MASIMULIZI
Monday, April 14, 2014
TEN CHAPTERS SEHEMU YA 12
RIWAYA : TEN CHAPTERS
SEHEMU YA 12
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Saa nne za asubuhi Naomi akarejea chumbani kwake .Kabla hajaingia chumbani kwake alichunguza kwanza kama Genes alikuwepo pale na alipohakikihsa kwamba hakuwepo ndipo alipoingia ndani.Macho yalikuwa yamemvimba
kutokana na kulia .Alikitazama chumba chake halafu akachukua sanduku
na kuanza kupakia nguo na baadhi ya vitu
vyake vya muhimu.Alipomaliza akachukua kalamu na karatasi na
kuandika barua . Mara kadhaa alisimama kuandika barua ile na kujifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka.Alipomaliza kuandika barua ile akaisoma huku
machozi yakimtoka.
“ Utanisamehe Genes lakini lazima nifanye hivi kwa faida yetu sote.Ninakupenda sana na siku zote nitaendelea kukupenda.Wewe ni ,mwanaume wa pekee
kabisa kuwahi kutokea maishani mwangu
.” akasema Naomi huku akifuta machozi akatoka chumbani kwake na kwenda kuipenyeza
barua ile chini ya mlango wa chumba cha Genes,akarejea chumbani kwake na kuita taksi ambayo ilifika kwa haraka akapakia sanduku lake na kuondoka zake.
“ Kwa heri genes.Hatutaonana tena katika maisha haya.Kitu kimoja tu ambacho kitabaki moyoni mwangu ni kwamba sijawahi kumpenda mwanaume kama nilivyokupenda Genes.” Akawaza Naomi wakati akiondoka pale nyumbani.
ENDELEA……………………………..
Taarifa za kutoweka kwa Naomi zilifika kazini kwao na kumstua kila mtu.Walipigiana simu kuulizana lakini hakuna aliyekuwa na tarifa zozote za mahala alipo Naomi.Genes alizidi kuishiwa nguvu na kuogopa kadiri muda ulivyozidi kusonga mbele bila ya Naomi kuonekana au hata fununu za mahala alipo.
“ Naomi uko wapi? Kwa nini unanitesa kiasi hiki? Akawaza Gene baada ya kutoka ofisini kwa Naomi.Alikuwa ameegemea mti akiwaza
“ Wapi nitampataNaomi? Nafikiri kwenda kuripoti polisi lakini kabla ya hayo ngoja kanza nikaonane na kaak yake tujadiliane nini cha kufanya” akawaza Genes halafu akaeleke a katika kituo cha taksi akakodi taksi iliyompeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwa kaka yake Naomi ambaye hakuwepo nyumbani kwa wakati huo.Mpaka muda huo hakukuwa na taaifa zozote za kumuhusu Naomi .Genes akahisi miguu yake kuishiwa nguvu akaketi sofani na kumuomba mtumishi wa ndani amletee maji ya kunywa.Wakati akiwa amekaa sofani akitafakari mara simu yake ikaita.Alikuwa ni mama James jirani yake
“ Hallow mama James” akasema Genes baada ya kupokea simu
“ Genes umeonana na Naomi? Akauliza mama James
“ Hapana mama James.Bado sijaonana naye na ninaendelea kumtafuta.Hivi sasa niko hapa kwa kaka yake na bado hajaonekana.Nimefika hadi kazini kwake lakini hajaonekana kule na hakuna yeyote anayefahamu mahala alipo.Hapa nilipo nimechanganyikiwa na sielewi nitamtafutia wapi.Nafikiria kwenda polisi kutoa taarifa lakini sina budi kwanza kuwasiliana na ndugu yake” akasema Genes
“ Genes mbona Naomi ameonekana nyumbani muda si mrefu? Akasema mama James
“Naomi?! ……Genes akastuka
“ Ndiyo.Naomi ameonekena hapa nyumbani muda si mrefu.
“ Ouh ahsante Mungu.Bado yuko hapo nyumbani? Umeongea naye?
“ Hapana Genes.Sijafanikiwa kuongea naye.Nilimuona akishuka katika taksi na kuingia ndani
“ Ahsante sana kwa taarifa mama Jams.Ninakuja hapo nyumbani sasa hivi” akasema Genes na kutoka mbio hadi katika baa ya jirani akakodisha piki piki na kuelekea nyumbani kwake
“ Ahsane Mungu kwa kumrudisha Naomi” akawaza Genes huku kijasho kiki mtoka kwa furaha aliyokuwa nayo.Akatoa simu na kumpigia kaka yake Naomi
“ hallo Genes kuna habari gani? Akauliza kaka yake Naomi baada ya kupokea simu
“ Nimepigiwa simu na mmoja wa jirani zangu anasema kwamba Naomi kaonekana.Amefika pale nyubani muda si mrefu.Ka sasa niko njiani naelekea huko”
“ Dah ! Hizi ni taarifa njema sana.Nilikuwa na wasi wasi sana na nilikuwa najiandaa kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.Naomba unitaarifu tafadhali kuhusu hali yake pindi utakapoonana naye” akasema kaka wa Naomi
“ Sintamuacha Naomi atoweke tena.Nitafanya kila nnaloweza kumtafutia msaada wa kisaikolojia ili akili yake iweze kutulia kwani nina hakika atakuwa ameathiriwa sana taarifa ile ya kwamba ni muathrika wa virusi vya ukimwi.Kuathirika kwa ukimwi si mwisho wa maisha.Kama atazingatia masharti na kanuni za maisha ya kuishi na virusi anaweza akaishi miaka mingi.Naomi anahtaj msaada na nitamsaidia kwa kila namna nitakayoweza.Bado namuhitaji katika maisha yangu.Nafasi yake bado ni kubwa mno ,ninampenda na sintaacha kumpenda.Majibu ya vipimo vile hayawezi kunitenganisha naye hata kidogo.Hata kama dunia yote itapinga mimi kuwa na Naomi siko tayari kwa hilo.Naomi ni wangu na nitashi naye hivyo hvyo hata kama ameathirika na virusi” akawaza Genes akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake
Walifika nyumbani anakoishi Genes akamlipa dereva wa piki piki na kisha akakimbilia ndani ili kuonana na Naomi.Moja kwa moja akaelekea katika mlango wa chumba cha Naomi lakini ulikuwa umefungwa na hakukuwa na dalili zozote za kuwepo mtu mle ndani.Genes akapata woga akachukua ufunguo aliokuwa nao wa chumba cha Naomi akaufungua ule mlango na kuingia ndani .Naomi hakuwepo chumbani.Vitu vilikuwa vimepanguliwa hovyo na milango ya kabati la nguo ilikuwa wazi.Kabatini hakukuwa na nguo hata moja
“ Gosh Naomi kaondoka ! ..akahamaki Genes
“ Kachukua nguo na kila kitu chake cha muhimu.Kaelekea wapi? Genes akajiuliza na kukosa jibu.Akasimama kwa sekunde kadhaa akatafakari ,mwishowe akaamua kutoka na kuelekea chumbani kwake.Mara tu alipoufungua mlango wa chuma chake macho yake yakatua juu ya bahasha nyeupe.Akainama na kuiokota.Ilikuwa imeandikwa jina lake
“ Huu ni wandiko wa Naomi” akasma Genes huku akikaa kitandani na kuanza kuifungua barua ile.Mikono ilikuwa inamtetemeka.Aliitoa karatasi iliyokuwamo ndani ya bahasha na kuanza kuisoma
Kwako Geges
Natumai usomapo barua hii tayari nitakuwa mbali na upeo wa macho yako.Genes nimechukua maamuzi haya ya kwenda mbali nawe kutokana na hali halisi iliyojitokeza na ninafikiri hii ndiyo njia pekee na muafaka kwa sasa.
Genes kwanza kabisa nakuomba sana msamaha kwa mambo kadhaa.Kwanza ni kuivuruga mipango ya maisha yako.Najua unanipenda na mimi ninakupenda pia.Penzi letu lilikuwa ni la kutiliwa mfano na kwa pamoja tulikuwa na ndoto nyingi za kutimiza maishani lakini kwa sasa zitabaki kuwa ni ndoto tu na hazitakuwa kweli.
Pili naomba unisamehe sana kwa mstuko ulioupata baada ya kugundua kwamba nimeathirika na ukimwi.Naomba nikuweke wazi kwamba mimi si muathirika wa ukimwi kama ilivyodaiwa .Nilifanya mchezo mchafu ili ionekane kwamba nimeathirika na nisiweze kuendelea na mipango yetu ya ndoa.Nisamehe sana kwa hilo Genes lakini aomba nikiri kwamba ninakupenda kwa moyo wangu wote na nilikuwa tayari hata kufunga ndoa na kuishi nawe hali nikijua kwamba nilikuwa nafanya kosa kubwa sana.Genes sina lugha nzuri ya kulielezea hili kwani ni hadithi ndefu sana lakini naomba tu uelewe kwamba mimi na wewe haikupangwa tuwe pamoja.Nina hakika yupo Yule ambaye amendaliwa kwa ajili yako na si mimi.Genes wewe ni kijana mzuri mwenye kila sifa nzuri na ninajisikia fahari kukufahamu kijana kama wewe.Nakuomba usikate tamaa kumtafuta Yule ambaye aliumbwa kwa ajili yako.Mimi naomba unisahau kwa sababu I’ll never come back in your life again
Jambo la tatu ambalo nataka unisamehe ni kwa kukudanganya kuhusu mimi.I’m not who you think I am.Everything you know about me are all lies.Jina langu halisi si Naomi bali Linah.Naomba unisamehe sana kwa kukudanganya wewe na kila mmoja hapo Arusha lakini nilifanya hivyo ili kujaribu kujisahaulisha historia ya maisha yangu ambayo ninajitahidi kuisahau bila mafanikio.Nina historia ndefu na ambayo sintaweza kukuelezea katika barua hii .Ninachotaka ufahamu tu ni kwamba kuna mambo mengi ambayo huyafahamu kuhsu mimi na moja wapo ambalo nataka kuungama kwako ni kuhusu yule kaka niliyekufahamisha kwamba ni kaka yangu wa kuzaliwa naye si kweli hata kidogo .Yule aliwahi kuwa mpenzi wangu lakini ili kuyaficha mahusiano yetu ilitulazimu kuigiza kama kaka na dada.
Genes sitaki nikuumize zaidi kwani mpaka hivi sasa utakuwa umekwisha umia vya kutosha.Narudia tena kukuomba msamaha kwa ukweli huu niliokueleza lakini pamoja na hayo yote naomba ufahamu kitu kmoja tu kwamba ninakupenda na nitaendelea kukupenda katika maisha yangu yote.You ‘ll always be here in my heart forever ,and forever,and forever.
Linah
Jasho lilikuwa linamtiririka Genes baada ya kumaliza kuisoma barua ile.Alihisi kama chumba kinazunguka.
NAOMI NI NANI? NINI HISTORIA YAKE? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZi HII KATIKA SEHEMU IJAYO….
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment