Tuesday, April 15, 2014

TEN CHAPTERS SEHEMU YA 13




ninajitahidikuisahau bila mafanikio.Nina historia ndefu  naambayo sintawza kukuelezea katikabarua hii .Ninachotakaufahamu tu ni kwamba kuna mambo mengi ambayo huyafahamu kuhsu mimi na moja wapo ambalo nataa kuungaa kwako ni  kuhus yule kaka  niliyekufahamisha kwamba ni kaka yangu wa kuzaliwa naye si kweli hata kidogo .Yule aliwah kuwa mpenzi wangu lakini ili kuyaficha mahusianoyetu  ilitulazimu kuigza kama kaa na dada.




      “ Nilikutana na Naomi katika ndege,wote tukitokea Ufaransa.Tulizoeana haraka sana na nikajikuta nikivutiwa naye na kumtongoza.Alinikubalia na tukaja wote hadi Arusha .Wakati huo alijitambulisha kwangu kama Linah.Nilikaa naye hotelini kwa zaidi ya wiki mbili ndipo aliponieleza kwamba amepapenda sana Arusha na angetaka ahamishie maisha yake hapa.Aliniomba vile vile nimsaidie ili aweze kupata vitambulisho vipya vyenye jina la Naomi.Nilimuuliza sababu akasema anataka kuyasahau maisha yake ya nyuma pamoja na jina lake la Linah.Hakupenda nimuulize zaidi kuhusiana na maisha yake ya nyuma.Kwa kuwa nilikuwa nimetokea kumpenda sana nilimsaidia akapata kila alichokuwa akikihitaji na hatimaye akaanza maisha mapya hapa Arusha kwa jina la Naomi.Mke wangu aliporejea toka masomoni Ulaya ndipo mimi na Naomi tukaanza mahusiano ya kaka na dada ili mke wangu asije kustuka.Tumeendelea na mahusiano hayo ya siri hadi hivi sasa na kila mtu anajua kwamba Naomi ni mdogo wangu.Kuhusu maisha yake ni kwamba mpaka leo hi sifahamu ametokea wapi,ndugu zake ni akina nani na maisha yake ya nyuma yakoje.Ni msichana msiri sana kuhusiana na maisha yake na hata mara moja hajawahi kunitamkia loote kuhusiana na maisha yake na sikuwahi kumuuliza hata mara moja.Kuna nyakati alikuwa akiwasiliana na mtu Fulani na nilipoonyesha wasi wasi kwamba yawezekana akawa ni mwanaume mwingine akaniambia kwamba huyo alikuwa ni mdogo wake lakini hakuniambia huyo mdogo wake anahsi wapi.Genes hayo ndiyo ninayoyafahamu kuhusina na Naomi” Akasema Samweli.Genes akahisi kuishiwa nguvu akaenda kuketi sofani.





0 comments:

Post a Comment

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi