MASIMULIZI
Friday, April 11, 2014
TEN CHAPTERS SEHEMU YA 10
RIWAYA : TEN CHAPTERS
SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa iliwalazimu akina Genes wakapime kama wako salama na maambuki ya virusi vya ukimwi au kuna mmoja kati yao ameathirika.Ili kulifanya zoezi hilo kuwa la uhakika zaidi ,siku ya kupima waliongozana na mzee moja wa kanisa .Hakuna aliyekuwa na wasi na afya yake hata kidogo.Wote walikuwa wazima wa afya.Ndani ya gari la Naomi wakati wakielekea hospitalini kupima kulitawaliwa na vicheko na utani kama kawaida yao.
Damu zao zilichukuliwa na kupelekwa maabara kwa ajili ya vipimo.Baada ya saa moja majibu yao yakawa tayari.mzee wa kanisa akaitwa kwanza ndani akaongea na daktari kwa muda wa kama nusu saa hivi halafu wakaitwa akina Genes....Daktari aliwaeleza bayana alichokuwa amewaitia wote wawili ni kwa sababu damu ya mmoja wao imekutwa na virusi vya ukimwi..Wakatazamana..Kijasho kikawatoka.Wote mapigo yao ya moyo yakaanza kwenda kwa kasi ya ajabu sana..Walianza kuogopa.Hizi zilikuwa ni taarifa za kustusha sana..Ukimya mzito ukatanda mle ofisini kwa daktari.Taratibu daktari akalifungua faili lake na kuwatazama.Alimtazama sana Genes usoni kwa macho ya masikitiko....Kisha akisema
" Genes.."
" naam dokta" akajibu Genes kwa uoga.Daktari akamuangalia tena usoni.Genes jasho lilikuwa likimtiririka
ENDELEA................................................................................................
" Mbona unanitazama kwa uoga namna hiyo? akasema daktari huku akicheka .Genes akajifuta jasho na kujilazimisha kucheka kidogo.
" Umenistua sana daktari kwa taarifa yako ya kwamba mmoja wetu ameathirika na virusi vya ukimwi" akasema Genes huku akiendelea kujifuta jasho lililokuwa likimtiririka kwa wingi.Daktari akatabasamu na kusema
" Nawaombeni msistuke tafadhali." akasema daktari halafu akaanza kuwapa ushauri na kuwapa moyo kuhusiana na kupokea majibu ya vipimo vyao.Pamoja na ushauri ule bado haukusaidia kuwafanya Genes na Naomi nafsi zao zitulie.Baada ya kama nusu saa hivi ya daktari kuwapa somo , akalifungua faili lake akalisoma kidogo halafu akainua kichwa na kuwatazama akina Genes.
" Genes na Naomi ,kama nilivyowaeleza hapo awali kwamba katika vipimo tulivyovifanya tumegundua kwamba mmoja wenu ameathirika na virusi vinavyosababisha ukimwi.Kwa kuwa ninyi mnatakiwa kufunga ndoa hivi karibuni itakuwa vyema mkiyapata majibu yenu mkiwa pamoja.Je mko tayari kupokea majibu yenu? akauliza daktari
" Tuko tayari daktari" akasema Genes.
" Naomi vipi kuhusu wewe , uko tayari kwa majibu? akauliza daktari baada ya Naomi kuwa kimya.
" Niko tayari daktari" akajibu Naomi.
" Nafurahi kusikia hivyo" akasema daktari halafu akalitazama tena faili lile lenye majibu ya akina genes akasema
" Baada ya vipimo tumegundua kwamba damu ya Naomi ina maambukizi ya virusi vya ukim....." Kabla hajamaliza sentensi yake Naomi akaanguka na kupoteza fahamu.Haraka haraka akapakiwa katika kitanda maalum cha magurudumu na kukimbizwa katika chumba cha huduma ya dharura akaanza kupatiwa huduma .Wakati Naomi akiendelea kupatiwa huduma Genes alikuwa amejinamia akilia machozi.Mwalimu yule wa dini waliyekuwa naye pale hospitali pamoja na madaktari na washauri walikuwa wakijitahidi kumsaidia ili aweze kunyamaza .Juhudi zao zilizaa matunda na Genes akanyamza lakini bado alikuwa katika uchungu mkubwa.Akachukuliwa na kupelekwa katika chumba maalum ambacho aliombwa apumzike wakati akiendelea kupatiwa ushauri.Kwa dakika kadhaa eneo lile la hospitali lilikuwa na pilika pilika kubwa kutokana na tukio la Naomi kupoteza fahamu ghafla.
" Ouh jamani ni mkosi gani huu nimeupata mimi ? bado siamini..Siamini kabisa kama Naomi ameathirika .Nitafanya nini mimi? ..akalia kwa sauti Genes akiwa katika kile chumba alichokuwa amewekwa ili apumzike.
" Naomi ndiye msichana pekee ambaye ninampenda katika hii dunia.Nitafanya nini sasa bila ya kuwa naye? Hapana haiwezekani..This is not true.." akaendelea kulalama Genes kama mtu aliyechanganyikiwa.Jitihada za madaktari na wanasihi za kumtuliza Genes zilishindwa kuzaa matunda.Genes hakumsikiliza mtu yeyote.Alikuwa katika wakati mgumu sana .Alikuwa amekaa sakafuni akiwa amekilaza kichwa chake magotini.
" Ouh Mungu wangu nisaidie katika wakati huu mgumu nilionao kwa sasa.Naomba hii iwe ni ndoto na nikiamka Naomi awe mzima wa afya.Ninahitaji kumuoa Naomi.Ni msichana pekee ninayempenda katika hii dunia.Ni yeye pekee ambaye ninataka kuishi naye.." akasema Genes .Wote waliokuwamo mle chumbani wakamuonea huruma sana kwa hali aliyokuwa nayo.Ilikuwa ni hali ya majonzi makubwa.Madaktari wakashauriana na kuamua kwamba wamchome Genes sindano ya usingizi ili aweze kulala wakati Naomi akiendelea kupatiwa tiba.Hakukuwa na njia nyingine ya kumtuliza Genes zaidi ya kumchoma sindano ya usingizi ili alale.
" Daktari naomba rudieni kumpima tena Naomi.Naomi ninamfahamu vizuri hana maambukizi.Ni mpenzi wangu ninamfahamu vizuri.Tafadhali daktari naomba rudieni tena kumpima" akalalama Genes kama mtu mwenye matatizo ya akili.Daktari akamuomba atulie kitandani.Mara tu alipopanda kitandani akachomwa sindano ya usingizi na baada ya muda mfupi taratibu akaanza kufumba macho na hatimaye akalala.Walipohakikisha kwamba amelala kabisa madaktari wakaondoka na kumuacha muuguzi mmoja wa kumsaidia endapo ataamka.Wote wakaelekea katika chumba alichokuwa amelazwa Naomi.
“ Inasikitisha sana kwa kweli.Vijana hawa walikuwa tayari wamemaliza maandalizi yote ya harusi yao na hawakutegemea suala kama hili lingejitokeza.Inatia uchungu sana” daktari mmoja akamwambia mwenzake wakati wakielekea katika chumba alicholazwa Naomi
“ Inauma sana .Lakini hii inachangiwa na watu kutokupima afya zao mara kwa mara.iwapo kama wangekuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara wangeweza kugundua toka mapema kama mmoja wao ana maambukizi ya virusi vya ukimwi.” Akasema daktari mwingine.
“ Ninamuonea huruma yule msichana.Ni mzuri sana. Ninadhani hata yeye hakutegemea kama angeweza kuwa na maambukizi.Wanapendana sana na sijui watafanya nini baada ya mmoja wao kugundulika kuwa ameathirika.”
“ hakuna kitu kitakachoendelea tena . Mambo inabidi yafikie mwisho.najua inaumiza sana lakini hiyo ndiyo hali halisi.Yule kijana hana maambukizi ya virusi na iwapo ataoana na huyu binti basi lazima naye atapata maambukizi kitu ambacho hatutaki kitokee.Hatutaki maambukizi mapya yaendelee kutokea.Watabaki kuwa marafiki na endapo binti atataka kuolewa itamlazimu atafute mwenzake ambaye naye ana maambukizi haya na kwa pamoja wanaruhusiwa kuoana na hata kutengeneza familia.” Akashauri daktari .Kila mmoja alikuwa ameguswa sana na tukio lile.
* * * *
Genes alizinduka saa kumi na moja za jioni.Macho yake yalikuwa mazito sana kufunguka.Wauguzi walikuwapo pembeni yake wakamsihi atulie kwanza kwani alikuwa akitaka kunyanyuka.
" Genes,tulia kwanza.Endelea kupumzika....." akasema muuguzi mmoja mwenye umri wa makamo.
Genes akanyoosha mkono na kumfanyia ishara yule muuguzi amsogelee karibu.Akamuinamia Genes ili kumsikiliza alichotaka kukisema.
" N...Na...Naomi..." akasema Genes.Ulimi wake ulikuwa mzito kutamka.
" Endelea kulala Genes" akasema yule muuguzi.Genes akajitahidi na kusema kwa sauti ndogo
" Yuko wapi Naomi?
Wale wauguzi wakatazamana wao kwa wao hali iliyozidi kumpa wasi wasi Genes.Akakusanya nguvu chache alizokuwa nazo akainuka na kukaa kitandani.
" Nipelekeni alipo Naomi" akasema Genes kwa sauti ndogo.
" Genes naomba uendelee kupumzika.Naomi yupo utamuona tu" akasema muuguzi
" Nataka kumuona Naomi sasa hivi.Nataka nikamuone mke wangu" akasema genes huku akiishusha miguu yake chini ya kitanda na kujaribu kusimama akataka kuanguka.Wauguzi wakamdaka na kumlaza tena kitandani.Machozi yakaanza kumtoka baada ya kumbu kumbu zote kumrejea..
" Siamini kama Naomi ameathirika kama walivyosema.Naomi hawezi kuathirika.Ninamfahamu Naomi vizuri.Ninampenda Naomi na hata kama ameathirika lazima nimuoe tu.Kama ni kufa niko radhi nife naye.Yeye ndiye mwanamke pekee ninayemtaka maishani mwangu.Lazima nimuoe Naomi." akawaza Genes .
Baada ya saa mbili za mapumziko hali ya Genes ikawa nzuri na akaruhusiwa kurejea nyumbani.Akampigia simu Hamidu rafiki yake ambaye hufanya biashara ya taksi na kumuomba afike kumchukua pale hospitali.Bila kupoteza muda Hamidu akafika na kumchukua Genes.
" Genes nini kinakusumbua mbona uko hivyo leo ? akauliza Hamidu.Genes hakujibu kitu alikuwa ameinama akiwaza.Hakuongea kitu hadi walipofika nyumbani kwa Genes.Akamuomba Hamidu asiondoke amsubiri,akaingia ndani na kwenda kugonga mlango wa chumba cha Naomi lakini hamkuwa na dalili za kuwepo mtu.Akatoka na kumwambia Hamidu waondoke wakaelekea moja kwa moja nyumbani kwa kaka yake Naomi .Alifunguliwa geti na kuingia ndani.Kitu pekee alichokihitaji ni kuonana na Naomi.
" Genes nasikitika sana,Naomi amesema haitaji kuonana na mtu yeyote kwa sasa.Naomba tuheshimu maamuzi yake na tumuache kwanza apumzike na akili yake itulie ndipo mkae na muongee,lakini kwa sasa ninyi nyote mko katika taharuki na hamtaweza kuongea au kuamua kitu cha maana.Tulizeni akili zenu kwanza na baada ya hapo mtafanya mamuzi yenye busara na yenye faida kwenu nyote.Kwa sasa naomba tumuache Naomi aendelee kuwa peke yake" akashauri kaka yake naomi.
"Shemeji ninaomba uniruhusu hata dakika mbili tu walau nimuone Naomi.Nikiiona sura yake tu nitatulia." akaomba Genes.kaka yake Naomi akafikiri kisha akasema
" Ngoja kwanza nikamuulize kama atakuwa tayari kuonana nawe kwa sasa " Kaka yake Naomi akasema na kuinuka pale sebuleni na kwenda hadi katika mlango wa chumba cha Naomi.Genes naye akainuka na kuanza kumfuata kwa nyuma .
" Naomi akiwa amejifungia chumbani akasikia mlango wake ukigongwa.Kwa uchovu akainuka na kwenda kuufungua .Akakutana na kaka yake.
" Samahani Naomi,najua ulisema hutaki kuonana na mtu yeyote yule lakini Genes amekuja na anaomba japo akuone kwa dakika moja tu."
kauli ile ya kaka yake ikaamsha tena kilio kwa Naomi.
" kaka nimekwambia sitaki kuonana na mtu yeyote leo especially Genes.." akasema Naomi na kuufunga mlango.
" Naomi !! Ikasikika sauti kubwa ya Genes.Kaka yake Naomi akastuka.Hakujua kama Genes alikuwa akimfuata.
" Naomi naomba nionane nawe tafadhali..!! . akasema Genes akiwa ameuegemea mlango.
Muda ulizidi kwenda bila ya mlango kufunguliwa.Genes akakaa chini na kuuegemea mlango wa chumba cha Naomi.
" Nitakesha hapa mlangoni.Sintaondoka hadi nionane na Naomi" akasema Genes
" Sintaondoka hadi nionanane nawe Naomi.Ni wewe pekee ninayekuhitaji katika maisha yangu.Nitaishi nawe hivyo hivyo...."
Akasema Genes huku akilia.
Ndani ya chumba Naomi alikuwa akilia machozi kwa uchungu hasa baada ya kusikia sauti ya Genes akilia kwa kwikwi pale nje ya mlango wake.
" I love you Genes ..I love you so much but I cant be with you again." akasema Naomi kisha akafungua dirisha na kuruka nje.Taratibu akapanda geti na kushuka upande wa pili kisha akatokomea kizani.
NAOMI AMEKWENDA WAPI ? NINI HATIMA YAKE NA GENES ? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII KATIKA SEHEMU IJAYO.
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment