MASIMULIZI
Friday, April 11, 2014
SERENA SEHEMU YA 10
RIWAYA : SERENA
SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Jason…!!. Serena akasema huku akimwangalia Dr jason usoni lakini kabla hajasema chochote
simu ya Dr jason ikaita
“Excuse me” akasema Dr Jason huku akiitoa simu yake mfukoni.Akaangalia mpigaji akakuta ni Dr Anna Maria Kanyunyu daktari ambaye kwa usiku huu alikabidhiwa jukumu la kuangalia hali ya mzee Albano.
“Hallow Dr Anna” Akasema Dr Jason
“Dr Jason kuna matatizo yametokea hapa.Tafadhali njoo haraka sana hospitali hali ya mzee Albano imebadilika ghafla.Amegeuza macho na moyo wake unapiga kwa mbali sana.”
“Anna nini kimetokeaaa !!! .. Dr Jason akauliza kwa sauti kubwa.
“Dr Jason hata mimi sijui,nilipigiwa simu kuwa nina mgeni wangu nje ,kwa kuwa mgonjwa alikuwa akiendelea vizuri nikaamua kutoka kwenda kumuona huyo mgeni wangu.Nilipouliza mapokezi nikaambiwa kuwa hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akinitafuta.Nikarudi tena ndani
ndio nikakuta hali hii…wahi Dr Jason..” akasema Dr Anna huku akilia.
“My God” …..Dr Jason akasema.
ENDELEA………………………………..
“Ok ! Calm down Anna.Fanya hivi .Haraka sana nenda ofisini kwangu kabati ya juu kabisa.Codes ni 13862.Fungua halafu chukua Anxylophylis mchome mgonjwa.fanya haraka sana…Hii itasaidia kuyarudisha mapigo yake ya moyo katika hali yake ya kawaida kwa haraka.Mimi niko njiani nakuja sasa hivi..
Baada ya kumaliza kuongea na Dr Anna maria Dr Jason akamtazama Serena ambaye tayari uso wake ulikwisha onyesha wasi wasi.
“What happened Dr Jason” Serena akauliza
“Twende hospitali haraka sana.Hali ya mzee imebadilika ghafla.”
“What..!!!!!” Akauliza Serena.
“we don’t have much time.Lets go” Dr
Jason akaacha pesa mezani na kushuka ngazi huku wakikimbia.Watu mle hotelini wakawa wakiwashangaa
“Dr Jason tell me is my father alive? Akauliza Serena wakiwa katika gari ya Jason wakiingia bara bara kuu.Dr Jason hakujibu kitu.
“Tell me Jason….is he ok? Akauliza tena serena huku akilia.
“I don’t know” akajibu Dr Jason na kumfanya serena azidi kulia.
Dr Jason akanyoosha mkono na kumshika Serena bega akamwambia.
“Please Serena be strong.He’s going to be ok”
Mawazo mengi sana yakamsonga juu ya kilichotokea.Jioni wakati
anamkabidhi mgonjwa kwa Dr AnnaMaria mgonjwa
hali yake ilikuwa nzuri sasa kimetokea kitu gani?Akawaza Dr Jason bila kupata jibu.
Aliendesha gari kama kichaa kuwahi hospitali .Alichokuwa
akikihitaji ni kuwahi hospitali kuokoa maisha ya Mzee albano.
*
*
*
*
Geti la kuingilia Patrick Charles Memorial hospital lilikuwa wazi.Kwa kasi ya ajabu Dr Jason akaingia na kupaki gari kisha akashuka garini na kukimbia kwa kasi kuelekea ndani ya jengo.Serena naye alikuwa akimfuata nyuma huku akilia.
Sindano aliyomchoma Dr Anna ilifanya kazi kwa haraka na kwa muda mfupi hali ya mzee albano ilianza kuleta matumaini baada ya mitambo inayoonyesha mwenendo mzima
wa mfumo wa mwili kuonyesha kuwa mifumo ilikuwa imeanza kufanya kazi tena.
Haraka haraka Dr Jason akaingia chumbani mle na kukuta timu ya madaktari wakiwa wamekwisha fika.Alipoingia wakampisha.Akaenda katika mitambo na kuitazama kwa sekunde kadhaa kisha akasema.
“naomba Philiculose haraka” Dawa hii ikaletwa akamchoma mgonjwa.
Akaandika katika karatasi vipimo vinavyotakiwa kufanyika kwa haraka.Watu wa vipimo walikuwa tayari na kwa kasi ya ajabu wakachukua damu kwenda kupima.Dakika kama tano hivi majibu yakarudi.Dr Jason akayasoma majibu yale ,jasho likamtiririka.Akampa Dr Henry naye akasoma asiamini alichokisoma.
Damu ya mzee Albano ilikutwa na chembe chembe za sumu aina ya dischoschis.Sumu yenye uwezo wa kuua kwa masaa mawili tu.
“My God I cant believe this” Dr Jason akasema mwenyewe
“Dr Henry can we have a minute please”
Dr henry na Jason wakatoka na kuelekea katika kijichumba kidogo.
“Dr Henry something is going on.”Dr Jason akasema
“yah there is must be something going on Dr Jason.Lazima kuna mtu alimchoma mzee albano sindano ya sumu.But who and why??”
“Hata mimi najiuliza.Kwa sababu kwa mujibu wa maelezo ya Dk Anna ambaye alikabidhiwa mgonjwa usiku wa leo ,alipigiwa simu na mtu anayedai kuwa ni mgeni wake yuko getini.Alipotoka
hakumkuta huyo mgeni wake na ndipo hapo tukio lilipotokea.Inaonekana alidanganywa ili atoke na alipotoka tu mtu huyu akapata nafasi ya kufanya alilokusudia.Thanx God nilikumbuka kuwahi kumchoma ile sindano ya Anxylophylis iliyoweza kuiondoa sumu kwa haraka.Nilipopata taarifa toka kwa Anna nilihisi lazima itakuwa ni dawa zimezidi ambazo zimetengeneza sumu mwilini.Sikuhisi kama inaweza kuwa ni sumu ya namna hii.”
“Kwa sasa inabidi tufunge milango yote ya hospitali wakati polisi wanafanya uchunguzi wao.Hili limeshakuwa ni suala la kipolisi sasa.”Akasema Dr henry.
“Ndiyo.Inabidi kuwataarifu haraka sana polisi na vile vile ulinzi uimarishwe hapa hospitali na hasa katika chumba hiki cha mzee Albano”
Dr Jason akarudi haraka mle chumbani na kutazama tena maendeleo ya mgonjwa.Hali yake haikuwa ile mbaya ya kutisha.Dr Jason akapumua kwa nguvu ,akamshukuru Mungu kwa kuepusha tukio lile.Pamoja na hali ya mzee albano kuonyesha kuendelea vizuri bado moyo wake ulijaa wasi wasi mwingi kutokana na kilichotokea.
“Aliyefanya hivi alikusudia kitu gani? Ni wazi alihitaji kumuua mzee albano.But why?Kuna kitu gani kinachoendelea nyuma ya pazia?? Lazima kuna kitu kinachoendelea.I need to do whatever I can to protect him and make him alive.that’s what I promised Serena.”akawaza Dr Jason
Mlango ukafunguliwa alikuwa ni Dr Henry akiwa ameongozana na maafisa wa polisi ambao walikuwa wamevaa nguo maalumu za kuingilia katika chumba kile.
“Dr Jason hawa ni maafisa
wa polisi na wamekuja hapa ili kupata maelezo yatayowasaidia katika uchunguzi wao”
“Maafisa huyu ndiye daktari wetu bingwa Dr Jason.na yeye ndiye aliyekabidhiwa jukumu zima la kuhakikisha mzee albano anapata matibabu yenye kufaa.”
Baada ya utambulisho ule wakapata maelezo toka kwa Dr jason kuhusu sumu ile na jinsi inavyofanya kazi.
“Mchomaji aliichoma sumu hii katika pakiti hili la maji tulilokuwa tumemtundikia mgonjwa.Sumu hii ikawa ikiingia mwilini na kuchanganyika na damu.Tunashukuru sumu hii haikuwahi kuingia kwa wingi kwani baada tu ya kupata taarifa toka kwa Dr Anna nilimwambia asimamishe kila kitu kinachoingia mwilini kwa mgonjwa, halafu akamchoma sindano ya Anxylophylis inayoyeyusha sumu kali mwilini kwa haraka sana.”
Baada ya maelezo Dr Jason akakumbuka kuwa alikuwa amekuja na Serena.Akatoka mle chumbani akaingia katika kijichumba kidogo cha pembeni akainua simu.
“Hallow mapokezi yule binti wa Mzee albano yuko hapo?”
“Ndiyo yuko hapa pamoja na mama yake na ndugu zake wengine”
“Ok naomba niongee naye tafadhali”
Sekunde chache akasikia sauti ya Serena ailiyoonyesha wazi alikuwa akilia
“Hallow Jason tell me how’s my father?
“Mzee anaendelea vizuri,hayuko katika ile hali ya hatari tena.Tumewahi sana na kwa sasa anaendelea vizuri.”
“Ok thank you
so much
Jason for your help.” Akasema Serena
“Serena I promised that I’ll do whatever I can to make your
father alive.” Akasema Dr Jason na mara Dr Henry akaingia mle ofisini
“Ok tutaongea baadae…………”Dr Jason akakata simu.Dr henry alionekana akiheama na alikuwa na wasi wasi mwingi.
“Dr Jason kuna taarifa mbaya tumezipata sasa hivi”
“Taarifa zipi hizo dk Henry?
“Dr Selemani amefariki dunia dakika chache zilizopita kwa ajali ya gari”
“What !!?” akauliza Jason kwa mshangao
“That cant be.Dr Selemani huyu wa hospitali hii au unamsema Selemani yupi?
“Huyu huyu Selemani daktari wetu.Taarifa imekuja toka polisi sasa hivi.”
Dr jason akakaa kitini akihisi kuchanganyikiwa.Dr Selemani
ndiye daktari pekee wa dawa za usingizi aliyekuwa akimtegemea katika operesheni ya mzee Albano.
Kila mmoja mle chumbani akawa akiwaza lake.Mambo haya yalimchangaya sana Dr Jason.Wakiwa katika ukimya simu ya Dr Henry ikaita akipokea na kuongea kidogo kisha akamgeukia Dr Jason.
“Dr Jason tunatakiwa na polisi.Kuna mambo wanataka kutueleza.”
Wakatoka na kuelekea katika chumba kidogo ambacho polisi walikuwa wakikitumia kama ofisi yao ya uchunguzi.
“Dr henry na Dr Jason kuna mambo ambayo tunadhani ingefaa muyafahamu.Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wakati wa tukio kamera za ulinzi zinazochukua picha katika eneo
la kuzunguka chumba alimolazwa mzee albano zilikuwa zimezimwa.Hii inaonyesha kuwa mtekelezaji wa tukio hilo anahusika moja kwa moja na uzimaji wa kamera hizo.Picha toka kamera ya ulinzi katika lango la kuingilia hospitali hii haikuzimwa inamuonyesha Dr Selemani kuwa aliingia hapa dakika tatu kabla ya tukio kutokea na kuondoka dakika mbili baada ya tukio.Dakika kumi na tano baadae tunapata taarifa kuwa amefariki kwa ajali ya gari.Kuna kila sababu ya kumuunganisha Dr Selemani na tukio hili.Ingawa bado uchunguzi rasmi haujathibitisha lakini kuna kila dalili kuwa matukio haya yanafungamana.Hizo ni ripoti za awali ambazo tumeona ni bora mkafahamu ili kuchukua hatua zinazofaa.Kwa sasa tunamshikilia kijana aliyekuwapo katika chumba cha mitambo ya kamera wakati tukio linaendelea kwa maelezo zaidi.Tutazidi kuwafahamisha kadiri tunavyopata taarifa nyingine za kiuchunguzi.”
Dr Jason alikuwa akitiririka jasho.Taarifa ile ikamuogopesha sana.Uhai wa mzee Albano ulikuwa mashakani..
“Dr Henry “ akasema Jason wakati wakiwa ofisini kwa henry.
“Kuna kitu cha hatari kinaendelea hapa.Japokuwa uchunguzi bado haujathibitisha lakini nina kila sababu ya kuamini kuwa Dr Selemani ndiye ama alishiriki katika zoezi la kumchoma Mzee Albano sindano ya sumu kwa lengo la kumuua kabisa.Angalia mtiririko wa matukio.Dakika chache kabla ya tukio ameonekana akiingia hapa.Muda mchache baadae tukio linatokea naDr Selemani anaondoka.Huoni kuna kila sababu ya kumuhusisha na tukio hili?Isitoshe ni kwamba hakukuwa na upasuaji wowote usiku wa leo kwa hiyo Dr Selemeni alikuja kufuata nini wakati hayuko katika ratiba ya kuingia kazini usiku ? Dr Henry Maisha ya mzee Albano yako hatarini
na tusipokuwa makini basi anaweza kuuawa muda wowote.Nina imani hata hiyo ajali inayosemekana kutokea iliyosababisha kifo cha Dr Selemeni si ajali ya kawaida.Ni lazima itakuwa imepangwa kitaalamu sana ili kupoteza ushahidi.We have to do something urgent” Akasema Dr Jason kwa wasiwasi mkubwa.
“Unashauri tufanye nini Dr Jason?
Akauliza
Dr Henry
“Let me think what we can do..”
Jason akatoka na kuelekea katika chumba cha mgonjwa.Akahakikisha kila kitu kiko safi na mgonjwa anaendelea vizuri.Akaingia katika kichumba kidogo cha pembeni akakaa akitafakari.
“I must save him.I promised Serena that I’ll save her father.”
*
*
*
*
Ni mtu mmoja tu ambaye alikosekana katika kikao hiki cha dharura naye ni mheshimiwa mbunge Stella Kamutere.Hakuwa ametaarifiwa juu ya kikao hiki cha ghafla kilichoitishwa na baba yake Mr Kamutere.Chumba walichokuwamo kilikuwa kimya kana kwamba hakuna watu.Hakuna aliyekuwa akiongea kila mmoja alikuwa akitafakari la kwake.Nyuso zao zilionyesha kuvuja jasho licha ya hali ya ubaridi kutawala katika chumba kile.
“Jamani ,tumelazimika kuitana tena hapa kwa dharura kutokana na hali ya mambo jinsi inavyokwenda” Akafungua kikao kile Mr Kamutere.
“Kama tulivyokuwa tumeazimia wakati wa kikao chetu cha asubuhi,kila kitu kilifanyika kama tulivyokuwa tumepanga .Mr Kumzaya alifanikiwa kuonana na Dr Selemani wakaongea na akakubali kuifanya kazi ile.Alifanikiwa kuifanya ile kazi lakini dakika za mwisho kuna uzembe mdogo ulifanyika na hivyo nasikitika kuwaambia kuwa mpaka sasa Mzee Albano yuko hai na anaendelea vizuri.Taarifa toka vyanzo vyetu vya ndani ya hospitali ile inasema kuwa Dr Jason aliwahi kutaarifiwa juu ya hali ya mgonjwa kubadilika ghafla na akawahi hospitali kuokoa maisha ya mzee Albano.This guy is so smart.Kama tulivyokuwa tumepanga baada ya kufanya kazi tuliyokuwa tumemtuma,vijana wetu walifanya kazi yao vyema sana na nafurahi kuwaaambia kuwa Daktari aliyefanya kazi ile Dr Selemani tayari amekwisha zimwa katika ajali ambayo haina utata wowote.Kwa hilo wala msiwe na shaka yoyote.Nilichowaitia hapa usiku huu ni kujadili tena kwa haraka jinsi gani tufanye ili tuweze kufanikisha suala hili kwa haraka sana.Kwa
kadiri tunavyochelewa ndivyo zoezi linavyozidi kuwa gumu na kuna kila dalili kwamba daktari huyu Dr Jason atamfanyia upasuaji mzee Albano na uwezekano wa kupona ni mkubwa sana”
Akanyamaza
na kuwatazama tena wajumbe waliokuwa kimya wakimsikiliza kwa makini.
“Ndugu zangu ,safari hii tunatupa karata yetu
ya tena.Tunataka mpaka kufika kesho jioni mzee Albano awe amekufa.Kitu cha kwanza ninachokitaka kufahamu ni nani watakaofanya operesheni ile.Nina maana ni madaktari gani watakaoshirikiana na Dr Jason katika operesheni hiyo.Nataka mpaka kesho mchana niwe nimepata taarifa hiyo.Taarifa hiyo nataka iwe na siku kamili na muda ambao operesheni hiyo itafanyika.Tukisha fahamu ni akina nani basi tunaweza kujua kwa haraka nini tufanye.Vile vile mpaka sasa hivi tayari tuna uhakika kuwa operesheni hiyo itaongozwa na Dr Jason ambaye kwa bahati mbaya naweza sema ni mchumba wa mwanangu Stella na hiyo ndiyo sababu hamjamuona katika kikao hiki.Sikutaka kumtaarifu kuhusu kikao hiki kwa sababu hangeweza kukubali iwapo lingetokea azimio la kumuondoa Dr Jason duniani.Kwa hatua tuliyofikia ni hatua ambayo ni lazima tufanye maamuzi magumu ili tuwe na uhakika na maisha yetu.Endapo mtu yeyote ataonekana kuwa ni kikwazo kwetu basi hatuna budi kumdhibiti haraka sana.Kwa taarifa yenu ni kwamba endapo mpaka kesho saa sita mchana hatutakuwa tumepata
ufumbuzi basi hatutakuwa na jinsi zaidi ya kumuua Dr Jason ambaye ndiye tegemeo kubwa katika operesheni hii.No Jason no operation ,that means Mr Albano must die.”
Mr Kamutere akatulia akawaangalia wajumbe wote kwa macho makali.Nyuso za baadhi ya wajumbe hawa zilionyesha wasiwasi mwingi.
“Ndugu mwenyekiti nina wazo” Akasimama Mr Ezekiel kumzaya
“Ndugu mwenyekiti pamoja na kwamba Dr Jason ni moja kati ya kikwazo kikubwa sana kwetu ,lakini siafiki suala la kumuua kwa sasa.Ikumbukwe kuwa leo hii limefanyika jaribio la kumuua mzee Albano na tayari suala hili kwa sasa liko mikononi mwa polisi.Papo hapo Dr Selemani ambaye kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani toka jeshi la polisi ,tayari anashukiwa kuhusika na jaribio lile lililoshindwa la kumuua Mzee Albano.Ikiwa na Dr Jason naye atauawa,lazima kutazuka taharuki na kuzua maswali mengi yatakayopelekea uchunguzi wa kina ufanywe na mwisho wa siku tutaishia kukamatwa.Mkumbuke pia kuwa ugonjwa wa mzee Albano unatazamwa kwa jicho la karibu sana na serikali na ni serikali ndio walioagiza Mzee albano apelekwe pale Patrick Charles
memorial hospital.Iwapo kutatokea tatizo lolote lile litakaloleta udadisi basi serikali haitasita kutumia nguvu zake zote katika kupata majibu na mkono wa serikali siku zote ni mrefu na haishindwi kitu.Mzee Albano amekuwa ni mmoja kati ya watu wenye heshima ya kipekee sana katika jamii ya watanzania.Hebu jengeni picha siku moja tunaonyeshwa kuwa ni sisi ndio tumemuua mzee Albano
nini kitatokea.? Nadhani wananchi watatamani watumalize wenyewe kwa mawe.Ili kuepuka aibu na fedheha ya namna hiyo inatubidi tufanye mambo kwa umakini mkubwa sana hasa kwa sasa ambapo jaribio la kwanza limeshindikana.Ninachopendekeza mimi suala la kumuua Dr Jason liwe la mwisho kabisa iwapo kutaonekana hakuna tena jinsi nyingine ya kufanya.Daktari mkuu pale Patrick Charles
memorial hospital Dr Henry ni rafiki yangu wa siku nyingi.Tulikutana Uingereza wakati tukisoma.Hebu nipeni muda mpaka kesho saa nne asubuhi niweze kuongea naye .Nataka niongee naye kwa nafasi na utulivu mkubwa na kwa jinsi tunavyofahamiana najua hawezi kukataa.Nataka kupandikiza mtu wetu katika operesheni hiyo.Kwa sasa hawana mtu wa dawa za usingizi baada ya daktari tegemeo Dr Selemani kufariki dunia.Dr Henry ataitumia nafasi hiyo kupandikiza mtu wetu pale na huyo ndiye atakayefanya kazi yote na Mzee Albano hataamka milele.Atakuwa
ameenda na siri yake moyoni..Sijui mnaonaje mpango huu?
Nuru ya matumaini ikarejea tena katika nyuso za wajumbe na kwa mbali walionekana wakitabasamu.
“Mpango huu ni mzuri sana Mr Kumzaya”
Akasemammoja wa wajumbe wa kikao kile
“Ila nina swali kwa Mr kumzaya.Itakuwaje iwapo huyo rafikiyo Dr Henry atakataa kushirikiana nasi?
Mr Kamutere akataka kumjibu lakini Dr Kumzaya akamfanyia ishara kuwa aache yeye atamjibu.
“Katika dunia ya sasa hakuna kitu kinachoongea zaidi ya pesa.We have lots of billions ambazo hatutaki zipotee iwapo mzee Albano ataamka.We have money and we must use them.Hakuna upungufu wowote ule tutakaoupata iwapo tutatumia one billion or two out of billions we have .Naomba mniamini ndugu zanguni kuwa Dr Henry ni lazima
akubali .Naomba mniamini kwa hilo.”
Mr Kamutere akakohoa kidogo kisha akajibu.
“Tunakuamini sana Mr Kumzaya.Ulifanya kazi kumshawishi Dr Selemani kutufanyia kazi
ingawa ilishindikana katika hatua za mwishoni.Mimi binafsi nakuamini sana na nina uhakika kazi hii utaifanya vizuri.Ndugu zanguni naomba tumpe fursa hii Mr Kumzaya ili aweze kushughulikia suala hili.”
Mr Avinash Patel Akasimama na kuuliza.
“Nimekuelewa ndugu mwenyekiti ,ila kuna kitu nataka kufahamu.Mr Kumzaya amezungumzia juu ya kupandikizwa kwa daktari wetu.Nataka kumfahamu daktari huyo ni nani na ana uwezo gani kiasi cha kutokutiliwa shaka siku za usoni..”
Mr
Kumzaya akatabasamu kisha akasimama na kujibu.
“Mr Avinash tunapokuwa na mtandao kama huu,si kwamba sisi tuliopo hapa ndio tunaoweza kufanya kila kitu na si kwamba kila aliyeko katika mtandao huu ni lazima afahamike.Wapo watu wengine wengi na wazito ambao hawatakiwi kujulikana kabisa kama wanashirikiana nasi.Linapotokea suala linalotuhusu kila mmoja hufanya kazi hiyo katika sehemu yake.Kwa hiyo Mr Patel
usistuke.Tunao madaktari wa kutumainiwa wanaoweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi katika mazingira yoyote na wakati wowote.Ila naomba nisiwataje kwa majina wala wanatoka katika hospitali zipi hapa nchini kwa sasa.Naomba tu muelewe kuwa
wapo na wako tayari kufanya kazo yoyote tutakayowapa”
Kila mmoja mle chumbani akaridhika na majibu ya yaliyotolewa.Maelekezo machache yakatolewa na Mr Kamutere kisha kikao kikafungwa kwa makubaliano ya kukutana kesho saa sita mchana.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………….
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment