Saturday, April 12, 2014

SERENA SEHEMU YA 11




Wapo watu wengine wengi na wazito ambao hawatakiwi kujulikana kabisa kama wanashirikiana nasi.Linapotokea suala linalotuhusu kila mmoja hufanya kazi hiyo katika sehemu yake.Kwa hiyo Mr Patel  usistuke.Tunao madaktari wa kutumainiwa wanaoweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi katika mazingira yoyote na wakati wowote.Ila naomba nisiwataje kwa majina wala wanatoka katika hospitali zipi hapa nchini kwa sasa.Naomba tu muelewe kuwa  wapo na wako tayari kufanya kazo yoyote tutakayowapa”




            “Shughuli ilianza kwa kasi ya kutia matumaini.Baada ya miezi mitano, kupitia mtandao wa vigogo hao,kampuni iliweza kuidhinishiwa mabilioni ya fedha.Baada ya mwaka mmoja tena tukachota mabilioni mengine ya fedha na mwaka jana tumemaliza kabisa kiasi kilichokuwa kikitakiwa kulipwa kwa ajili ya kandarasi ile.Mpaka sasa hivi mradi umesimama na pesa za mradi zote zimekwishachukuliwa .Hakuna yeyote ajuaye kama mabilioni haya yamekwishachotwa na mtandao wa vigogo kupitia kampuni yangu.Kila kitu kimekwisha wekwa sawa,namaanisha kuhusu mambo ya kule benki kuu na si rahisi kwa mtu asiyehusika kuelewa kuhusu mabilioni haya mengi ambayo mengi ni fedha za wafadhili,kupitia mfuko wao wa kusaidia mapinduzi ya kijani Tanzania.Matakwa ya mradi huo yalitaka kushirikisha pia sekta binafsi,na wadau mbali mbali wa kilimo.Mzee Albano akaitwa na kuombwa kushiriki katika mradi huo na kuelezwa jinsi atakavyonufaika nao akiwa kama mdau mkubwa wa sekta ya kilimo kwani yeye ana viwanda vya kusindika mazao karibu katika kila mkoa nchini.Mzee Albano alikubali kushiriki katika mradi ule.Mambo yalibadilika pale mabilioni ya kwanza yalipotoka na yakagawanywa.Mzee Albano alishangaa pale alipopewa mgao wake.Mwanzoni alikataa lakini baada ya kuonywa kuwa ni lazima achukue pesa zile alizitunza katika akaunti maalumu bila kuzitumia.Mwaka jana mzee Albano aliibuka tena na kudai kuwa anataka kurudisha pesa zile alizogawiwa na  kujitoa kabisa katika mradi.Baada ya kumkatalia kufanya hivyo,aliazimia kurudisha fedha zile kwa lazima na kisha kuutangazia umma juu ya uchotwaji wa fedha ile nyingi.Kitendo cha yeye kutaka kuutangazia umma juu ya mradi ule hewa ni cha hatari kwani mtandao huu una vigogo wengi wa serikali na watu wenye nyadhifa kubwa,wafanya biashara wakubwa n.k.Hatukuwa tayari kuona hilo linatokea kwa hiyo azimio likawa ni kuhakikisha kwa gharama zozote zile mzee Albano ananyamazishwa.Natumai unaelewa ninamaanisha kitu gani.Si kwamba ugonjwa wa mzee Albano hautibiki ,lakini ilikuwa ni moja ya mikakati yetu ya kuhakikisha kuwa mzee huyu haponi na anakufa katika mazingira ambayo hayatakuwa na mashaka yoyote.Baada ya Dr Jason kugundua kuwa kuna uwezekano wa kumfanyia upasuaji mzee Albano imebidi tuingie kazini tena kuhakikisha kuwa kwa gharama zozote zile hili halifanikiwi.Sikufichi Dr Henry hata jaribio la jioni hii ni sisi ndio ndio tulilifanya na kwa bahati mbaya likashindikana.”

0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi