Thursday, April 3, 2014

" BEFORE I DIE" SEHEMU YA 3





lakini yawezekana pia ukawa haujaathirika.Kama itakuwa hivyo tutaimba kwa furaha na kumtolea Mungu sadaka na utayaanza maisha mapya.Je uko tayari kwenda kupima na kuhakiki afya yako kesho?






            “Nashukuru sana kwa makaribisho yenu mazuri ,nimejiskia faraja sana.Kwa kuwa nitakuwa nanyi kwa kipindi kirefu tutazidi kuongea na kufahamiana zaidi lakini kwa asubuhi hii ningeomba niseme machache.Kwa mujibu wa maelezo ya awali niliyoyapata toka kwa kaimu meneja mzee Ernest ni kwamba kwa siku za hivi karibuni kampuni yetu imekuwa haifanyi vizuri.Mauzo yamepungua na hivyo kupunguza kasi ya uzalishaji.Hii ni changamoto yangu ya kwanza kuishughulikia.Si changamoto ya kwangu tu bali ni yetu sote sisi kama wafanyakazi.Japokuwa kampuni hii inamilikiwa na mzee Benard lakini wadau wakubwa ni nyinyi wafanyakazi.Kwa umoja wenu mnaweza mkaipandisha kampuni au mkaishusha na kuiua kabisa.Ndugu wafanyakazi nataka tuanze upya ili kwa pamoja tuweze kupambana na hii changamoto kubwa ya kushuka kwa uzalishaji na mauzo.Nataka kila mmoja mahala pake pa kazi aone kwamba yeye ni sehemu ya kampuni na hivyo jukumu zima la uzalishaji ni la kwake.Nataka sote kwa pamoja tuwe na ari mpya ya kufanya kazi kwa bidii ,maarifa na ushirikiano.Ni silaha hii tu ya ushirikiano ndiyo itakayotuweka juu katika soko hili la ushindani mkubwa.Kwa kuwa kampuni hii ni yetu sote nawaahidi iwapo tutafanya kazi kwa bidii na kuogeza uzalishaji na mauzo,mishara yetu itapanda na kuboresha zaidi hali za maisha yetu kwani wote hapa tunafanya kazi kwa ajili ya kuwa na maisha mazuri ikiwa ni pamoja na kuwasomesha watoto wetu wapate elimu bora.Yote haya yanawezekana kama tutajituma katika kazi .Naamini yote yanawezekana kama kila mmoja atatimiza wajibu wake.Mwisho kwa kumalizia napenda kuwataarifu kwamba ofisi yangu iko wazi kwa mtu yeyote mwenye shida au matatizo mbali mbali.Nitapokea vile vile ushauri toka kwa kila mtu anayetaka kunipa ushauri ni jinsi gani tutaweza kuipeleka mbele kampuni yetu..Mwisho kabisa nawahakikishia kwamba pamoja kwamba kampuni yetu inapitia kipindi kigumu kwa sasa lakini hakuna mfanyajkazi hata moja atakayepoteza ajira yake.Ahsanteni sana kwa kuniskiliza.”






1 comment:

  1. mama mkatili sana huyo hata kumpongeza

    ReplyDelete

Followers

 

BONYEZA "LIKE" NA UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA KWA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

Powered By masimulizi