“Dr Jason ,sina neno la
kukushukuru kwa wema na juhudi zako za kumjali baba yangu.Toka ameletwa
hospitalini kwenu umekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa anapona na kuwa
mzima tena.Kwa sasa hali si shwari kama wote tunavyojua kwa sababu aliyekusudia
kumuua baba hatujui nini itakuwa hatua yake ya pili.Kwa sasa wewe ndio tegemeo
pekee la baba kupona.Inatakiwa sisi tukulinde wewe kwa kila hali na si wewe
kunilinda mimi.
Kwa hiyo Dr Jason usijali,mimi nitakuwa salama,pale nyumbani pana usalama wa kutosha Kuna walinzi masaa ishirini na nne wa kampuni ya ulinzi,na kama ulivyomsikia mkuu wa polisi aliyefika pale kujua hali ya baba alisema kuanzia usiku huu nyumbani kwetu kutakuwa na askari wenye silaha kwa ajili ya kutulinda,kwa hiyo usihofu kitu.I’ll be ok.Halafu mama akijua kuwa nimelala hotelini tena na mwanaume itakuwa taabu tupu” Akasema Serena na kumfanya Jason aweke kijiko chini akamtazama Serena kama vile ndio kamuona kwa mara ya kwanza.

0 comments:
Post a Comment