonga alinitazama akagundua kuwa nilikuwa na matatizo.Baada ya kunihoji nikamuelezea  historia nzima ya maisha yangu,akanionea huruma akanichukua hadi nyumbani kwake.Mzee huyu ni baba yako.Nilianza kuishi pale kwenu na kusaidia kazi za nyumbani.Siku moja mmoja kati ya walinzi wa baba alinibaka,nikamsemea kwa baba akamfukuza kazi.Nililia sana baada ya kusikia kuwa mlinzi yule alikuwa ameathirika na virusi vya ukimwi.Baadae nilianza kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara.Nilikuwa naumwa,nakohoa na kutapika Mama akasema nilikuwa nimeambukizwa ukimwi tayari.Toka wakati huo nimekata tama na maisha yangu ninasubiri siku ya kufa kwangu……………..” Grace akashindwa kuendelea akaanza kulia.




1 comment:

  1. nimejikuta natokwa na machozi cjui kwa nn binadamu wengine tuko hivyo kuwanyanyapaa binadamu wenzetu

    ReplyDelete

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi