MASIMULIZI
Saturday, April 12, 2014
BEFORE I DIE SEHEMU YA 11
RIWAYA: BEFORE I DIE
SEHEMU YA 11
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Leo nimegundua kitu ambacho sikuwa nimekigundua hapo awali.Marina ana uzuri wa asili uliojificha .Mtoto yule ni mzuri.Kuna kitu nimekiona katika macho yake ambacho kimenisisimua mwili wangu wote.Sielewi kama niko sahihi kwa hisia zangu lakini nahisi hisia zangu ziko sahihi.There is a connection between us.Kuna nguvu inayonivuta kuwa karibu na Marina.” Innocent akawaza halafu akainuka na kusimama
huku mikono yake imeshikilia kiti
“No ! No No Innocent you are wrong.Marina isn’t the one”” Innocent akasema kwa sauti ndogo huku akizunguka zunguka mle ofisini.Akaenda na kusimama dirishani.
“ A woman of my deams must be simple,educated,full of love,…and…..” Innocent akawaza akahisi kama kichwa kikimuuma.
“marina is a simple girl,asiyekuwa na elimu but I can see something in her eyez..I can see passion..I can see love..Kama akibadilika anaweza akanifaa.” Mawazo ya innocent yakakatizwa na simu ya mezani iliyolia mle ofisini.
ENDELEA……………………
Saa kumi na mbili za jioni Innocent akamaliza kazi ,yeye na Marina wakaelekea nyumbani kwao.Tayari giza lilikwisha tanda walipowasili nyumbani.Akiwa ametangulia mbele na Marina akimfuata nyuma Inno akafungua mlango wa sebuleni na kukutana na sura ya mama yake iliyostuka ghafla baada ya kumuona Marina akiwa nyuma ya Inno.
“Inno ukitaka tuelewane leo ,mtoe huyo kahaba ndani mwangu.” Mama Innocent akainuika na kusema kwa hasira
“Mama tafadhali……..” Inno akajaribu kuongea lakini akakatishwa na sauti ya juu iliyojaa ukali ya mama yake.
“Nakwambia Innocent kama unataka tuelewane leo muondoe huyo kahaba wako haraka sana.Sitaki kumuona ndani ya nyumba yangu.Innocent umekuwaje siku hizi? Sikutegemea kama iko siku utakuja kuwa na uhusiano na watu kama hawa.” Mama yake akafoka
“mama tafadhali naomba unisikilize japo kidogo” Innocent akasema
“Inno nimekwisha sema kwamba kahaba huyu halali humu ndani leo.Kama huamini leo ndiyo atanitambua..” Mama Innocent kwa hasira akamsukuma Inno akaanguka pembeni halafu akamvaa Marina akamsukuma nje akaanguka chini na kutoa ukelele wa maumivu.
“Nimekwambia toka asubuhi kwamba sitaki nikuone ukiwa na mwanangu.Unachomfuata fuata mwanangu ni kitu gani wewe kahaba? “ mama Innocent akasema kwa hasira huku akimvuta Marina mkono ili kumtoa nje.Innocent alikiona kitendo kile kikamuumiza sana.Kwa nguvu akamvuta mama yake akamwachia Marina.
“Mama imetosha.Siwezi tena kuvumilia matukano na manyanyaso kama haya kwa binti masikini kama huyu.Sitaki kusema lolote mama ila naomba uelewe kwamba kwa vile hutaki Marina akae hapa basi na mimi naondoka.” Innocent akasema huku akihema kwa hasira.Akamfuata Marina pale chini alipokuwa amelala akamwambia
“Marina nyamaza kulia.Nisubiri nikachukue baadhi ya vitu vyangu tunaondoka wote” Marina hakujibu kitu alikuwa akilia kwa maumivu.Innocent akaenda chumbani kwake akachukua begi lake na kupakia baadhi ya vitu vyake muhimu kama nguo na baadhi ya nyaraka za kiofisi ,mara Sabrina akaingia
“Kaka Innocent ni kweli unaondoka? Sabrina akauliza huku akitokwa na machozi
“Sabrina nimeamua niondoke.Nimechoka na vituko vya mama yangu.”
Huku akilia Sabrina akauliza
“sasa Innocent usiku huu unaenda kulala wapi?
“Sabrina sijajua bado lakini nitalala sehemu yoyote ile.Mimi mtoto wa kiume siwezi kushindwa maisha” Innocent akasema huku akimalizia kufunga zipu za begi lile kubwa
“Innocent kama unaondoka basi hata sisi tunaondoka.Siwezi kuendelea kuishi hapa kama wewe haupo.Wewe ndiye uliyekuwa mtetezi wetu.kama wewe haupo hakuna mtu mwingine atakayetujali” Sabrina akasema kwa hisia kali
“Sabrina tafadhali msiondoke hapa nyumbani.wewe na Grace ni sehemu ya familia hii .Subirini kwanza nirekebishe sehemu ya makaazi halafu nitawachukua tukaishi wote.” Innocent akasema huku akimpiga piga Sabrina mgongoni.
“Kaka Innocent suala la mahala pa kukaa halina taabu.Nimechelewa kukutaarifu kwamba nimepata kazi katika taasisi moja isiyo ya kiserikali inayoshughulika na kuwasaidia wanawake wenye kansa na matatizo mbali mbali .Dada Latoya ambaye ndiye mwenye taasisi hiyo ameniahidi kunipatia nyumba ya kuishi .Nitakupigia simu nikutaarifu zaidi.” Grace akasema huku akilibeba begi la Innocent wakatoka mle chumbani.Innocent akastuka kidogo na kumuangalia Sabrina
“ Unasema Latoya?
“ ndiyo Latoya.Unamfahamu?
“ Latoya huyu bilionea? Akauliza Innocent
“ Sifahamu kama ndiye
huyo Latoya bilionea unayemsema lakini yeey ana taasisi ya kusaidia walemavu na watu watu wenye matatizo mbali mbali.Umewahi kumuona?
“ Hapana sijaahi kumuona lakini nimewahi kusikia kwamba kuna bilionea mkubwa wa Kitanzani anaitwa Latoya anyway hongera sana kwa kufanikiwa kupata kazi.Tafadhali nipigie simu kesho ili tuongee kwa undani zaidi.Kwa sasa bado nina hasira sana” Innocent akasema .Walipotokeza sebuleni mama yake Innocent bado alikuwa amesimama amefura kwa hasira Wakatazamana usoni kwa sekunde kadhaa halafu Inno akasema
“Mama mimi naondoka.Nitatafuta mahala pengine pa kuishi .Siwezi kuvumilia kumuona Marina akiteseka na kunyanyaswa.Laiti ungejua matatizo makubwa aliyonayo binti huyu usingethubutu kumtolea maneno makali kama uliyomtolea.Nitamtuma dereva kuja kumalizia vitu vyangu vilivyobakia kesho.” Innocent akamuaga mama yake.Akamuinua Marina ambaye alikuwa akigugumia kwa maumivu makali na kwa kusaidiana na Grace na Sabrina wakampakia katika gari ,akaliwasha na kuondoka huku kila mmoja akiwa haamini kama ni kweli Innocent alichukua maamuzi ya kuondoka nyumbani kwao.Mpaka taa za gari zinafutika machoni pake bado mama yake aliendelea kusimama pale nje akiwa na hasira zisizomithilika.
Innocent akageuka na kumtazama Marina aliyekuwa amekaa kiti cha pembeni.Alikuwa akigugumia kwa maumivu.
“Unajisikiaje Marina?
akauliza
“Nasikia maumivu makali sana tumboni” Marina akasema kwa sauti yenye kuonyesha ni wazi alikuwa akisikia maumivu makali mno
“Kesho nitakupeleka hospitali ili ukaanze matibabu.” Akasema Innocent.
“nashukuru sana Innocent kwa msaada wako.lakini Inno hukupaswa kuondoka nyumbani kwenu kwa ajili yangu.Ungeniacha mimi nirudi nikaendelee kuishi kule ninakoishi” marina akasema
“Marina nimechoshwa na vitendo vya unyanyasaji vinavyofanyika katika ile nyumba.Mungu ametujalia uwezo lakini isiwe ni sababu ya kuwanyanyasa wale wasiokuwa na uwezo.Kitendo cha leo alichokifanya mama kimeniumiza mno…” Innocent akasema na kuongeza mwendo wa gari.
“Bado sijapata jibu kwa nini mama amfanyie Marina namna ile.Kama mama alipaswa kumuhurumia na kumpokea .Alipaswa kuonyesha ile huruma ya kimama.Bila ya kutambua kwamba Marina ni mgonjwa amemsukuma na kumsababishia maumivu makubwa.Siku zote nimemvumilia lakini leo mama ameniumiza kupita kiasi.” Innocent akawaza huku moyoni bado akiwa na hasira kila akikumbuka kitendo kile
“Usiku huu itanibidi nitafuate mahala nikalale.Marina anahitaji kupumzika na kesho asubuhi nimpeleke hospitali.Kesho ndipo nitapanga vizuri nini kifuate baada ya hatua hii ya kuondoka nyumbani.Nitahitaji kupata mahala pa kuishi lakini isiwe ni sehemu inayohusiana na familia yangu.Familia yangu imejaa watu wasio hata na chembe ya ubinadamu.Nitatafuta nyumba ya kupanga na kuwachukua Sabrina na Grace na kuishi nao kwani najua baada ya mimi kuondoka pale nyumbani maisha yao yatakuwa magumu sana”
Usiku huu hakuwa na mahala pengine alipokuwa akipaamini zaidi ya 104 lodge.Ni hoteli tulivu mno na ya kupendeza.Ni katika hoteli hii ndipo Inno alimleta Marina siku ya kwanza walipoonana.Pale hotelini wakapewa chumba na wahudumu wakawasaidia kubeba mabegi ya Inno hadi chumbani.
“Marina utakula chakula gani usiku huu” Inno akamuuliza Marina aliyekuwa amekaa sofani
“Sijisikii kula chakula chochote Inno”
“hapana Marina unapaswa ule chakula ili mwili uwe na nguvu.” Inno akasema akaiendea simu na kuagiza waletewe chakula chumbani kwao.
Haikuchukua muda chakula kikaletwa na kuwekwa mezani.Inno akambembeleza Marina ajitahidi kula japo kidogo.Marina akala kijiko cha kwanza na cha pili akashindwa kuendelea zaidi.Inno akamsogelea karibu akakishika kijiko chake na kuchota chakula.
“marina tafadhali naomba jitahidi kula.Chakula hiki ndicho kitakupa nguvu “ Inno akasema huku akimuangalia Marina ambaye pamoja na maumivu aliyoyasikia akatabasamu na kufungua mdomo Innocent akamlisha chakula.
“Jitahidi karibu unamaliza” Inno akaendelea kumbembeleza hadi alipomaliza sahani nzima
“ Safi sana.Sasa unaweza kupanda kitandani kupumzika.Mimi nitalala hapa katika sofa” Innocent akamwambia Marina .Marina akamtazama Inno usoni kwa sekunde kadhaa na kusema
“Inno nashukuru sana “
“Usijali Marina.” Akasema Inno na kumsaidia Marina kuinuka pale sofani na kumpeleka kitandani akamlaza na kumfunika shuka.
“Pumzika Marina ,kesho nitakupeleka hospitali na kisha nitashughulikia suala la wapi tutakwenda kuishi.Siwezi kukuruhusu urejee tena kule ulikokuwa ukiishi”
Marina hakujibu kitu ,aliendelea kumtazama Inno usoni ambaye aligeuka na kwenda kuketi sofani .Alionekana mwingi wa mawazo.
Pale sofani Inno alikuwa ameinama akijaribu kufikiri juu ya mambo kadhaa ambayo anahitaji kuyafanya.Mara akasikia sauti ya Marina ikimuita.Akainuka pale sofani na kumfuata Marina kitandani
“Innocent naomba kukuuliza”
“Uliza Marina “
“Ni kwa nini unanifanyia mambo yote haya? Najaribu kuwaza lakini sipati jibu .Inawezakanaje mtu ambaye sina undugu naye wowote,sina urafiki naye wowote,na kikubwa zaidi mtu kutoka katika familia ya kitajiri anifanyie mambo kama haya mimi masikini ninayefanya biashara ya kujiuza?.Hebu niweke wazi Innocent ni kwa nini umejitolea kunifanyia mambo yote haya hadi ukaamua kuliacha jumba lenu la kifahari kwa sababu yangu? Marina alisema huku akilia.Innocent akamtazama,akasikia uchungu moyoni.Akainama na kumfuta machozi
“Usilie Marina.Nimefanya haya yote kwa sababu ninapaswa kufanya hivi” Inno akajibu kwa ufupi.
“Innocent bado hujajibu swali langu.Nataka kufahamu sababu ya wewe kunifanyia mambo haya yote.Kila siku umekuwa ukipoteza muda mwingi na kuacha kazi zako ili kunishughulikia mimi.”
Innocent akatafakari ajibu nini.Akamtazama Marina aliyekuwa akisubiri apewe jibu
“Marina mimi ndivyo nilivyo.Huwa ninaumia sana kila nimuonapo binadamu mwenzangu akiteseka hivyo kama uwezo unaniruhusu kwa wakati huo,lazima nimsaidie.”
“nakubali Innocent una roho nzuri lakini kwa nini uamue kunichagua mimi ? Marina akauliza
“Marina nafikiri hayo ni maongozi ya Mungu.Hata mimi sifahamu ni kwa nini macho yangu yalikuona wewe tu na si mwingine.Pumzika Marina tutaongea zaidi kesho”Akasema Innocent na kugeuka akaanza kupiga hatua kurejea katika sofa.Marina akamuita tena,Inno akageuka
“Innocent unaniogopa?
Huku akitabasamu Innocent akajibu
“kwa nini nikuogope Marina”
“Siwezi kujua ,lakini ninaona kama bado unaniogopa .Innocent nakubali nimeishi maisha mabaya sana lakini kwa sasa sitaki tena kuishi maisha ya namna ile.Nataka kubadilika.Naomba usiniogope tena Innocent.Nisaidie niweze kuanza maisha mapya” Marina akasema na kumfanya Innocent acheke kicheko kidogo
“Marina nafurahi sana kusikia kwamba uko tayari kubadilika.Nakuahidi nitafanya kila niwezalo ili kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha mazuri na yenye furaha.”
“Nashukuru sana Innocent.Sijawahi kukutana na binadamu mwenye roho nzuri kama ya kwako.” Marina akasema .Innocent akarudi na kuketi sofani.
TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO………..
KWA SIMULIZI ZAIDI TEMBELEA HAPA MASIMULIZI
0 comments:
Post a Comment
Followers
MAHABA
SERENA
BEFORE I DIE
I DIED TO SAVE PRESIDENT
FAIDIKA NA MASIMULIZI
DEATH MESSENGER
CHOMBEZO ZA MASIMULIZI
MISS TANZANIA PART 2
Blog Archieves
April 2014
(57)
About Me
pettysean.blogspot.com
View my complete profile
Total Pageviews
BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU
Powered By
masimulizi
0 comments:
Post a Comment