Monday, April 14, 2014

BLEEDING HEART SEHEMU YA 12



ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA 
 Machozi yakazidi kumtiririka Paula .Akainua kichwa chake akatazama katika meza yake ya vipodozi ambapo pembeni yake kulikuwa na picha moja kubwa ya mwanamke mzuri akitabasamu.Ilikuwa ni picha ya mama yake ambaye alifariki angali Paula bado mdogo sana.Akaitazama picha ile kwa uchungu akaiweka kifuani kwake   “Ouh My Mother ..why you had to marry this heartless man ?
Look what I’m going through right  now.I feel like my heart is bleeding inside for the pain I’m feeling right now….Mother why he cant let me be with the man I truly love? …Paula akaendelea kudondosha machozi.   “Ninaona aibu kuwa na baba kama huyu mwenye roho ya kikatili.Pamoja na yote aliyonifanyia,pamoja na kumdhalilisha Joe mbele yangu lakini siku zote akae akijua kwamba Joe ni mwanaume wa maisha yangu.Joe is my guardian angel.Joe is my second living part.hawezi kamwe kunitenganisha na Joe labda anitoe uhai wangu.Kwa maumivu haya ninayoyapata sasa hivi yananifanya nimpende Joe zaidi”  

   ENDELEA………………………………….      

   Joe alihisi kama anaota kuna mtu anamtikisa ili aamke .Akafumbua macho na kugundua hakuwa akiota bali ni kweli alikuwa akitingishwa ili aamke.Mama yake   alikuwa amesimama pembeni ya kitanda chake .   “ Mama..shikamoo” Joe akasema kwa sauti ya uchovu huku akiyafikicha macho yake.   “marahaba Joe habari yako.Unajisikiaje leo?  “Nahisi maumivu makali sana ya kichwa.Sikuweza kupata usingizi usiku wa leo” Joe akasema huku akijiinua na kuketi kitandani.Mama yake akamtazama usoni kwa huruma na kusema   “Joe Paula yuko sebuleni anahitaji kuonana na wewe.”  Joe akamtazama mama yake kwa sekunde kadhaa kisha akasema   “mama naomba umwambie aondoke.Siwezi kuonana naye sasa hivi”  “Kwa nini Joe?  “Mama nashindwa nitamuonaje usoni.Nimefikiria sana usiku wa leo na nimeona ni bora kama tutaachana kabisa.Nadhani hatukupangiwa kuwa pamoja”   “Joe mwanangu nafahamu ni jinsi gani unavyoumia moyoni kwa mambo yaliyotokea.Pamoja na yote yaliyotokea nakuomba tafadhali usimuache Paula.Anakupenda sana na ni mwanamke pekee anayekufaa maishani.”   “mama nafahamu kama Paula ananipenda na mimi ninampenda mno,lakini hatuwezi kuwa pamoja tena.Its already complicated.”   “Joe sisi wazazi wako hatuwezi kukupangia mtu wa kuwa naye maishani.Sisi tulimpenda Paula na tumeona ni binti anayekufaa.Kama wewe mwenyewe kwa hiari yako umeona kwamba kuachana ni suluhisho la matatizo yenu.hatuwezi kukupinga .Ila nakuomba kitu kimoja”  “Kitu gani hicho mama”  “naomba uongee na mwenzako na kama ni kuachana umweleze wazi wazi “   Joe akafikiri kidogo kisha akasema   “Ok nitaonana naye.Mwambie aje chumbani kwangu”     Dakika mbili baadae mlango wa chumba chake ukafunguliwa na Paula akaingia.Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba kwa kulia.Joe akastuka   “Paula what happened?  Paula akaenda pale kitandani na kumkumbatia Joe    “Joe sijalala usiku wa leo.Nimelia sana “ Paula akajibu  “Paula hata mimi sijaweza kulala usiku wa leo.Nimekesha macho nikiwaza juu ya mustakabali wetu.” Joe akasema na kumfanya Paula ainue kichwa chake na kumtazama kisha aksema   “Joe nimekuja kukuomba msamaha kwa yaliyotokea jana.Huwezi kufahamu tukio la jana limenisababishia maumivu gani moyoni.Sijawahi kuumia kama hivi katika maisha yangu.Nafahamu vile vile kwamba uliumia sana kwa kitendo  alichokifanya baba yangu.Kilikuwa si kitendo cha kibinadamu.Alikukosea heshima,alinikosea na mimi vile vile.Sielewi ni kitu gani kimemuingia baba yangu hadi akawa na roho mbaya namna ile.Joe nakuomba samahani sana kwa kitendo cha jana ,naomba unisamehe mimi kwa niaba ya baba yangu.Najiona kama mimi ndiye mkosaji.Tafadhali Joe naomba toka ndani ya moyo wako unisamehe na kwa pamoja tusahau yaliyotokea na tusonge mbele katika kulipigania penzi letu” Paula akamwambia Joe ambaye alikuwa amemkazia macho akimtazama   “Paula,siku zote nilikuwa nikifahamu kwamba lazima kutakuwa na ugumu kwa baba yako kuukubali uchumba wetu.Nilikwisha jiandaa kwa hilo ,lakini sikuwa nimetegema kwamba ingetokea kama ilivyotokea jana.Hakukuwa na ulazima wa mzee Stephano kufanya vile alivyofanya.Haikumlazimu yeye kunidhalilisha mimi ili kunyesha hasira zake kwa baba yangu.Alitakiwa anieleze kwa utaratibu unaofaa kwamba hawezi kuukubali uchumba kati yetu kuliko kunifukuza ndani mwake kama mnyama.Siku zote nimekuwa nikimchukulia baba yako kama baba yangu na ninampa heshima kubwa sana,lakini kwa kitendo alichonifanyia jana ,kilinifanya nijiulize mara mbili kama kweli mzee Stephano anastahili heshima kubwa kama hii.Sikufichi Paula niliumia sana.Sikuwahi kuumizwa kama nilivyoumizwa jana.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilihisi maumivu makali ya moyo kiasi kwamba nilihisa kama moyo wangu ukivuja damu.”Joe akatulia na kumtazama Paula mbaye alikuwa makini akimsikiliza    “Nilijiuliza sana nini sababu ya baba yako kunichukia namna ile?.Kwa namna sura yake ilivyokuwa jana nina uhakika baba yako alikuwa tayari hata kunitoa uhai wangu ili tu nisiweze kuwa na mahusiano na mwanae.Baadae ilinibidi niwaulize wazazi wangu sababu ya uhasama na chuki kubwa namna ile.Nilichokisikia kutoka kwa baba yangu kiliniumiza kiasi ambacho sijawahi kuumia katika maisha yangu”   “ Joe baba yako alikueleza nini sababu ya ugomvi wao?  Joe akavuta pumzi ndefu ,akamtazama Paula na kusema.   “Paula nitakachokueleza kitabadili kabisa maisha yetu,lakini sina budi kukueleza ukweli”   Joe akamweleza ukweli juu ya kila kitu kilichotokea hapo awali na kuzifanya familia zile ziishi katika uadui mkubwa.Mpaka anamaliza macho ya Paula yalikuwa yamejaa machozi.   “Joe tell me it’s a joke.tell me its not true..” Paula akasema huku akiinuka pale kitandani  “Kwa nini nikudanganye Paula? Huo ndio ukweli “  “Ouh My God why me? Puala akasema kwa uchungu huku akiishika sehemu ulipo moyo wake.Kimya kirefi kikatanda mle ndani .Baada ya dakika kama nne hivi Joe akasema    “ Paula tukisema tuongee kuhusu suala hili tunaweza kuongea mwaka mzima na tusipate muafaka.Baada ya kufikiria sana nimefikia uamuzi mmoja ambao nadhani itakuwa ni suluhisho kwetu.”   “Uamuzi gani huo Joe” Paula akauliza kwa wasi wasi  “Kwa kitendo alichokifanya baba yako,kimesababisha  jeraha kubwa moyoni mwangu na ambalo litachukua muda kupona.Nafahamu kwamba jambo hili limekuhuzunisha hata wewe pia.Kwa maana hiyo hata kama tukisema tupambane kwa dhumuni la kuwa pamoja tutakuwa tunajidanganya.Hatutaweza kuwa na furaha maishani.Kila nikuonapo usoni,nitakuwa nikikumbuka kitendo cha kikatili alichokifanya baba yako .I cant live with that Paula..I real can’t .Kwa maana hiyo itakuwa vyema kama uhusiano wetu utaishia hapa.I love you so much Paula,more than anything but I don’t think we’re made for each other.Lets put an end to our relationship.” Mara tu alipomaliza na kumtazama usoni Paula akaanguka na kupoteza fahamu..      Kitendo cha Paula kupoteza fahamu kikamstua Joe akamuendea pale alipokuwa  amelalal Paula na kuanza kumtikisa.   “Paula ! Paula “ Paula hakuwa na fahamu.Joe mwili ulikuwa ukimtetetmeka asijue afanye nini.Haraka haraka akatoka na kumwita mama yake ambaye alikuja mbio mle chumbani   “Ouh Mungu wangu.Amezimia huyu ! “  Mama yake Joe akasema kwa mstuko huku akimuinamia Paula.   “Fungua madirisha yote ipatikane hewa ya kutosha.”Akaamuru mama Joe  Joe akafungua madirisha na kusimama kando ya meza huku moyo ukimwenda mbio sana.    “Joe twende tumtoe humu ndani tumpeleke seuleni kwenye hewa ya kutosha.” Mama Joe akasema na  kwa pamoja wakambeba Paula na kumtoa mle chumbani wakampeleka sebuleni .Paula akalazwa katika sofa kisha mama Joe akaanza kumpepea.   “Joe umemfanya nini mwenzio kiasi cha kumfanya apoteze fahamu?  Huku akionekana kuwa na wasi wasi mwingi Joe akasema   “mama sijamfanya kitu chochiote kibaya zaidi ya kumweleza wazi kwamba kutokanana mambo yaliyotokea hatuwezi tena kuendelea na mahusiano yetu”   “Ouh Joe ! Kwa nini lakini umefanya hivyo? Mwenzio huyu anakupenda sana na ndio maana amepatwa na mstuko mkubwa ulipomwambia kwamba hamuwezi kuendelea kuwa na mahusinao.” Mama Joe akasema   “mama sikuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kumweleza ukweli Paula.Itakuwa vizuri kama kila mmoja akiumia lakini baada ya muda tutasahau na kuendelea na maisha yetu ya kawaida  kuliko mateso ambayo nitakuwa nayo kama  nitaendelea kuwa na mahusiano na Paula”    “Joe tafadhali usimtese hivyo huyu mtoto .Paula ni binti mzuri na ambaye anakufaa sana katika maisha yako.Tafadhali mwanangu usivunje uhusiano wako naye” Mama yake akasissitiza.   “mama najua mnampenda Paula sana ,na hata mimi nampenda mno lakini kutokana na yaliyotokea hatutaweza tena kuendeleza mahusiano yetu.Itakuwa vizuri kama kila mmoja akaendelea na maisha yake mwenyewe” Joe akasisitiza huku mama yake akimuangalia kwa jicho kali.   “Joe unafanya makosa makubwa sana” mama yake akasema  huku akiendelea na zoezi la kumpepea Paula.   Baada ya dakika kumi Paula akafumbua macho.Joe akapumua kwa nguvu .Paula akageuza macho na kutazamana na Joe,machozi yakaanza kumtoka.   “Paula ,nyamaza kulia mwanangu.”mama Joe akambembeleza.  “mama siwezi kunyamaza.Joe amesema hanitaki tena.Nimemkosea kitu gani mama? Paula akasema huku akilia   “nyamaza Paula.haya ni masuala madogo mtaongea yatakwisha”  “mama , Joe ndiye maisha yangu,nitawezaje kuishi bila yeye?Ninaumia sana moyoni mama” mama Joe akasikia uchungu mwingi akashindwa kuvumilia kumuona Paula akilia.Akamfuata Joe aliyekuwa ametoka  nje   “Joe hebu nenda kakae uongee na mwenzio mumalize haya mambo.Kwa nini lakini unamtesa mwenzio kiasi hiki? Mama Joe akawa mkali kwa mwanae.Taratibu Joe akajivuta kuelekea ndani.Paula alipomuona Joe akataka kuinuka na kumfuata lakini Joe akamuwahi.   “Paula kaa upumzike.Unahitaji mapumziko”  “Joe naomba uniambie nimekukosea kitu gani hadi unifanyie hivi? Ninakupenda Joe.Wewe ndiye mwanaume wa pekee kwangu katika hii dunia.Naomba tafadhali tuziweke tofauti za wazazi wetu pembeni lakini tuendelee kuwa pamoja”   Joe akamtazama Paula kwa macho ya huruma na kusema   “Paula wewe ni binti wa pekee sana ambaye kila mwanaume wa dunia hii anaota awe nawe.Ninakupenda sana Paula zaidi ya unavyoweza kufikiri.Naomba unielewe Paula kwamba nilichokisema hakimaanishi kwamba sikupendi .Ninakupenda sana.Nilisema vile kwa faida yetu sote kwani wote tunahitaji kuwa na maisha yenye furaha na amani siku zote.Kwa kitendo alichokifanya baba yako,kamwe katika maisha yangu sintaweza kuwa na amani moyoni.Kama nitakuwa nawe nitakuwa nikiumia sana kila ninapokuona.Tafadhali naomba unielewe Paula.” Joe akasisistiza.   “Kwa maana hiyo unanihukumu kwa kosa alilolitenda baba yangu? Paula akauliza   “Si kwamba nakuhukumu lakini naomba utambue kwamba baba yako alifanya jambo baya sana .Kitendo alichokifanya ni cha kinyama mno na hakivumiliki.” Joe akasema huku sauti yake ikianza kupanda kuonyesha ni jisni gani alivyochukizwa na kitendo kile cha baba yake Paula   “Joe lazima tukubali kwamba wazazi wetu sote wamefanya makosa kwa hiyo hatupaswi kuteseka kwa makosa waliyoyafanya wao”   “Makosa ? wazazi wangu mimi hawajafanya kosa lolote.Ni baba yako ndiye aliyefanya kosa baya sana.” Joe akasema kwa sauti kubwa.   “Si baba yangu tu aliyechangia mambo haya kufika hapa yalipofika” Paula akasema  “Paula nakuomba usiwahusishe wazazi wangu na mambo aliyoyafanya baba yako ambaye ana roho mbaya kama shetani…..”Joe akasema kwa ukali lakini ghafla Paula akasimama huku amefura kwa hasira.   “Enough Joe ! Stop saying bad things about my father !! “ Paula akasema kwa ukali   “kwa hiyo unamtetea baba yako kwa mambo anayoyafanya? “ Joe akauliza   “Hata kama mefanya makosa he is still my father and you have to respect him,sintavumilia kusikia ukimtusi baba yangu mbele yangu” Paula akafoka   “paula nakushangaa sana unaposimama na kumtetea baba yako ambaye akiwa na akili zake timamu alidiriki kumbaka mama yangu mzazi…..” Joe akasema lakini Paula akaingilia kati   “Umesahau kwamba ni baba yako ndiye aliyemfunga baba yangu gerezani ili kulipiza kisasi.Mbona mimi silalamiki wala kumtusi baba yako?   “Funguka macho Paula,baba yako alifungwa kwa sababu ni mhalifu.Aliiba fedha ya umma.Laiti ningekuwa mimi ndiye hakimu ningemhakikisha anafia gerezani”   Paula akachomwa na kauli ile akajikua akimnasa kibao kikali Joe.  “Na uwe ni mwanzo na mwisho kumdharau baba yangu.”    Kwa kasi ya aina yake Paula akatoka mle sebuleni na kuelekea kwao.mama Joe akaingia mle sebuleni huku akihema   “Joe kumetokea nini? Mbona mwenzio ametoka kwa kasi huku akilia?   “mama kilichotokea nimemweleza ukweli Paula lakini badala yake anasimama na kumtetea baba yake ambaye mimi namuona kama shetani.”   “Joe umefanya makosa sana.Unatakiwa umuombe msamaha mwenzio.Hukupaswa kumdharau mzazi wake hata kama amekutendea jambo gani.Ulitaka akuunge mkono wakati ukimtusi baba yake? Joe,yule ni baba yake mzazi hata ufanye nini atabaki kuwa baba yake na siku zote hatakubali baba yake adhalilishwe na mtu yoyote”   “mama kama ni hivyo yeye  ndiye aliyepaswa kuniomba msamaha mimi kwa sababu baba yake ndiye aliyeanzisha mambo haya yote.” Joe akasema huku mama yake akimtazama kwa macho makali    “Joe katika siku ambazo umenisikitisha ni siku ya leo.Kitendo cha kuamua kuachana na Paula kimenichukiza moyo wangu sana.Ninampenda yule msichana na ni yeye pekee anayekufaa maishani mwako.Iko siku moja utayakumbuka maneno yangu lakini utakuwa umeshachelewa sana.” Mama Joe akasema na kuondoka kwa hasira pale sebuleni akaingia chumbani kwake,..   “Vyovyote vile itakavyokuwa mama,lakini sihitaji kuwa na Paula tena maishani.Nimeshaamua na hakuna ambaye atayabadili maamuzi yangu” Joe akasema taratibu huku naye akielekea chumbani kwake. 

0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi