Wednesday, April 16, 2014

SERENA SEHEMU YA 14







            “Serena alikuwa wazi huu ni muujiza mkubwa.Mtu ambaye nilikuwa namuota usiku na mchana ,leo nimelala naye hoteli moja. I real love this girl.Pamoja na kwamba niko katika mahusiano na Stella kwa sasa lakini Serena siku zote amekuwa kichwani mwangu toka siku ile ya kwanza nilipomuona kule Mbeya.Japokuwa kuna kipindi niliamua kumsahau na kuendelea na maisha yangu na nikaufungua moyo wangu kwa Stella ,lakini bado nimejikuta kuna kitu nakikosa toka kwa Stella.Kuna kitu maalum  ambacho anacho Serena pekee.Hiyo ndo sababu kwa nini nimekuwa namuwaza Serena usiku na mchana.Hii ni vita na ambayo ninajua ni ngumu kupita maelezo ,lakini nina imani nitashinda.Mpaka sasa maendeleo si mabaya.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuhakikisha mzee Albano anapona,kitu ambacho nimekwisha muhakikishia Serena kuwa kinawezekana.Baada ya mzee wake kupona furaha ya Serena itarudi tena na hapo ndipo tutakuwa na nafasi pana na uwanja mpana zaidi wa kuongea mambo mengi.Kuna kitu kimekuwa kikiniumiza kichwa sana tangu tukio la jioni ya leo.Nimetokea kutomwamini mtu yeyote yule.Kilichofanyika jioni ya leo kwa mzee Albano kimenifundisha kitu kikubwa sana.I must do something.Nina imani nitakachokifanya kitakuwa msaada mkubwa kwa mzee Albano.Ninachofikiria kukifanya ni hatari kubwa ila Mungu atakuwa upande wangu .Kwa ajili ya Serena nitafanya kitu chochote kile.…..”Dr Jason akawaza huku ameshika kichwa chake.Akamalizia maji yaliyokuwa katika glasi halafu akachukua kijitabu chake kidogo cha kumbukumbu ambacho amehifadhi kumbukumbu zake muhimu.Akachukua kipochi chake kidogo cha mfukoni akakifungua na kutoa laini ya simu.Hii ni laini ya simu ambayo huwa anaitumia kwa nyakati kama hizi au akiwa na mambo mengine muhimu akaichomeka katika simu yake...Akaandika namba toka katika kile kijitabu akapiga.




0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi