MASIMULIZI
Saturday, April 12, 2014
TEN CHAPTERS SEHEMU YA 11
RIWAYA: TEN CHAPTERS
SEHEMU YA 11
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Naomi akiwa amejifungia chumbani akasikia mlango wake ukigongwa.Kwa uchovu akainuka na kwenda kuufungua .Akakutana na kaka yake.
" Samahani Naomi,najua ulisema hutaki kuonana na mtu yeyote yule lakini Genes amekuja na anaomba japo akuone kwa dakika moja tu."
kauli ile ya kaka yake ikaamsha tena kilio kwa Naomi.
" kaka nimekwambia sitaki kuonana na mtu yeyote leo especially Genes.." akasema Naomi na kuufunga mlango.
" Naomi !! Ikasikika sauti kubwa ya Genes.Kaka yake Naomi akastuka.Hakujua kama Genes alikuwa akimfuata.
" Naomi naomba nionane nawe tafadhali..!! . akasema Genes akiwa ameuegemea mlango.
Muda ulizidi kwenda bila ya mlango kufunguliwa.Genes akakaa chini na kuuegemea mlango wa chumba cha Naomi.
" Nitakesha hapa mlangoni.Sintaondoka hadi nionane na Naomi" akasema Genes
" Sintaondoka hadi nionanane nawe Naomi.Ni wewe pekee ninayekuhitaji katika maisha yangu.Nitaishi nawe hivyo hivyo...."
Akasema Genes huku akilia.
Ndani ya chumba Naomi alikuwa akilia machozi kwa uchungu hasa baada ya kusikia sauti ya Genes akilia kwa kwikwi pale nje ya mlango wake.
" I love you Genes ..I love you so much but I cant be with you again." akasema Naomi kisha akafungua dirisha
na kuruka nje.Taratibu akapanda geti na kushuka upande wa pili kisha akatokomea kizani
ENDELEA…………………………………….
Baada ya kuruka dirisha
na kutokomea kizani,Naomi alisimama mita chache toka ilipo nyumba ya kaka yake na kuitazama huku machozi mengi yakiendelea kumtoka.
“ Utanisamehe Genes lakini sitaki kuonana nawe kwa sasa.Pengine hatutaweza kuonana t ena katika maisha yetu yaliyobaki.This is for the best of us.” Akasema Naomi kwa sauti ndogo halafu akaanza kutembea kwa haraka.Alitembea hadi katika klabu moja ya burudani pale akaita taksi.Dereva taksi akamshangaa Naomi kwa namna alivyokuwa.Alikuwa amesawajika mno.Nywele zake nzuri zilikuwa zimevurugika,miguuni hakuwa na viatu
“ dada una matatizo? Akauliza yule dereva taksi wakati akiliondoa taksi
“ Kaka naomba unipeleke sehemu niliyokuomba tafadhali,” akajibu Naomi
“ Samahani dada yangu,nilitaka tu kufahamu kama umepatwa na tatizo pengine ninaweza kukusaidia.”
“ Ahsante sina tatizo” akasema Naomi na safari ikaendelea.Bado machozi yaliendelea kumtoka kila alipomfikiria Genes na kilichotokea
“ Sijui Genes atakuwa katika hali gani mida hii.Ouh gosh ! nimemsababishia mateso makali ya moyo. Ni kijana mzuri ,mwenye moyo wa huruma na upendo.Ananipenda na hata mimi ninampenda sana.Ni mwanaume ambaye niliamini kwamba ndiye nitakayekuwa naye katika maisha yangu yote yaliyobaki hapa duniani lakini kumbe nilikuwa najidanganya nafsi yangu.Kwa hali hii niliyonayo sintaweza kuwa na mwanaume ambaye moyo wangu unamtaka.Sintaweza tena kuwa na Genes.Kwa nini dunia inaniadhibu namna hii? Haya yote niliyoyapitia hayatoshi
hadi niendelee kuteseka namna hii? Nimefanya jambo gani baya kiasi cha kuadhibiwa namna hii? Akazama katika mawazo huku machozi mengi yakiendelea kumtoka
“ Nilidhani maisha yangu tayari yametulia na nitakuwa na furaha daima baada ya kumpata Genes mwanaume wa maisha yangu lakini haiwezekani tena.Inaniuma sana kuachana na mwanaume niliyempenda katika kwa moyo wangu wote tena siku chache kabla ya ndoa yetu.Najua ataumia sana lakini hakuna namna nyingine ya kufanya kwa sasa zaidi ya kwenda kuishi mbali naye..” Akawaza Naomi na kuinamisha kichwa
chini
Dereva taksi akasimamisha gari katika nyumba aliyokuwa ameelekezwa na Naomi.Akaufungua mlango akashuka na kumuomba dereva amsubiri ili aweze kumletea pesa yake .Akaenda kugonga katika dirisha la tatu upande wa mbele
na mara pazia likafunuliwa na sura ya mwanadada mmoja ikajitokeza.
“ Trisha ni mimi Naomi.Naomba unifungulie” akasema Naomi na baada ya muda wa dakika mbili hivi geti likafunguliwa
“ Naomi !!..” akasema
mwanadada yule aliyetoka ndani kwa mshangao mkubwa
“ What happened !!!” akasema tena huku akimkumbatia Naomi
“ Trisha naomba kwanza umpatie yule kaka wa taksi pesa yake aondoke” akasema Naomi.Trisha akakimbia ndani akatoka na hela akampatia yule dereva taksi akaondoka zake
“ Karibu ndani Naomi” akasema Trisha huku bado akiendelea kumshangaa Naomi.hakuwahi kumuona hata siku moja Naomi akiwa katika hali ile
“ Naomi niambie nini kimetokea? Akauliza Trisha baada ya Naomi kuketi sofani
“ Trisha ni mambo makubwa sana lakini naomba tafadhali tusiyaongelee mambo hayo kwa sasa.I need to rest for now” akasema Naomi
“ Naomi .! Mimi ni rafiki yako mkubwa na hata siku moja sijawahi kukuona ukiwa katika hali kama hiyo.Nini kimekupata? Nahitaji kujua Naomi.Tafadhali naomba unieleze”
“ Trisha nafahamu kwamba wewe ni kila kitu kwangu na siwezi kukuficha jambo lolote lile,lakini naomba kwa hili tusiliongelee kwa sasa.Nitakueleza lakini si usiku huu.Nahitaji kwanza nipumzike”
akasema Naomi
Trisha akamuangalia Naomi kwa mshangao.Aliogopa sana.Bila kupoteza muda Naomi akapanda kitandani na kujilaza.
“ Trisha kitu kingine naomba usimweleze mtu yeyote kwamba niko hapa kwako usiku huu”
“ Hata kaka yako?
“ Huyo ndo sitaki kabisa
ajue mahala niliko usiku huu” akasema
Naomi halafu akajifunika shuka
“ Masikini Genes sijui atakuwa katika hali gani huko aliko.Nimemsababishia maumivu makubwa ya moyo. Ataumia sana lakini bado anayo nafasi ya kumpata mwanamke wa ndoto zake.Ni kijana mzuri mwenye kila
sifa na nina hakika lazima atampata mwanamke mwenye sifa na watapendana sana japokuwa itamchukua muda mrefu kunisahau.Alikuwa na matarajio makubwa na mimi.Tulikuwa na ndoto nyingi sana siku za usoni.Tulipanga tutengeneze familia nzuri yenye furaha na upendo lakini yote hayo hayawezekani tena.Kwa sasa
ninachotakiwa kukifanya ni kimoja tu..to disappear.Natakiwa niondoke kabisa na kupotea
and this is my life for now ” akawaza Naomi akiwa amejifunika shuka huku bado akiendelea kulia.
“ Yes ! I have to disappear.Natakiwa nifutike kabisa machoni mwa Genes. Kesho nitaanza safari yangu .Nitaondoka Arusha na kuelekea Dar es salaam.Kuna mambo ambayo natakiwa nikayafanye pale na baada ya kukamilisha mambo hayo nitapotea kama upepo vile.No body will see me again.Wengi watasikitika sana lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutoweka.” Akaendelea kuwaza Naomi
“Zilibaki siku chache tu
kabla yakufunga ndoa . Kwa nini
mambo haya yanaibuka wakati huu ambao nimekwisha yajenga tena maisha yangu na kuanza kusahau maisha ya nyuma yaliyopita? Nadhani huu
ni mwendelezo wa y ale mabalaa ambayo yamekuwa yakiniandama kwa muda mrefu .Nimepitia mambo mengi sana lakini kwa hili la sasa limeniumiza mno.Nimeumia sana hasa ukizingatia kwamba tayari nilikwisha mpata mwanaume wa maisha yangu mwanaume ambaye ninampenda kwa moyo wangu wote.Inauma sana lakini yote namuachia Mungu yeye
ndiye atakayenisaidia kwa hili nitakaloenda kulifanya.” Akaendelea kuwaza Naomi huku akilia.
**********************************
Ni saa sita na dakika nane za usiku bado Genes amekaa katika mlango wa chumba cha
Naomi.Bado Naomi hakuwa ameufungua mlango wake.
“ Naomi tafadhali fungua mlango nataka niongee nawe.Naomba usinifanyie hivi tafadhali” akasema Genes akiwa amekaa chini mlangoni.
Kaka yake Naomi naye akaja na kuanza kugonga mlango akimtaka Naomi afungue lakini mlango haukufunguliwa.Akaenda chumbani kwake na kurudi na lundo lafunguo. mkononi .Akaanza kujaribisha funguo moja baada ya nyingine na mara funguo moja ikakubali mlango ukafunguka.Wote wakapigwa na butwaa baada ya kukuta chumba kikiwa kitupu.Naomi hakuwepo.
“ Naomi yuko wapi? Akauliza genes
“ Hata mimi nashangaa.Lakini alikuwa humu chumbani kwake
na sikumuona ametoka” akasema kaka yake Naomi halafu akaelekea katika dirisha lililokuwa wazi
“ Naomi atakuwa ameruka kupitia hapa dirishani na kuondoka.”
“ Ouh my gosh !!..where is she now ? akauliza Genes kwa wasi wasi
“ Sifahamu atakuwa wapi..” akasema kaka yake Naomi huku akionekana kuogopa sana
“ Ouh jamani Naomi kwa nini lakini mambo haya yanatokea? Umekwenda wapi? Akalalama Genes
“ Kwa hiyo tunachukua hatua gani? Akauliza Genes
“ Hakuna cha kufanya kwani sifahamu ni wapi tutaanza kumtafutia Naomi.Ninaona tusubiri hadi kupambazuke ndipo tujue ni wapi atakuwa ameelekea.Nina hakika kesho lazima atarejea kwa sababu kila kitu chake kiko humu.Hajaondoka na kitu chochote kile na hata simu yake hii hapa mezani”
“ Kama hajachukua kitu chochote basi hatakuwa ameenda mbali atakuwa maeneo
ya karibu na hapa nyumbani.Twende tukamtafute kuzunguka nyumba.Kuna mahala atakuwa amejificha akikwepa kuonana nami” akashauri Genes
Wakatoka na kuanza kuizunguka nyumba nzima wakimtafuta Naomi lakini hawakuweza kumuona.
“ Naomi hawezi kukaa maeneo haya Genes.Lazima kuna mahala amekwenda.Tusubiri hadi kesho asubuhi tutapata jibu.Kwa sasa ngoja niwapigie simu watu kadhaa niwaulize kama anaweza kuwa amekwenda kwao” akasema kaka yake Naomi na kuchukua simu yake akaanza kuwapigia watu kadhaa akiwaulizia kuhusu Naomi.Aliwapigia watu zaidi ya kumi lakini hakuna hata mmoja aliyefahamu
Naomi alikuwa wapi usiku ule
“ Katika marafiki zake ninaowafahamu hakuna hata mmoja wao ambaye anafahamu wapi alipo Naomi usiku huu.Ninamfahamu Naomi lazima kuna mahala atakuwa amekwenda .”
“ Kwa nini tusitoe taarifa polisi ? akauliza Genes
“ Hakuna haja ya kwenda polisi.Naomi yuko salama na kesho atarejea hapa.Usiwe na wasi wasi Genes Naomi ni msichana mkubwa na anajua kujilinda”
Saa nane za usiku Genes akarudishwa nyumbani kwa gari.Chumba cha Naomi kilikuwa kimefungwa . Kwa kuwa alikuwa na ufunguo wa akiba akafungua chumba kile .Chumba kilikuwa kitupu Naomi hakuwepo.Akakaa kitandani na kulia kwa uchungu
“ Naomi uko wapi mpenzi wangu? Kwa nini umeniacha nikiteseka namna hii? Kwa nini umenikimbia malaika wangu? Ninahitaji kuongea nawe.nahitaji tukae
tuliongelee suala hili .Niko tayari kwa kila ktu na hakuna kitu kitakachoweza kunizuia mimi kuwa nawe.Hata kama umeathirika mimi bado ninakupenda na niko tayari kwa lolote kwa sababu yako Naomi.Please come back my love..I need you now and always..” akasema Genes kwa uchungu huku machozi mengi yakimtoka .Alikuwa amekaa kitandani mkononi akiwa na picha ya Naomi .Akaikumbatia picha ile kwa nguvu
“ Ouh Naomi kwa nini yametokea haya hawa kwa wakati huu ambao tumekaribia
kuitimzia ndoto yetu? Why you my love? ..akazidi kulia Genes halafu akarejea tena chumbani kwake.Alihisi kichwa chake kizito sana .Mawazo mengi yalimsonga.Akakaa katika sofa na kuanza kukumbuka toka siku ya kwanza alipomtia machoni Naomi na hadi walipoanzisha mahusiano yao na kuwa wachumba.Taratibu isingizi ukaanza kumpitia akalala pale pale sofani
****************************
Saa kumi na mbili za asubuhi Genes akastuka toka usingizini.Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuchukua simu yake na kumpigia kaka yake Naomi na kumuuliza kama ana taarifa zozote za Naomi.bado hakukuwa na taarifa zozote za wapi alipo Naomi.Kichwa cha Genes kikajaa mawazo mengi
“ Ninampenda sana Naomi kwa moyo wangu wote na ni mwanamke pekee ambaye ananifaa katika maisha yangu.Hata kama tayari ana virus vya ukimwi mimi sijali.Nitakuwa naye hivyo hivyo.Nitamtafuta kokote aliko na nitaishi naye .Najua kitendo cha kukutwa na virusi ndicho
klichomfanya akatae kuonana nami na kukimbia.” Akawaza Genes halafu akasimaa na kuangala darini
“ Ninafahamu kwamba Naomi amekimbia kwa sababu moja tu .Anajua kwamba mimi ninampenda na niko tayari kuishi naye hata kama tayari ana virusi vya ukimwi .Ananipenda sana na lengo lake ni kunizuia nisiambukizwe
virusi.Ninachotakiwa kujiuliza hapa ni je niko tayari kuishi na mtu mwenye virusi vya ukimwi hata kama ninampenda? Akajiuliza Genes na kukaa kwa sekunde kadhaa kitafakari.
“ ni swali gumu sana lakini kwangu mimi jibu lake ni ndiyo.kwa namna ninavyompenda Naomi niko tayari kuishi naye hata kama ana virusi vya ukimwi.Japokuwa nafahamu suala hili lazima litapinga vikali sana na ndugu na jamii nzima lakini sioni mwanamke mwingine mwenye kunifaa maishani zaidi yake. Yeye ni kila kitu kwangu.Siko tayari kuishi na mwanamke mwingine katika hii dunia zaidi ya Naomi.Kinachofuata hapa ngoja nikaanze kumtafuta mimi mwenyewe.Siwezi kusubiri hadi atakaporejea.Nitaanzia ofisini kwao..” akawaza genes na kuchukua maji akakimbia bafuni kuoga halafu akaelekea ofisini kwa Naomi
Saa nne za asubuhi Naomi akarejea chumbani kwake .Kabla hajaingia chumbani kwake alichunguza kwanza kama Genes alikuwepo pale na alipohakikihsa kwamba hakuwepo ndipo alipoingia ndani.Macho yalikuwa yamemvimba
kutokana na kulia .Alikitazama chumba chake halafu akachukua sanduku
na kuanza kupakia nguo na baadhi ya vitu
vyake vya muhimu.Alipomaliza akachukua kalamu na karatasi na
kuandika barua . Mara kadhaa alisimama kuandika barua ile na kujifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka.Alipomaliza kuandika barua ile akaisoma huku
machozi yakimtoka.
“ Utanisamehe Genes lakini lazima nifanye hivi kwa faida yetu sote.Ninakupenda sana na siku zote nitaendelea kukupenda.Wewe ni ,mwanaume wa pekee
kabisa kuwahi kutokea maishani mwangu
.” akasema Naomi huku akifuta machozi akatoka chumbani kwake na kwenda kuipenyeza
barua ile chini ya mlango wa chumba cha Genes,akarejea chumbani kwake na kuita taksi ambayo ilifika kwa haraka akapakia sanduku lake na kuondoka zake.
“ Kwa heri genes.Hatutaonana tena katika maisha haya.Kitu kimoja tu ambacho kitabaki moyoni mwangu ni kwamba sijawahi kumpenda mwanaume kama nilivyokupenda Genes.” Akawaza Naomi wakati akiondoka pale nyumbani.
NAOMI AMEKWENDA WAPI? NINI ANATAKA KUKIFANYA ? TUENDELEE KUWA PAMOJA KATIKA SIMULIZI HII.
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment